Katazo na Marufuku ya Michango mashuleni hapa Nchini ni Kongole kubwa kwa Awamu ya 5 na ya 6. Michango ilikuwa mzigo kwa wananchi

njwanjwanjwa

Member
Jul 28, 2022
8
11
Moja ya Vitu ambavyo Serikali inapaswa kupongeswa navyo katika swala la Elimu ukiachilia mbali miundombinu ya madarasa nk basi huachi kabisa kuipongeza serikali hii inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu pamoja na ile ya mtangulizi wake Hayati John Magufuli kwa katazo na marufuku ya Michango mashukeni kwa kuleta Elimu bure.

Hili nalo lilikuwa ni kichaka cha baadhi ya Wakuu wa shule kujinemeesha kupitia hiyo Michango na mwisho wa siku ilikuwa ni mzigo mkubwa kwa wananchi wa hali ya chini kisomesha watoto wao.

Kwa kufuta Ada pamoja na michango mingine mashuleni hii ninpongezi kubwa sana kwa Serikali yetu.
NB: Japo kuwa serikali ilifanikisha kupiga marufuku na kuzuia michango mashuleni , huu mchango wa chakula Bado ni sugu na mwiba kwa wananchi. Wengi wanashindwa kuumudu na shule za hapa nchini zina viwango tofauti vya mchango huo na umekuwa njia ya kupitisha na kuhalalisha Michango mingine. Huwezi Amani kuna baadhi ya shule mchango wa chakula umefika Hadi Laki moja na usheee!

Chukulia mwananchi wa hali ya chini mwenye watoto watutu (3) shule moja na wote anapaswa kuwalipia mchango wa chakula kila mmoja tsh 100,000 maana yake anapaswa kulipa tsh Laki tatu.

Na mbaya zaidi kwa baadhi ya shule Hata kama mtoto hajala chakula cha shule kwa Mwaka mzima au kwa miaka minne alazimika kulipa gharama zote za Mchango chakula kwa miaka minne amalizapo kidato cha Nne. ( 10,000 x 4)

Wazazi wengi na wadau wengi wa Elimu wanashauli na kupendekeza yafuatayo kuhusu mchango sugu wa chakula kwa baadhi ya shule

1. Serikali iweke fungu la Chakula kwenye ile hela ya Ruzuku (capitation fee) mashuleni ili kutamatisha huu usemi wa Elimu bila malipo maana mchango wa chakula umekuwa mzigo mzito kwa maananchi mlala hoi.

Kama Serikali itaendelea kuruhusu mchango wa chakula mashuleni ulipwe na WAZAZI tafsiri yake ni kwamba Serikali imewapunguzia tu Michango kwa kumlioia mwanafunzi Michango ya Ada ya mitihani, Ada ya Shule (20000) nk na kumwachia mzazi au Mlezi atoe mchango wa 80,000 Hadi 100,000+ kwa ajili ya chakula kwa baadhi ya shule maana si shule zote hapa nchini wanafunzi wanakula chakula.

2. Mchango wa chakula mashuleni ufutwe kama Michango mingine maana ni kichaka cha kuhalalisha na kupitisha michango mingine.

3. Mchango wa chakula uwe hiari katika halmashauri na shule zinazotoa chakula. Wachangishwe wanaokula au waliokula chakula hicho na shule ziwe na data base y’a wanafunzi wanaokula.

4. Kama maanafunzi hajala chakula cha shule kwa term nzima ama mwaka mzima ama kwa kipindi chote alichosoma shule husika basi amalizapo kidato cha Nne asilipishwe mchango wa chakula ambacho hakula.

5. Shule ziruhusu bidhaa ya chakula kuuzwa maeneo ya shule maana kuna baadhi ya shule hupiga stop uuzwaji wa aina yoyote ya chakula hata mihogo, maandazi nk kwenye vipindi vya breakfast na lunch ili iwe kama adhabu ya kuwashindisha njaa wanafunzi na aone umuhimu wa kulipia mchango wa chakula.

Mwisho,
Katika pita pita zangu nimekutana na hii Parent Report form ya mwanafunzi x kwa Mzazi wake Mwaka 2014. Aloo kwa sasa ukiisoma kwenye kipengele cha mengineo kinachohusu Michango na Ada utastaajabu sana. Si chini ya michango 10 mzazi aliyokuwa akichangishwa katika shule husika.

1. Ada: 20,000 /=
2. Mchango wa chakula: 80,000/=
3. *Mchango wa watumishi: 21,000/=
4. Mchango wa Taaluma: 20,000/=
5. *Mchango wa Uzio : 15,000/=
6. Ada ya mtihani pre-national kidato cha pili: 10,000/=
7. Necta kidato cha pili: 10,000/=
8. Pre- National kidato cha Nne: 15,000/=
9. Necta kidato cha Nne. 35,000/=
10. *Mchango ujenzi choo cha watumishi: 15,000/=

Nadhani kwa sasa wazazi wanaowapeleka watoto wao shule hiyo wanafurahia sana kukisekana kwa michango na fedha hizo ambazo wangetoa kulipia michango bila Shaka zinatumika kwenye shughuli nyingine za maendeleo hivo kupiga vita Umasikini. Viva Awamu ya Sita Viva Dkt Raisi Samia Suluhu Hassani unaeishi na kutekeleza ndoto za myangulizi wako hayati JPM kwenye swala la Elimu bure. Kazi Iendeleeeeee!
 

Attachments

  • 557AD051-B40A-4494-A9F8-1F84396DF496.jpeg
    557AD051-B40A-4494-A9F8-1F84396DF496.jpeg
    561.1 KB · Views: 3
Michango mbona ipo kama kawaida, huku Mwabepande wilaya ya kinondoni wanafunzi wa shule ya msingi Kila wiki eti Wana mitihani na Kila mwanafunzi anatakiwa kuja na 1000, darasa moja Lina wanafunzi 120.
 
Michango mbona ipo kama kawaida, huku Mwabepande wilaya ya kinondoni wanafunzi wa shule ya msingi Kila wiki eti Wana mitihani na Kila mwanafunzi anatakiwa kuja na 1000, darasa moja Lina wanafunzi 120.
Mkuu bola huko kwenu huku hela ya mitihani 2000 na mtoto aspoipeleka nafukuzwa shule
 
Mkuu michango Sasa hivi mbona tayari imerudi upya au huko kwenu bado haijafika
Tatizo nyie pia ni fom foo livaz 2020 kutoka kanda ya ziwa ndo mnajitekenya na kucheka wenyewe! Pathetic! Hata enzi ya ngosha michango ilikuwa kama kawaida! Tunawacheki tu hlo swaga lenu la elimu bure!

Huku shule zikiwa hazina walimu, zana za kufundishia na kujifunzia hasa madawati! Mmeongeza na unifom nyingine ya track suit na tishet ambazo imekuwa ni mirad ya walimu! Kwa michango yenu hakuna tofaut na mtu kulipa ada!

Tena mmefanya shule binafsi kupandisha ada maana hao wenye shule wamejua kuwa shule za umma ni kambi za kuzalisha wajinga wapya ambao ndio mtaji wa chama chenu cha ccm!

Mzaz mwenye akili timamu hataman mwanae achaguliwe shule ya umma basi tu hana jinsi maisha tight pritate ni kipengele kwake kwa hyo ada na wiz wa mitihan! Viongoz wao watoto wao hawasomi na wakwetu wao ni nje ya nchi! Au magu si ana watt wa primary? Wanasoma shvle gan hapo geita?
 
Acha kuhusu kuchangisha wanafunzi maana huko bado kupo, lakini pia hata kuwachangisha waalimu kunaendelea.

 
Hiyo michango ya chakula imekuwa kichaka cha upigaji haileti sense shule ni ya kutwa wanafunzi wanatoka eneo hilo hilo mzazi analazimishwa apeleke mahindi gunia moja na nusu kwa term ya kwanza pamoja na maharage debe 2 na hela ya mpishi tsh 60000 kwa hiyo miezi sita.Kwa bahati mbaya bei ya vyakula mwaka huu ni mbaya ni wazazi wachache wanaoweza kumudu kununua mahitaji hayo hali inayopelekea drop out na watoto wengi hawaripoti shuleni kuanza masomo ya kidato cha kwanza kwa wakati au hawafiki kabisa.Mimi naona suala la mtoto kula shuleni iwe ni hiari na si kulazimisha watoto kula maugali hayo ambayo yana low quality na michuzi ya na michuzi ya maharage
 
Back
Top Bottom