Bima ya Afya kwa wote, serikali ifanye yafuatayo kufanikisha

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Jan 2, 2023
230
549
1. Watoto wote wanaozaliwa wakatiwe Bima ya afya kabla ya kuruhusiwa kutoka hospitali

2. Watoto wote wanaoandikishwa kuanza shule lazima wawe na kadi ya Bima ya afya kama ilivyo kwenye sare ya shule na madaftari

3.Mfuko wa Bima ya afya (NHIF) utengeneze mpango maalumu wa kutoa elimu hasa mashuleni kuelezea umuhimu wa Bima ya afya kwa kutumia mifano halisi ya watu wanaokufa kwa kukosa huduma bora za afya

Tangu tupate uhuru nchi zetu hizi zilizotawaliwa zimeshindwa kabisa kubuni vitu vyake na kuvisimamia

Karibu project nyingi, program nyingi kwenye sekta mbali mbali hususani hapa kwetu Tanzania zinafadhiliwa na wazungu na viongozi wetu wanachekelea na kusifu hadi imefikia hatua wanashindana na kujisifu kwa kutambiana nani kafanikisha misaada mingi kwa nchi

Sekta ya afya inaongoza kwa kuwa na project na misaada mingi kutoka nje kiasi kwamba ikakata tu Taifa lazima itikisike kwa kushindwa kumudu gharama za afya. Hii yote ni kwasababu serikali imebweteka na haitaki kuwekeza huko

Mpango wa Bima ya afya kwa wote umesemwa na wanasiasa wamehubiri lakini nikama wanajiongelesha tu kwasababu watanzania hawajajengewa misingi ya kutambua na kuthamini umuhimu wa Bima. Wao wanachojua ni kulalamika pale atakapoenda hospitali halafu gharama zimshinde

Ili upate mass support kwenye jambo lolote ni lazima uanze na kutengeneza "mind set" za hao walengwa walipokee kwa mikono miwili. Katika kujenga mind set kuna mahali utalazimika kutumia akili nyingi na wakati mwingine mchanganyiko wa akili na nguvu

Ili Bima ya afya iwe endelevu inabidi tuanze kuwekeza kwa watoto wanaozaliwa na vijana waliopo mashuleni kwasasa

Hawa wanatakiwa kujengewa uelewa wa umuhimu wa kuwa na Bima kwa namna zote; kwa kutumia akili kuwashawishi na kujenga uelewa na matumizi ya nguvu kulazimisha pale inapobidi

Ni ajabu sana eti NHIF wameanzisha kifurushi cha toto afya halafu imekuwa "hiyari" kwa wazazi! Tunatengeneza Taifa la kubembeleza kwa kila kitu hadi kwenye afya zao???

Kwa mfano; NHIF sera yao ya toto afya kwasasa hasa kwa wanafunzi ni kwamba inatakiwa wanafunzi wote wasiokuwa na Bima wawe tayari kujiunga ndipo shule hiyo itaingizwa kwenye mpango wa toto afya kwa kuingiza wanafunzi wote bila kuacha hata mmoja. Yaani kama shule ina wanafunzi 700 wasio na Bima ni lazima wote wawe tayari kuchangia Tsh.54,500/_ kwa mwaka ndipo shule husika itaingizwa kwenye mfumo ila wasipofikia idadi (kwa mfano 20 wakigoma) wote wataachwa!

Mtazamo wangu katika hili naona kuwa ingetungwa sheria maalumu kwa watoto wote wanaozaliwa kabla mzazi hajaruhusiwa kwenda nyumbani ahakikishe amekamilisha taratibu zote za kumkatia Bima mtoto wake. Yaani Bima ikikamilika ndipo mzazi aruhusiwe kutoka kwenye geti la hospitali. Semina wanazopewa wajawazito wakati wanahudhuria kliniki mojawapo iwe elimu kuhusu Bima ya afya. Mahitaji wanayoambiwa kuaandaa, moja wapo iwe ni fedha ya kukata Bima ya afya kwa mtoto anayetarajia kuzaliwa

Kama imewezekana kutekeleza sera ya wazungu ya kutaka mwanamke na mwanaume waambatane kliniki siku ya kwenda kuanza kliniki ya mimba, hili la Bima ya afya linashindikana nini?

Kwa upande wa shuleni, kwasasa michango na ada vimefutwa kwa ngazi zote za elimu na serikali inajigamba mtaani.

Hata hivyo wanajigamba pasipokujua wanaandaa kizazi ambacho hakitakuwa "responsible"! Kizazi cho hoya hoya ndicho kinachoaandaliwa hapa

Siku hizi shule za serikali za kawaida kwenye darasa la wanafunzi 70 unakuta walioko serious na shule na wanazingatia masomo vizuri kwa kuwa na vitendea kazi vinavyowahusu kama daftari, kalamu, sare safi na viatu nadhifu wanakuwa 20! Zaidi ya robo tatu hawako responsible na hauwafanyi chochote kwasababu kisingizio ni "mazingira magumu" ya wazazi

Lakini hao hao wakiumwa familia nzima itachangishana kwa dharula kutafuta pesa ya matibabu. Hapa serikali ingetunga sheria kwamba kila mtoto anayaandikishwa darasa la kwanza sharti awe na kadi ya Bima ya NHIF inayofanya kazi kwa mzazi kulipia Tsh.54,500/_ kwa mwaka. Hii haishindikani

Utaratibu huu ukifanyika na watoto wakawa wanaelimishwa mara kwa mara, wakishakuwa wakubwa hakuna mtu atawasukuma kulipia kadi zao za Bima. Hakuna mtu atawalazimisha kukata Bima kwa ajili ya watoto wao

Zamani wakati huduma za NHIF zinasua sua wafanyakazi waliongoza kwa malalamiko na matusi mengi kwa mfuko wa Bima kwamba wanakatwa hela za bure tu ni bora waache kukatwa wagharamikie matatibabu wenyewe

Lakini kwasasa baada ya huduma za NHIF kuboreshwa sidhani kama kuna mfanyakazi atasimama na kutoa kejeli kwamba Bima ya afya haina msaada

Mimi nilianza kuiheshimu siku ambayo mzee wangu alilazwa pale MOI na akafanyiwa upasuaji uliogharimu karibu mil.2 na gharama zote zikalipwa na NHIF. Huwa naikumbuka siku hii hasa kutokana na mazingira ya kipato changu na cha wanaonizunguka. Kulikuwa hamna namna tungeweza kupata kiasi hicho cha fedha kwa haraka!

Wachangiaji wa Bima ya afya wakiwa wengi, serikali itapata uwezo wa kuboresha huduma za afya kwa kuanzisha hata viwanda vya madawa na hatimaye kuondokana na utegemezi wa wafadhili ambao mara zote wanatoa ufadhili wakiwa wamelenga kupata faida fulani
 
Hapana sio kweli kuwa kama shule ina watoto 700 ni lazima wote wawe tayari kukatiwa bima ndio shule iruhusiwe!! Wamesema hata wakiwa 100 ambao wako tayari kulipia bima, basi watakatiwa tu.

Kuhusu bima ya afya kwa watoto serikali ingetumia tu amri, kuwa kuanzia shule ya msingi hadi sekondari ni lazima mtoto awe na bima, iingizwe tu kwenye gharama za shule.

Na hawa ambao hawajaanza shule chini ya miaka 5, iwe hakuna dirisha la CASH, kwenye hospital zote za serikali, iwe ni bima tu. WATANZANIA, bila shuruti ni wagumu kutii!!!

Leo wanapiga kelele hasa juu ya bima ya watoto, kuondolewa, wakati ni aibu nchi nzima ni watoto laki 210 tu ndio wenye bima kati ya watoto zaidi ya milioni 15!!
 
Shida si watoto kukatiwa bima, shida hiyo bima ni kias gani,? Kuna wananchi wanaishi chini ya dola 2.

Waanze kulegeza kamba, maisha yawe mazuri(nafuu) kwa watanzania wa chini kabisa.
 
Back
Top Bottom