Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,890
- 2,777
hii habari nimeisikia kwa mbali ikisomwa toka vichwa vya habari magazetini. Nadhani ni gazeti la uhuru. Kamteua shehe mkuu na kadhi nadhani. Hii ina maana mfumo wa dini ya kiislam unatambulika rasmi zanzibar?
usidhani ni kweli habari hiyo. Kwani ulikuwa hujui hilo. Zanzibar wana Mufti na kadhi Mkuu yaani wao wana mahakama ya kadhi ambayo inashughulikia kesi zinahusu masuala ya dini ya Kiislamu kama ndoa, mirathi, talaka na kadhalika
Rais anateua viongozi wa dili ili likitokea jambo lolote kati ya dini na serikali viongozi hawa watakua monitered na serikali. Naamini mufti atakuwa anasikiliza kila anachokitaka rais coz ndo amemmteua.RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein ameteua viongozi wa dini ya Kiislamu akiwemo Mufti Mkuu pamoja na Kadhi Mkuu wa Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu, Saleh Omar Kabhi ameteuliwa kuwa Mufti Mkuu wa Zanzibar ambaye anachukua nafasi ya Harith bin Khelef aliyefariki miaka miwili iliyopita nchini India akitibiwa.
Sheikh Kabhi ni kiongozi wa Baraza la Maulamaa Zanzibar, lenye uwezo wa kutoa kauli ya mwisho kuhusu masuala ya dini ya Kiislamu kwa Zanzibar.
Kabla ya uteuzi huo mpya, alikuwa Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar ambaye Makao Makuu yake yalikuwa katika Kisiwa cha Pemba.
Aidha, Rais Dk. Shein amemteua Sheikh Khamis Haji Khamis kuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar.
Kabla ya uteuzi huo, alikuwa akikaimu nafasi hiyo kwa muda wa miaka minne kutokana na kifo cha Kadhi Mkuu Mussa Makungu.
Pia Sheikh Hassan Othman Ngwali ameteuliwa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar.
Mufti pamoja na Kadhi Mkuu ndiyo viongozi wa ngazi za juu katika masuala ya mambo ya Kiislamu ikiwemo kutoa taarifa za kuandama kwa mwezi pamoja na kutoa fatwa katika masuala
yote yanayohusu mambo ya Kiislamu.
Zanzibar ambayo asilimia 95 ya wakazi wake ni wafuasi wa dini ya Kiislamu ingawa sio nchi ya
Kiislamu, imekuwa ikitegemea viongozi hao akiwemo Mufti na Kadhi Mkuu katika kuyapatia fatwa mambo mbalimbali yanayohusu dini ya Kiislamu ikiwemo mirathi na ndoa.
Kwa hisani ya Habari Leo
RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein ameteua viongozi wa dini ya Kiislamu akiwemo Mufti Mkuu pamoja na Kadhi Mkuu wa Zanzibar.