Rais wa Zanzibar awateua Mufti na Kadhi Mkuu wa Zanzibar

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,770
2,544
hii habari nimeisikia kwa mbali ikisomwa toka vichwa vya habari magazetini. Nadhani ni gazeti la uhuru. Kamteua shehe mkuu na kadhi nadhani. Hii ina maana mfumo wa dini ya kiislam unatambulika rasmi zanzibar?
 
RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein ameteua viongozi wa dini ya Kiislamu akiwemo Mufti Mkuu pamoja na Kadhi Mkuu wa Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu, Saleh Omar Kabhi ameteuliwa kuwa Mufti Mkuu wa Zanzibar ambaye anachukua nafasi ya Harith bin Khelef aliyefariki miaka miwili iliyopita nchini India akitibiwa.

Sheikh Kabhi ni kiongozi wa Baraza la Maulamaa Zanzibar, lenye uwezo wa kutoa kauli ya mwisho kuhusu masuala ya dini ya Kiislamu kwa Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huo mpya, alikuwa Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar ambaye Makao Makuu yake yalikuwa katika Kisiwa cha Pemba.

Aidha, Rais Dk. Shein amemteua Sheikh Khamis Haji Khamis kuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huo, alikuwa akikaimu nafasi hiyo kwa muda wa miaka minne kutokana na kifo cha Kadhi Mkuu Mussa Makungu.

Pia Sheikh Hassan Othman Ngwali ameteuliwa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar.

Mufti pamoja na Kadhi Mkuu ndiyo viongozi wa ngazi za juu katika masuala ya mambo ya Kiislamu ikiwemo kutoa taarifa za kuandama kwa mwezi pamoja na kutoa fatwa katika masuala
yote yanayohusu mambo ya Kiislamu.

Zanzibar ambayo asilimia 95 ya wakazi wake ni wafuasi wa dini ya Kiislamu ingawa sio nchi ya
Kiislamu, imekuwa ikitegemea viongozi hao akiwemo Mufti na Kadhi Mkuu katika kuyapatia fatwa mambo mbalimbali yanayohusu dini ya Kiislamu ikiwemo mirathi na ndoa.

Kwa hisani ya Habari Leo
 
usidhani ni kweli habari hiyo. Kwani ulikuwa hujui hilo. Zanzibar wana Mufti na kadhi Mkuu yaani wao wana mahakama ya kadhi ambayo inashughulikia kesi zinahusu masuala ya dini ya Kiislamu kama ndoa, mirathi, talaka na kadhalika
 
Nchi inayoendeshwa kwa mazoea. Katiba inasemaje kuhusu serikali na dini? Kwenye makatasi bado Zanzibar inaosomeka kama 'secular state'. Sasa huu uteuzi wa kiongozi wa dini unaiweka wapi huo u-secular?
 
Kuna memba wa JF aliwahi kuuliza; kama Zanzibar ni Islamic State. Mimi pia nimeshangazwa na habari hii?

Katiba ya Zanzibar inasema kuwa ni nchi ya Kiislamu? Kama Katiba ya TZ inatamka kuwa Jamhuri ya Muungano haina dini, Je, Zanzibar si sehemu ya Jamhuri ya Muungano ya TZ? Hapo kuna uvunjaji wa Katiba na Mh Pinda ajiandae kujibu kwenye nxt session ya Bunge.
CUF,BAKWATA na Masheikh kwa unafiki watakaa kimya.Mh Tundu Lisu akiuliza,watamtukana,Maaskofu wakisema watadhihakiwa!

Nasubiri kejeli za MS & co
 
usidhani ni kweli habari hiyo. Kwani ulikuwa hujui hilo. Zanzibar wana Mufti na kadhi Mkuu yaani wao wana mahakama ya kadhi ambayo inashughulikia kesi zinahusu masuala ya dini ya Kiislamu kama ndoa, mirathi, talaka na kadhalika

basi sioni ubaya wa kuwa na hiyo kitu huku bara kwni sijasikia ubaya wowote kuhusu hizo taasisi. Ila kama alivyosema jk, waanzishe kwa gharama zao kwani huku bara sio zanzibar. Tena huku wakristo ni wengi kuliko waislam
 
RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein ameteua viongozi wa dini ya Kiislamu akiwemo Mufti Mkuu pamoja na Kadhi Mkuu wa Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu, Saleh Omar Kabhi ameteuliwa kuwa Mufti Mkuu wa Zanzibar ambaye anachukua nafasi ya Harith bin Khelef aliyefariki miaka miwili iliyopita nchini India akitibiwa.

Sheikh Kabhi ni kiongozi wa Baraza la Maulamaa Zanzibar, lenye uwezo wa kutoa kauli ya mwisho kuhusu masuala ya dini ya Kiislamu kwa Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huo mpya, alikuwa Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar ambaye Makao Makuu yake yalikuwa katika Kisiwa cha Pemba.

Aidha, Rais Dk. Shein amemteua Sheikh Khamis Haji Khamis kuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huo, alikuwa akikaimu nafasi hiyo kwa muda wa miaka minne kutokana na kifo cha Kadhi Mkuu Mussa Makungu.

Pia Sheikh Hassan Othman Ngwali ameteuliwa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar.

Mufti pamoja na Kadhi Mkuu ndiyo viongozi wa ngazi za juu katika masuala ya mambo ya Kiislamu ikiwemo kutoa taarifa za kuandama kwa mwezi pamoja na kutoa fatwa katika masuala
yote yanayohusu mambo ya Kiislamu.

Zanzibar ambayo asilimia 95 ya wakazi wake ni wafuasi wa dini ya Kiislamu ingawa sio nchi ya
Kiislamu, imekuwa ikitegemea viongozi hao akiwemo Mufti na Kadhi Mkuu katika kuyapatia fatwa mambo mbalimbali yanayohusu dini ya Kiislamu ikiwemo mirathi na ndoa.

Kwa hisani ya Habari Leo
Rais anateua viongozi wa dili ili likitokea jambo lolote kati ya dini na serikali viongozi hawa watakua monitered na serikali. Naamini mufti atakuwa anasikiliza kila anachokitaka rais coz ndo amemmteua.
 
RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein ameteua viongozi wa dini ya Kiislamu akiwemo Mufti Mkuu pamoja na Kadhi Mkuu wa Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu, Saleh Omar Kabhi ameteuliwa kuwa Mufti Mkuu wa Zanzibar ambaye anachukua nafasi ya Harith bin Khelef aliyefariki miaka miwili iliyopita nchini India akitibiwa.

Sheikh Kabhi ni kiongozi wa Baraza la Maulamaa Zanzibar, lenye uwezo wa kutoa kauli ya mwisho kuhusu masuala ya dini ya Kiislamu kwa Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huo mpya, alikuwa Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar ambaye Makao Makuu yake yalikuwa katika Kisiwa cha Pemba.

Aidha, Rais Dk. Shein amemteua Sheikh Khamis Haji Khamis kuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huo, alikuwa akikaimu nafasi hiyo kwa muda wa miaka minne kutokana na kifo cha Kadhi Mkuu Mussa Makungu.

Pia Sheikh Hassan Othman Ngwali ameteuliwa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar.

Mufti pamoja na Kadhi Mkuu ndiyo viongozi wa ngazi za juu katika masuala ya mambo ya Kiislamu ikiwemo kutoa taarifa za kuandama kwa mwezi pamoja na kutoa fatwa katika masuala
yote yanayohusu mambo ya Kiislamu.

Zanzibar ambayo asilimia 95 ya wakazi wake ni wafuasi wa dini ya Kiislamu ingawa sio nchi ya
Kiislamu, imekuwa ikitegemea viongozi hao akiwemo Mufti na Kadhi Mkuu katika kuyapatia fatwa mambo mbalimbali yanayohusu dini ya Kiislamu ikiwemo mirathi na ndoa.

Kwa hisani ya Habari Leo

Raisi ambaye ni kiongozi mkuu wa serikali anawateua viongozi wakuu wa dini mufti na kadhi.

Kwakuwa mtoa pesa ndiye huchagua wimbo basi hapo ni kwamba dini imekubali kuingia kwenye mfuko wa serikali, watakuwa wanatenda na kutekeleza matakwa ya serikali na sio mahitajio ya dini husika.
 
Hii miaka mitano mpaka tuimalize tutaona, kusikia pamoja na kushuhudia mambo mengi sana.
 
Asiyejua maana usimwambie maana. ZANZIBAR IS ISLAMIC STATE. Mukitaka musitake. Tunasubiri katiba mpya ndipo mtakapojua mbivu na mbichi.
 
Nilikuwa sipati picha kamili ya maana ya kuwa na Mahakama ya Kadhi, kwa tukio la Rais wa Zanzibar kuteua viongozi wa dini sasa nimeelewa maana ya mahakama hiyo.

Kwa Zanzibar kutokana na idadi kubwa ya Waumini wa Kiislamu inafanyika hivyo, lakini kwa huku bara naona kama ikifanyika hivyo inaweza kusababisha migongano fulani kutokana na idadi kubwa raia wenye dini tofauti.

Dk. Shein ateua viongozi wakuu wa kidini Zanzibar

RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein ameteua viongozi wa dini ya Kiislamu akiwemo Mufti Mkuu pamoja na Kadhi Mkuu wa Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu, Saleh Omar Kabhi ameteuliwa kuwa Mufti Mkuu wa Zanzibar ambaye anachukua nafasi ya Harith bin Khelef aliyefariki miaka miwili iliyopita nchini India akitibiwa.

Sheikh Kabhi ni kiongozi wa Baraza la Maulamaa Zanzibar, lenye uwezo wa kutoa kauli ya mwisho kuhusu masuala ya dini ya Kiislamu kwa Zanzibar. Kabla ya uteuzi huo mpya, alikuwa Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar ambaye Makao Makuu yake yalikuwa katika Kisiwa cha Pemba. Aidha, Rais Dk. Shein amemteua Sheikh Khamis Haji Khamis kuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar. Kabla ya uteuzi huo, alikuwa akikaimu nafasi hiyo kwa muda wa miaka minne kutokana na kifo cha Kadhi Mkuu Mussa Makungu. Pia Sheikh Hassan Othman Ngwali ameteuliwa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar.

Mufti pamoja na Kadhi Mkuu ndiyo viongozi wa ngazi za juu katika masuala ya mambo ya Kiislamu ikiwemo kutoa taarifa za kuandama kwa mwezi pamoja na kutoa fatwa katika masuala yote yanayohusu mambo ya Kiislamu.

Zanzibar ambayo asilimia 95 ya wakazi wake ni wafuasi wa dini ya Kiislamu ingawa sio nchi ya Kiislamu, imekuwa ikitegemea viongozi hao akiwemo Mufti na Kadhi Mkuu katika kuyapatia fatwa mambo mbalimbali yanayohusu dini ya Kiislamu ikiwemo mirathi na ndoa.
 
Nilikuwa sijapata picha nini kinajilia kwenye Mahakama ya kadhi, kwa utaratibu huu kama Rais anateua viongozi wa dini kwa vyo vyote serikali inawajibika nao ikiwa ni pamoja na posho na gharama nyingine za uendeshaji wa chombo hiki.
 
Je, ikitokea Rais akawa mkristu kisha akamteua Mchungaji wa Kulutheri kuwa Shekh mkuu waislam watakubali?!!!
 
Kwani wewe ulifikiri inakuwaje kuhusu mahakama ya kadhi? Kadhi ni alternative ya hakimu kwenye serikali secular. Kwa ufupi Uislam ni dini ambayo doctrine yake haiwezi kutenganishwa na mfumo wa kiserikali. Mfumo wa kimagharibi ya separation of Church and State si mfumo sahihi kuendesha mambo yao ndio maana wanalalamika sana kwa kuuita mfumo Kiristo.

Lakini sasa hiyo haiwezekani hapa Tanzania bara; na hata huko Zanzibar ni makosa makubwa sana kwa serikali inayojiita secular ya huko Zanzibar kuendekeza hii mifumo dini kama kuteua kadhi au mufti. Sema tu hakuna namna ya kurekebisha hii hali na watu wasio waislam wanaoishi Zanzibar japo ni wachache lakini wamejifunza kuwa wavumilivu kushi wakiwa wamezungukwa na maisha kandamizi ya kidini;

Somo tunalojifunza hapa ni kutowapa nafasi wale wanaotaka kututawala kwa misingi ya kidini kama hawa wa mahakama ya kadhi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom