Rais Samia: Wizara ya Afya ituambie tuendelee kuvaa barakoa au tupumzike

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Rais ameiagiza wizara hiyo kufanya tathmini ya hali ya ugonjwa wa UVIKO-19 nchini na kutoa utaratibu kama bado kuna haja ya wananchi kuendelea kutumia barakoa.

Amesema “Inaonyesha watu wamechoka nazo, niwaombe sasa Wizara ya Afya waangalie mwenendo huu tunaokwenda nao, lakini watathmini hali ilivyo halafu watuambie tuendelee kuwa nazo au kwa muda tupumzike.”

Hata hivyo, Rais Samia amewataka wale ambao hawajachanja wachanje kwa hiari ili kuweza kuwa kwenye hali nzuri ya kuzuia maambukizi ya janga hilo kwasababu bado ugonjwa upo na watu wajifunze kuishi nao.
 
Hata hivyo, Rais Samia amewataka wale ambao hawajachanja wachanje kwa hiari ili kuweza kuwa kwenye hali nzuri ya kuzuia maambukizi ya janga hilo kwasababu bado ugonjwa upo na watu wajifunze kuishi nao.
Hiyo dawa haija expirre tu!
 
Rais ameiagiza Wizara hiyo kufanya tathmini ya hali ya Ugonjwa wa UVIKO-19 nchini na kutoa utaratibu kama bado kuna haja ya wananchi kuendelea kutumia Barakoa.

Amesema “Inaonyesha watu wamechoka nazo, niwaombe sasa Wizara ya Afya waangalie mwenendo huu tunaokwenda nao, lakini watathmini hali ilivyo halafu watuambie tuendelee kuwa nazo au kwa muda tupumzike,”

Hata hivyo, Rais Samia amewataka wale ambao hawajachanja wachanje kwa hiari ili kuweza kuwa kwenye hali nzuri ya kuzuia maambukizi ya janga hilo kwasababu bado ugonjwa upo na watu wajifunze kuishi nao.
Ni yeye tu ndiyo anazivaa
Kwa hiyo ni bora aulize wizara kama aendelee kuvaa au la!
Sema ni zuga hiyo, anatafuta namna ya kuacha kuyavaa
Sisi wananchi hatujawahi kuyavaa
Hiyo ilikuwa nguvu ya JPM
 


Tunatishana Sana Ndugu Zangu

Vigogo Wafa, Vigogo Wapukutika Ni Uzushi Mtupu
Tumtangulize Mungu Mbele, Tutaishinda COVID 19 Kwa Maombi
Natangaza Ijumaa, Jumamosi Na Jumapili
Tutamshukuru Mungu Kuishinda COVID 19





BY MZILANKENDE Mnyago
 
Maana halisi ya siasa ni unafiki,pamoja na wizara ya afya kusema corona bado ipo ila baada ya tamko hili hawawezi kusema tuvae barakoa.
 
Ni yeye tu ndiyo anazivaa
Kwa hiyo ni bora aulize wizara kama aendelee kuvaa au la!
Sema ni zuga hiyo, anatafuta namna ya kuacha kuyavaa
Sisi wananchi hatujawahi kuyavaa
Hiyo ilikuwa nguvu ya JPM
Mwisho kaona aibu mwenyewe, maana hakuna anae vaa zaidi yake , ana tia hadi aibu , 90% hawa Vai yeye anang'ang'ania utazani COVID 19 imeanzia Tanzania.
 
Mh. Ummy sijui bado anaona ukakasi wakwe wa watu kushiriki NHIF!
Dah ila katika siku ambayo Mh. Ummy aliongea kauli mbaya zisizokuwa na ushahidi ni siku anaelezea issue za NHIF. Ni bora angenitafuta nimpige shule ya actuarial Science kidogo aone mathematical modeling inavyoweza kuonesha uzembe wa uongozi wa NHIF. N siyo kweli kabisa eti wakwe au wastaafu wanaugua sana, sehemu kubwa forgeries ndizo zimeufikisha mfuko hapo ulipo. Watendaji wa NHIF walimdanganya. Kwa nini asigetafuta hata independent opinion toka kwa watalaamu hata wa UDSM, IFM, Mzumbe au ile institute ya insurance wamtemee cheche za uhai vs kukaukiwa kwa mfuko? Nashauri ukiwa kiongozi kabla ya tamko ni muhimu sana kuseek opinion na ikiwezekana unakuwa na timu yako 24/7 kwa ushauri.
 
Rais anakosea kitu, wenye maamuzi ya mwisho sio wizara ya afya, ni nchi wahisani, awaambie wazungu wananchi wake wanaojitokeza pale akiwepo wakiwa wamevaa barakoa sasa wamechoka kuzivaa.
 
Watu wenye imani juu ya Bwana Yesu Kristo hutambua ya kwamba juu uwepo wa nguvu ya Roho Mtakatifu wala hakuna jambo lolote lile baya ambalo litaikumba dunia.

Lakini siku nguvu hii kuu ikisitishwa kwa mamlaka ya mbinguni basi kila aina ya uovu ulikusudiwa kwa hila za shetani utafanyika juu ya sura ya nchi. Baragumu Saba zinaisubiri dunia hii chini ya utawala wa Ibilisi, na wakati na majira yake yamekaribia mno.

Beware.
 
Back
Top Bottom