Rais Samia: Tuendelee kuchukua tahadhari dhidi ya uwezekano wa uwepo wa mvua la El Nino nchini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Kilele cha Mbio za mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Baba Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Wiki ya Vijana kitaifa katika Uwanja wa Kwaraa Babati, Mkoani Manyara leo tarehe 14 Oktoba, 2023.


View: https://www.youtube.com/live/SmEA1CXV-WI?si=KH-Yb-X6fnJvAcfW

PROF. NDALICHAKO, WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU – KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU

Naomba niwapongeze vijana wetu sita wakimbiza mwenge wa uhuru kitaifa 2023 ambao waliongozwa na Cde. Abdallah Shaibu Kaimu. Vijana hawa shupavu, wazalendo na mahiri wameukimbiza Mwenge kilomita 27,437.82 katika mikoa 31 na halmashauri 195 na wamefanya kazi hi kwa siku 196 bila kupumzika.

Leo taifa letu la Tanzania limetimiza miaka 24 tangu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipotutoka. Wakati wa uhai wake alijitoa sana katika kulikomboa taifa letu lakini pia alishiriki katika ukombozi wa mataifa mengine ya bara la Afrika. Alijenga na kusimamia misingi imara ya umoja, amani, upendo na mshikamano katika taifa letu.

Watanzania tutaendelea kumkumbuka Baba wa Taifa na kuenzi falsafa na maono yake kwa vitendo na kurithisha kwa vizazi vijavyo. Mbio za 2023 zilizinduliwa Aprili 1, 2023.

Miti 5,296,912 imepandwa
Kupitia mwenge wa uhuru, jumla ya miti 5,296,912 imepandwa. Aidha, kupitia halmashauri na kampeni ambayo ni maelekezo ya serikali yako Mh. Rais, ambapo kila halmashauri inatakiwa kupanda mili 1,500,000, jumla ya miti 232,679,875 imepandwa nchini kote. Mh. Rais nikuhakikishie mbio za Mwenge wa Uhuru zitaendelea kufuatilia miti iliyopandwa kwa miaka mitano mfululizo ili kuhakikisha kwamba inatunzwa na inakuwa kwa ajili ya kuleta mabadiliko chanya ya tabianchi na uhifadhi endelevu wa mazingira yetu.

Miradi 1,424 imezinduliwa
Mafanikio mengine yaliyopatikana ni ukaguzi na uzinduzi wa miradi, ambapo jumla ya miradi 1,424 yenye thamani ya 5,287,212,850,000 imezinduliwa au kuwekewa jiwe la msingi. Na Mh. Rais, na miradi hii ambayo imepitiwa na Mwenge ni sehemu tu ya miradi mingi mikubwa ambayo imekuwa ikitekelezwa na serikali yako makini ya Awamu ya Sita.

Miradi iliyokaguliwa ilikuwa katika sekta ya afya, elimu, maji, barabara, uwezeshaji wa wananchi kiuchumi, na kwakweli huko ambapo miradi imekaguliwa wananchi wana shukrani kubwa kwako Rais kwa kazi ya kupeleka maendeleo kwa kila kona ya nchi.

Wananchi 46,835 walijitokeza kupima VVU
Katika mafanikio mengine kwenye jitihada za kupambana na UKIMWI, jumla ya wananchi 46,835 walijitokeza kupima VVU kwa hiari, na ambapo watu 1,884 walibainika kuwa na VVU na wote washirika hao walipewa ushauri nasaha na kusajiliwa vituo vya afya ili kupata huduma stahiki.

Watu 16,832 walijitokeza kupima Malaria
Kwa upande wa Malaria, jumla ya watu 16,832 walijitokeza kupima na kati yao watu 1,032 sawa na 6.1% waliopimwa walibainika kuwa na vimelea vya malaria.

Lita 3,979 za damu zapatikana
Watanzania walihamasishwa kujitolea damu safi na salama ambapo lita 3,979 zilipatikana. Damu hiyo inayopatikana inatunzwa katika benki yetu ya dam una itatumika kuleta matumaini ya kuishi kwa Watanzania wenye uhitaji.

Miradi 7 yenye thamani ya 1,855,828,000 yakataliwa
Kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa, mbio za Mwenhge wa Uhuru ziliendelea kutoa elimu kwa Watanzania kuhusu Rushwa na athari zake na katika miradi iliyokaguliwa kulibadilika dosari ndogondogo lakini Mwenge ulivyokuwa unakuta dosari hizi ulikuwa unatoa maelekezo, inarekebishwa na kuruhusu miradi ile iendelee kutoa huduma kwa wananchi.

Kuna miradi 7 yenye thamani ya 1,855,828,000 yakataliwa na Mwenge wa Uhuru. Nyaraka za miradi iliyokataliwa Mh. Rais, imekabidhiwa kwa TAKUKURU na zitakabidhiwa kwako rasmi leo hii na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru.

SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Maadhimisho haya tumekuwa tunafanya kila mwaka yakiambatana na kumbukumbu ya mwalimu JK Nyerere, na leo hii inatimia miaka 24 tangu kifo chake.

Vijana ndio nguzo na nguvu kazi ya ujenzi wa taifa lolote lile, na hasa tunavyodhamiria kujenga taifa linalojitegemea. Karibu 35% ya watanzania ni vijana, na ndio tegemeo kuu la nguvu kazi ya ujenzi wa taifa.

Tunataka kujenga taifa lenye vijana waadilifu, wachapakazi na wazalendo ili wachangie kikamilifu katika ujenzi wa taifa lao. Hivi tunavyozungumza, ujenzi wa vyuo vya VETA 64 unaendelea nchini, na vingine 50 vitajengwa. Tunataka kila wilaya iwe na chuo cha VETA.

Serikali inaweka nguvu kubwa katika maeneo mengi ili yalete ajira kwa vijana.

Zaidi ya 95% mabadiliko ya tabia nchi yanachangiwa na shughuli za kibinadamu, na kusababisha athari kubwa kama mafuriko, ukame, joto na kupanda kwa kina cha bahari.

Kwa upande wetu, hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kutunusuru, na tuendelee kumuomba atuhifadhi. Tutunze mazingira yetu, tuhifadhi vyanzo vya maji na kupanda miti. Kila wilaya inatakiwa kupanda na kukuza miti 1.5M kila mwaka.

Kulikuwa na tuzo ya upandaji miti, waliopanda mingi na kuitunza walikuwa wanapata zawadi. Naomba tuzo hizo zirudi.

Suala la ufugaji wa kuhamahama tuliangalie, tujikite kwenye ufugaji wa kisasa. Pia, tunataka wananchi watumie nishati safi na rafiki ili uchomaji wa mkaa uishe.

Nipongeze kampeni za kutunza mazingira zinazoendeshwa sehemu mbalimbali.

Niwaase watanzania na wanamanyara kuchukua tahadhari dhidi ya wagonjwa wa UKIMWI. Niombe kila mmoja awe mlinzi wake mwenyewe.

Pia, umuhimu wa lishe bora katika kuzalisha nguvu kazi ya Taifa. Bado hali ya lishe nchini sio nzuri, 28% ya wanawake wenye umri wa kuzaa wana upungufu wa damu na 32% ya wana uzito uliozidi. Udumavu ni 30% ni kiashiria kibaya cha lishe.

Tatizo la udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 ni 30%, uzito pungufu ni 12%, ukondefu 3% na uzito uliozidi ni 4%. Mikoa ya Iringa 56.9%, Njombe 50.4%, Rukwa 49.8%, Geita 38.6%, Ruvuma 35.6%, Kagera 34.3%, Simiyu 33.2%, Tabora 33.1%, Katavi 32.2%, Manyara 32% , Songwe 31.9% na Mbeya 31.5% inaongoza kwa lishe duni.

Tuendelee kuchukua tahadhari dhidi ya uwepo wa mvua kubwa hasa mikoa ya kanda ya ziwa na pwani wa bahari ya hindi. Matangazo haya yanatoleww, lakini huoni hadhari inayochukuliwa, bado mitaro ya maji imejaa takataka. Niwaombe wasimamizi wa miji wahimize usafi wa maeneo hayo.

Nidhamu na uadilifu wa watumishi wa umma katika kuhudumia wananchi, tumekuwepo na malalamiko ya wananchi juu ya uwepo wa lugha chafu, kucheleweshwa huduma au kudaiwa rushwa kwa watumishi wa serikali. Wakuu wa mkoa na wilaya mlibebe ipasavyo.

Nitoe wito kwa watanzania wote kuongeza ushirikiano kwa Mamlaka ya kudhibiti dawa za kulevya na vyombo vingine vya dola katika mapambano dhidi ya biashara na matumizi ya dawa za kulevya ili tuokoe vijana wetu.
 
Uhuru tulishapata na sasa una zaidi ya miaka 60

Ni bora Mbio za Mwenge wa Uhuru zibadilishwe na sasa ziitwe Mbio za TAKUKURU na Wakimbiza Mwenge wawe JKT na Maafisa wa TAKUKURU

Nawatakia Sabato Njema 😄
 
Mlioko frontline tupeni update kinachojiri kwenye battlefield kati ya ishmail na bro wake isaka.
 
Back
Top Bottom