Rais Samia ni kiongozi mwenye misuli ya Uongozi ya kustahimili Vishindo vya aina zote

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,338
9,766
Ndugu zangu Watanzania,

Rais Samia apewe sifa zake, apongezwe na kupewa moyo, afarijiwe na kuungwa mkono. Apewe ushirikiano na kuendelea kuaminiwa. Kwa hakika, Rais Mama Samia ni kiongozi mwenye misuli ya uongozi. Ni kiongozi mwenye kifua imara na madhubuti, jasiri na mkakamavu. Ni kiongozi mwenye subira na uvumilivu wa kiwango cha hali ya juu sana. Hana wa kufanana naye wala kufananishwa naye. Hana wa kulingana naye wala kulinganishwa naye. Ni Mama Samia mmoja tu tuliye naye na atakayeendelea kuwepo hapa nchini. Hakuna awezaye kubeba abebayo katika kifua na moyo wake katika kuliongoza Taifa letu.

Misuli ya uongozi aliyo nayo Rais Samia ni imara na madhubuti sana. Yenye uwezo wa kuhimili vishindo vya aina zote vya uzito wa aina yoyote ile. Ndio maana unaona namna anavyomaliza na kutatua mambo mbalimbali makubwa na mazito kwa hali ya utulivu wa hali ya juu sana. Huwezi ukamuona wala kumsikia Rais Samia akiongea kwa kukurupuka, jazba, au mihemuko pasipo mpangilio wa kimantiki na kihoja. Ni kiongozi ambaye wakati wote huzungumzia mambo kwa utulivu, busara, hekima, na umakini wa hali ya juu sana.

Rais Samia hanaga kule kujikwaa kimaneno akiwa jukwaani. Huwezi ukasikia maneno yake au hotuba yake yakileta tafrani, mpasuko, sintofahamu, migogoro, mivutano, gumzo, au hatari ndani au nje ya nchi. Ni kiongozi ambaye huuchunga ulimi wake na kutambua athari ya maneno yake kama mkuu wa nchi. Anatambua ya kuwa ulimi wake ukiteleza kidogo au ukitamka maneno kwa hasira na jazba unaweza ligawa au lipasua Taifa. Anajua anaweza leta migogoro na sintofahamu ndani ya Taifa.

Ndio maana unaona wakati wote Rais Samia akisimama popote pale ndani ya Taifa na kuzungumza, unaona Taifa likitabasamu, likifurahi, likishangilia, likipumua, likitamalaki kwa amani na upendo. Ndio maana Rais Samia hata asipoonekana hadharani kwa siku moja watu wanaanza kumuulizia na kuwa na hamu ya kumuona hata akienda Kariakoo kutembea. Wanakuwa na shauku ya kusikia sauti yake, maana wanajua mama yao ni wa faraja na upendo kwao siku zote. Wanajua ni mwenye upendo na huruma tele kwao. Ni mwenye faraja na kutia moyo na matumaini wananchi wake.

Jiulizeni, Watanzania wenzangu, Mheshimiwa Rais Samia ametuvusha katika mangapi magumu kama Taifa? Tumeshinda vita na mapambano mangapi kama Taifa? Tumepigana vita vingapi? Sote tunakumbuka kwa ujasiri, ushupavu, na umadhubuti wake namna alivyotuvusha salama vipindi vigumu vya mtikisiko wa uchumi wa dunia uliosababishwa na ugonjwa wa COVID-19 pamoja na vita vya Ukraine. Tunakumbuka namna alivyotuvusha kipindi cha mfumuko wa bei ulimwenguni kote.

Tumevushwa na Rais Samia na serikali yake kwa kuwa wakati wote aliliweka Taifa mikononi mwa Mwenyezi Mungu na kumuomba Mungu amuongoze katika kulitumikia Taifa letu. Alijikabidhi mikononi mwa Mungu ili ampatie njia na maarifa ya kuliongoza Taifa letu, maana alijua hawezi pekee yake kwa akili za kibinadamu. Ndio maana Mungu amekuwa nasi kama Taifa, ametutetea na kutulinda kama Taifa, na kutupa neema na baraka kama Taifa katika kila nyanja. Popote alipogusa na kuweka mikono yake, Rais Samia palipata kufanikiwa na Watanzania walipata matumaini na furaha katika mioyo yao.

Tulivuka pia kama Taifa kutokana na ushupavu, umadhubuti, na ujasiri alio nao Rais Samia. Tulipenya kutokana na maono makubwa aliyo nayo katika kifua chake, tulipiga hatua na kutizama mbele kwa matumaini kutokana na utulivu wa uongozi alio nao Rais Samia na aliojaliwa na Mwenyezi Mungu. Pamoja na kuwa na misimamo ya uongozi yenye maslahi kwa Taifa isiyo yumba wala kuyumbishwa.

Ndio maana tunaona Taifa likiendelea kusonga mbele na kutamalaki kwa amani na utulivu nchini. Hakuna upenyo kwa shetani kuligawa Taifa letu wala kuvuruga amani na utulivu vilivyopo hapa nchini. Rais Samia ni mboni ya Taifa inayopaswa kulindwa kwa nguvu na wivu mkubwa sana, kwani ndiye taa yetu kama Taifa na nuru ya Watanzania. Tusikubali yeyote kwa maslahi yake binafsi aiguse mboni yetu ya Taifa.

Tuendelee kumuombea Rais wetu afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia Watanzania. Tusimuache mpweke na tusikubali ashambuliwe na wachache wenye maslahi yao binafsi na ajenda zao ovu na chafu kwa Taifa letu. Tumpiganie kwa maombi na kumtetea kwa maombi ili Mungu aendelee kumlinda, kumtetea, na kumpigania dhidi ya wale wanaotafuta madaraka kwa tamaa na uchu wa mamlaka. Tusimame naye popote asimamapo, kwa kuwa muda wote amesimama na Taifa letu analolipenda na kulipigania kwa dhati ya moyo wake.

Kazi iendelee! Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Akiona huu uzi wako atakutukana sana


Mithali 29:2
[2]Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi;
Bali mwovu atawalapo, watu huugua.
Rais Samia Ni mwenye Haki ndio maana Taifa limechanua kwa furaha na amani.Taifa zima limejaa Tabasamu.ndio maana amani na utulivu vimetamalaki hapa nchini maana hakuna mwenye kinyongo ndani ya moyo wake
 
Sawa ila Hii Haiondoi hatia ndani mwake,nenda kamuulize nini kinachomtesa sasa akikujibu kitafakari?
 
huyu mama ni mugwana na mchapa kazi wa hali ya juu..inafika mahali upinzani wana haha
Upinzani wamepoteana kwa sasa na hawaelewi ni vipi wanaweza kushindana naye katika sanduku la kura ,ndio maana unaona kwa sasa watu kama Lissu wamekata pumzi .maana pamoja na kuropoka sana lakini wamejikuta hakuna anayewaunga mkono wala kuwasikiliza au kuwaunga mkono
 
Watanzania hawajaridhika na mkataba wa Bandari yake Salama. Serikali isione aibu kuachana na Waarabu.

Tunaposema Bandari Imegawiwa, maana yake Imegawiwa, tena bure. Wadau wanaodai kuwa kuna rushwa zinanuka kwa kugawiwa Bandari zetu kwa wajomba, maana yake Rushwa inanuka.

Hivi vijisababu na hoja mbovu mbovu walizozitoa na wanazoendelea kuzitoa baada ya kushurutishwa kuhusu mkataba huu, havina maana yeyote ile. Ni uwongo kutaka kuhalilisha Udhalimu na Ufisadi unaotumika kumleta Mwarabu kuja kututawala.

Pinga udhalimu, maangamizo, Ukoloni mamboleo na ufisadi unaofanywa dhidi ya Watanzania,Watanganyika na Wamasai wa Taifa hili kwa nguvu zako zote. Wakemee Vibaraka wote wa Waarabu.
 
Misuli ya kiongozi inaendana na uwezo wa kujibu hoja za wananchi anaowaongoza. Siyo yeye kunyamwza na kuwanyazisha wananchi
 
1692647217705.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom