DOKEZO Rais Samia, Watumishi Wastaafu wa Jeshi tunaomba utusaidie kupata stahiki zetu, tunateseka

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
➤ Sisi ni Watumishi wa Umma Wastaafu tuliokuwa tunafanyia kazi vikosi mbalimbali vya Jeshi, tuliajiriwa kila mtu na CV namba yake na kila mtu alipewa barua ya kuajiriwa pia kila Mwajiriwa alikuwa na C/NO yake ya kupatia Mshahara kutoka Hazina (Pay Slip tunazo).

➤ Tukiwa katika ajira tulikuwa tunapandishwa Vyeo na pia tukapewa barua za kuthibitishwa kazini.

➤ Pamoja na hayo tulifanya kazi katika mazingira magumu, miaka ya mwanzo tulipoanza kazi tulikuwa tunapewa ‘unform’, Viatu na Pesa na Likizo.

➤ Kuanzia Miaka ya 1998 mambo yakabadilika tukawa hatupewi tena, ikawa inapita hadi miaka mitatu au minne ndio mnapewa tena ya mwaka mmoja.

➤ Kabla ya kustaafu tuliandika barua kuomba tupatiwe haki hizo lakini mpaka leo (Agosti 11, 2023) hatujajibiwa.

Baadhi yetu tulikuwa katika Mifuko ya NPF, tukahamishiwa NSSF baadaye tukahamishiwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

➤ Mfano kuna Mtumishi ambaye ametumikia miezi 495 lakini kwenye malipo akapewa miezi 272, kisha miezi 223 iliyosalia haijulikani malipo yake yamepotelea wapi, hata alipouliza hakupata majibu ya kueleweka zaidi ya kuambiwa amuulize Mwajiri wake.

➤ Muda wa Kustaafu ulipofika tukawekwa kwenye kikokotoo, pesa tulizojiwekea kwenye Mifuko ya Hifadhi tukakuta zimekatwa, tukapewa nusu ya kile kilichokuwa tumechangia.

➤ Tulipohoji mbona pesa zetu zimekatwa tukajibiwa kuwa ‘ndizo mtakazo kuwa mnalipwa kwa mwezi’. Yote tumevumilia lakini maisha yanazidi kuwa magumu.

➤ Wakati tumelipwa malipo pungufu kutoka katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pia malipo ya Kiinua Mgongo hatujapata kabisa, tulipouliza tukaambiwa hatutapewa, tulipohoji tukaambiwa ni maelekezo kutoka juu, kwamba hatutakiwi kulipwa na Hazina.

➤ Tumeenda kwa Afisa Utumishi ili atuandalie malipo ya Kiinua Mgongo tukaambiwa hatupaswi kulipwa kiinua mgongo kwa kuwa sisi ni vibarua.

➤ Tunapatwa na mshangao wa majibu hayo, tukamuuliza Afisa Utumishi wetu kuwa ‘mbona tulikuwa tunapanda vyeo na Pay Slip tunazo’, akatujibu ‘tusihangaike hii ndio amri imetolewa’.

➤ Cha kushangaza waliopewa barua za kutokulipwa ni wachache zinazoonyesha hawastahili kulipwa Kiinua Mgongo, tukahoji mbona wengine hawajapewa hizo barua, wala hatujajulishwa, tulijibiwa tufuate barua walizotumiwa wenzetu.

➤ Tumebaki na mshangao wala hatujui hatima yetu.

➤ Tumefanya jitihada nyingi za kukutana na Waziri wa Ulinzi kupitia wasaidizi wake lakini imeshindikana.

➤ Tulipotaka kulalamika kwenye Vyombo vya Habari, wakasema masuala yetu hayatolewi kwenye Vyombo vya Habari.

➤ Aprili 2023 tulikutana na Mbunge mmoja, akaahidi kutusaidia kutukutanisha na Waziri wa Ulinzi lakini tangu wakati huo mchakato haujafanikiwa, tukijulishwa kuwa ratiba za Waziri zinambana.

➤ Wastaafu tuko wengi kuanzia wa Mwaka 2019.

➤ Wastaafu wenzetu wa miaka ya nyuma walilipwa vizuri kwenye Mifuko ya Hifadhi na kiinua mgongo wakapewa, leo sisi tunaambiwa vibarua Je? Kibarua anapata mshahara wa Hazina na anapandishwa cheo na kuthibitishwa kazini?

➤ Tunapewa majibu ya mdomo, kinachoumiza zaidi ni kuwa wakati wa kuajiriwa tulipewa barua, leo tunajibiwa mdomoni tu kwamba sisi ni vibarua, ukiuliza zaidi wanasema kuna wenzetu wachache wametumiwa barua, hivyo wengine wote tufuate kile kilichoandikwa katika barua za wenzetu wachache, hii si sawa.

➤ Tunaomba huruma yako kuna Watumishi wa Umma waliumwa maradhi mbalimbali wakiwa kazini mfano, TB, HIV na Corona hawakulipwa chochote na muda wa kustaafu umefika walivumilia yote hayo walijua watafika mwisho wa ajira yao watalipwa, leo wanaambiwa hawapaswi kulipwa kiinua mgongo je, hii ni haki?

➤ Mheshimiwa Rais, kwa nafasi yako tunaomba utusaidie; maisha yetu sasa yamekuwa magumu kwa mtihani huu tulioupata.
 
Mtoa hoja ume rise hii kitu ambacho kinawaumiza mno wastaafu wetu ambao wameitumikia nchi hii kwa haki.

Sijawahi kusikia mafao ya wabunge (5yrs only) yamecheleweshwa au kuwekewa mizengwe, wanalipwa on time!

Wastaafu wa iliyokuwa EAC, kuanzia Bandarini hadi Posta na Simu wengi wao kama sio wote wamekufa bila ya kupata haki zao, na tuelewe baadhi ya fedha zao hazikuwa za serikali, serikali iliiba fedha hizi
 
Yaani watumishi wa majeshi ndio mnalalamika hivi 😂😂 hii ni aibu kubwa sana 😂😂😂. Yaani ccm mliowapambania usiku na mchana ndio wanawafanya hivi 😂😂, tena wengine mlisaidia kuiba kura 😂😂😂 mpaka ccm wanashinda.

Sisi raia tutafanyaje sasa 😂.

Ninyi mlitakiwa mjipange vizuri na wenzenu waliobakia jeshini mfanye ambush moja tu mpaka ikulu, kisha muruke live kwenye tbc1 mkiwa mmeshapindua. 😂😂 Tatizo lenu mtalitatua wenyewe mkiwa viongozi wa serikali ya mapinduzi ya Tanzania zaidi ya hapo mtaendelea kuzungushwa na mafaili na mabarua na manyaraka na ninyi wakati mna ujuzi kamili wa medani, silaha na intelijensia.

Jiongezeni, ohoooo mtateseka sana.
 
Mtoa hoja ume rise hii kitu ambacho kinawaumiza mno wastaafu wetu ambao wameitumikia nchi hii kwa haki.

Sijawahi kusikia mafao ya wabunge (5yrs only) yamecheleweshwa au kuwekewa mizengwe, wanalipwa on time!

Wastaafu wa iliyokuwa EAC, kuanzia Bandarini hadi Posta na Simu wengi wao kama sio wote wamekufa bila ya kupata haki zao, na tuelewe baadhi ya fedha zao hazikuwa za serikali, serikali iliiba fedha hizi
Hii ni aibu kubwa sana 😂😂😂😂 yaani wastaafu wa jeshi hawajalipwa mpaka leo 😂😂😂. Tena wanazungushwazungushwa.

Ingekuwa wastaafu wa majeshi ya west Africa wangeshapindua siku nyingi sana 😂😂😂
 
Mchonga ulaaniwe huko uliko milele wewe na lichama lako la mboga mboga.

Ni nini sasa kinacho waogopesha kutoka live na kudai stahiki zenu kwa ukamanda wenu. Au ukamanda wenu upo kutishia tu vijana wa JKT makambini na kuonea raia.

Hili jeshi la namna gani duniani sijawahi ona makamanda hawana uthubutu kabisa, hamjifunzi hata kwa wenzenu huko?

Sasa raia wa kawaida nao wafanye nini kama nyie makamanda mpo hivi? Hii ni ajabu kabisa kuwahi kuiona duniani?

CCM wafikirieni na mtatue matatizo yao hawa makanda maana sasa hii ni aibu kubwa kwa jeshi. CCM futeni fedheha hii.
 
Wanajeshi halafu wanalalamika 😂😂😂
Sisi raia wachovu tutafanyaje? 😂😂😂

Yaani hao wanajeshi wangejipanga wakapindua tu nchi, wakimaliza waruke live tbc1 wakitangaza kuanguka kwa ccm. Kisha wajilipe pesa wanazodai.

Ni aibu kubwa sana 😂
Hii ni aibu huu uzi una huzunisha kuliko kuchekesha. Ni aibu kubwa jeshi kuwa nyonge kwa mamlaka kiasi hiki.

Jeshi la namna gani hili limetengenezwa ? Na wao wanaona sawa tu kuwa jeshi la namna hii kwa watawala.

Wanavuna walicho panda, wanapaswa wafahamu kuwa wao ni Jeshi kwa ajili ya raia/wananchi sio watawala hovyo kabisa 🚮
 
😂🤣

Wanaganya matukioa shetani mwenyewe anashangaa🤣
😂😂
Nimecheka sana. Yaani wanajeshi kabisa. Yaani ccm inafika hatua mtu anayeshika bunduki na yeye wanamuibia 😂😂😂😂

NB:
Kuna uchaguzi nilikoswakoswa na risasi maana eneo hilo palikuwa na vurumai kubwa sana maana walikuwa wanachakachua kura. Yaani walipiga risasi nyingi sana usawa wa kijiwe chetu maana watu walijaa eneo na eno hilo ni Karibu na ofisi ya kuhesabia kura na ni karibu na kijiwe chetu cha drafti. Sitakuja kusahau aisee. Ile siku.

Mimi najua watumishi wa majeshi kama wanajeshi na mapolisi ni matajiri sana. Na wakistaafu wanapewa hela nyingi mno. Maana wanawapambania ccm mno.

Leo haohao ndio wanalalamika wameibiwa pesheni zao 😂😂
 
Siku zote niliamini hawa ndiyo kada isiyodhurumiwa na kuonewa kama walimu.

Kumbe walimu na wao ni fungu moja la kukosa!!!

Kweli tz ujanja ni kuwa mwana siasa.
Kwa jinsi mapolisi wanayopiga mabomu na risasi nyingi muda wa uchaguzi na wanavyolinda wizi wa kura wa ccm, nilijua hao watu ni matajiri sana na wanalipwa pesa nyingi mno. Kumbe mpaka pensheni zao zimeliwa 😂😂😂.

Aisee CCM kwa wizi shikamoo 😂😂😂
 
Back
Top Bottom