Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 30,369
- 88,533
Unaambiwa Mtumishi wa uuma wa ngazi ya chini aliyefanya kazi serikalini kwa zaidi ya miaka 30. Anapostaafu analipwa 33% tu ya mafao yake.
Yaani kama mtumishi hiyo wa umma alistahili kupata milioni 100 kama mafao (kumbuka hii ni pesa yake halali aliyokatwa kupitia mshahara wake kwa miaka yote hiyo 30+), basi atapatiwa kiasi cha shilingi milioni 33 tu. Na kiasi kinachobakia analipwa kila mwisho wa mwezi kwa muda wa miaka 12! Ikitokea mstaafu akafariki wakati wowote ule baada tu ya kustaafu, na hicho kiasi nacho kinakomea hapo hapo (Wizi wa mchana huu 🤭)
Halafu kichekesho zaidi ni kwamba hiki kikokotoo ni kwa baadhi tu ya Watumishi wa umma! Mfano walimu, Manesi, Maafisa ugani, nk.
Ukija kwa Vigogo wa ngazi za juu, mfano Wabunge; eti wenyewe hawahusiki na hiki kikokotoo! (Ona ubaguzi na upendeleo wa wazi huu 🤭) Ingawa na wenyewe eti ni watumishi wa umma!! Yaani wenyewe kila baada ya miaka 5 ya Ubunge wao, wanapatiwa mafao yao yote yanayokadiriwa kuwa kiasi cha shilingi milioni 250 za Kitanzania!
Ukija kwa vigogo wengine wa juu zaidi; mfano Rais, Makamu, Waziri Mkuu, Spika, na sasa wake wa hao vigogo; ikitokea wamestaafu! Wanapewa mafao yao yote! Na kila mwezi wanalipwa mshahara wa 80% kama ule wa Kigogo aliyeko madarakani kwa wakati huo kwa maisha yake yote! (Ubaguzi mwingine huu 🤭)
Swali la kujiuliza!! Kwa nini serikali mnawafanyia wafanyakazi wenu uonevu na wizi wa mchana kiasi hiki?
Mkiulizwa, mnatoa sababu za kipuuzi tu; eti wafanyakazi wakipewa hela zao zote kwa mkupuo wanaishia kuzitapanya na kutapeliwa, na mwisho wa siku wanakuwa masikini!! Sasa hao wafanyakazi wastaafu wakizitapanya hizo hela zao, nyinyi mnapata athari gani? Je, waliwaomba muwatunzie kupitia hicho kikokotoo chenu cha wizi?
Na kama mnaona ni muhimu kufanya hivyo, kwa nini msifanye mpaka kwa Wabunge? Je, ni kwa mini msitoe uhuru kwa Wastaafu kuchagua kama wanataka kupewa 33% pekee, au mafao yao yote?
Binafsi nimeandika haya malalamiko baada ya kushuhudia wastaafu fulani hivi niliopanda nao daladala sehemu fulani, wakilalamika kwa uchungu baada ya kulipwa mafao kiduchu kwa mfumo wenu huu kandamizi wa 33%.
Ushauri wangu kwa serikali; rejesheni mara moja kikokotoo cha zamani. Acheni kuwadhulumu wastaafu pesa zao.