PSSSF ziko wapi Billion 14 za Rais Samia alizolipa kwenu kwa ajili ya Wastaafu wa ATCL

kisingi

JF-Expert Member
Apr 9, 2014
516
377
Raisi Samia Suluhu Hassan alilipa billion 14 za mapunjo ya madai ya kustaafu waliokuwa wafanyakazi wa Air Tanzania Company Limited tarehe 27/12/2023 kwenye mfuko wa PSSSF.

Hadi muda huu ni asilimia thelathini tu ya Wastaafu ndio wamelipwa wengine wanapigwa dana dana hawalipi. Hawa ni pamoja na marubani na ma engineer Wastaafu.

Tunaomba serikali iingilie kati hawa wazee walipwe haki yao aliyowalipia Raisi Samia.
Mwezi wa tatu sasa hawalipi ni ahadi tu.

Waziri Ndalichako, CAG hebu angalieni pale uhasibu maana wasi wasi upo kuwa pesa hiyo imetumika kwingine kama alivyogundua CAG kule NHIF.

Raisi alimtumbua DG Februari 6 lakini watendaji wa chini bado ni wale wale watamkwamisha na huyu mteule.

PSSSF lipenzi pesa ya Wastaafu sio yenu kutengenezea interest kwa kuizuia miezi kadhaa.
 
PSSSF Pesa alizolipa Rais Samia kwenu kwa ajili ya wastaafu ATCL walipeni wazee hawa au mnataka wafe.
 
Hakuna watu wajinga kama watumishi wa umma wa Tanzania yaani huko ofisini kuna mabogasi kibao wanashindwa hata kupambania haki zao za msingi.
 
Back
Top Bottom