Ningekuwa Rais Samia, leo ningemtumbua Makonda akiwa uwanja wa KIA kabla hajakanyaga ardhi ya Arusha

Mganguzi

JF-Expert Member
Aug 3, 2022
1,094
2,820
Mbwembwe zinazofanywa na makonda na tabia yake ya kujifanya yeye ni special kuliko wakuu wa mikoani wote leo ingemtokea puani.

Ashukuriwe Mungu leo Kuna mvua Arusha, lakini mji umesimama! Watu wanalazimishwq kwenda kumpokea makonda kwa misafara mikubwa. Mbona wakuu wa mikoa wanapokabidhiwa ofisi huwa inakuwa kimya kimya kwani yeye ana nini? Yaani Makonda anaenda kupokelewa kia kwa misafara ya magari msururu.

Wakuu wa idara, wakuu wa wilaya leo hawapo ofisini wameendq kumpokea Makonda! Kwakweli Leo ningekuwa rais Samia ningemrudisha Dar akiwa kia, kazi zinasimamq kwa ajili eti anakabidhiwa ofisi Kuna maajabu gani kwenye kukabidhiwa ofisi? Makonda unanini lakini? Kwani ungeenda kama wanavyoenda wakuu wa mikoa wenzako ungekufa? Punguza cheche utachoma nyumba.
 
Back
Top Bottom