Rais Samia: Vijana waliopita JKT wanapaswa kubeba uzalendo wa Nchi moyoni na sio mdomoni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Maadhimisho va Miaka 60 ya JKT katika Uwanja wa Jamhuri - Dodoma leo terehe 10 Julai, 2023.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema vijana wanaopita JKT wanapaswa kubeba uzalendo wa Nchi moyoni na sio mdomoni mwao na kuwa tayari kulinda, kupigania na kutetea nchi.

Ameipongeza JKT kwa kuendesha mafunzo mazuri ya utimamu kwa vijana, kuendeleza ujuzi wao pamoja na kutengeneza ajira, kupunguza kiwango cha umaskini pamoja na utegemezi.

Lengo la Serikali ni kuongeza uwezo wa JKT iweze kutekeleza majukumu yake vizuri hasa kwenye nyakati hizi ambazo mwamko wa vijana kujiunga na jeshi hilo umekuwa mkubwa.

Gwaride.jpg

Gwaride la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) likipita kwa mwendo wa pole na haraka mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mabele.jpg

Mabele2.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajab Mabele wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Samia Jeshi.jpg
 
60 yrs za JKT ,yeah nimepitia jeshi hili wakati ni jeshi nchi ilikua na heshima na adabu, salute kwako CO LT.COL MTONO pale 835kj,maana ulinifanya niwe ngangari, bila ya kusahau CO LT.COL SANGA pale 837kj, kambi hii ndio it pushed me to the limits, ilinijengea ujasiri, uthubutu mkubwa sana,hongera mno JKT kwa maadhimisho yenu
 
Back
Top Bottom