Rais Samia Kuongoza Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu Dk. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), yatakayofanyika kesho.

Kwa mujibu wa taarifa kwenye maadhimisho kumeandaliwa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na gwaride la vijana wa JKT, maonesho ya vifaa mbalimbali vya SUMAJKT na burudani za ngoma kutoka vikundi vya JKT.
Hayo yameelezwa na waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Innocent Bashungwa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari akielezea juu ya kilele cha maadhimisho ya miaka 60 tangu lilipoasisiwa jeshi hilo.

Waziri huyo alisema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan imeonesha jitihada zake za kuhakikisha JKT linaendelea kuwa kitovu cha malezi bora kwa vijana wa kitanzania.

"Namshukuru Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa jitihada anazozifanya za kuhakikisha JKT inaendelea kuwa kitovu cha malezi bora kwa viana wa kitanzania", alisema Bashungwa.

Aidha aliwashukuru JKT kwa maandalizi ya maadhimisho hayo, wadhamini na wote wanaoshirikiana katika maandalizi ya Mika 60 ya JKT pamoja na ongozi wa mkoa wa Dodoma chini ya Rosemary Senyamule kwa uratibu unaoendelea katika kufanikisha Maadhimisho haya ya kihistoria.

"Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT, kimetanguliwa na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na mbio za JKT marathon 2023 iliyofanyika Juni 25 hapa Dodoma, kuzinduliwa kwa Mnara wa kumbukumbu katika Makao Makuu ya JKT (Chamwino Dodoma).

Aidha kutakuwa na maonesho ya bidhaa ambayo yanaendelea hadi sasa katika viwanja vya Medeli East mkabala na SUMAJKT House na kushiriki katika huduma za kijamii kama kutembelea hospitali уа Uhuru iliyopo wilayani Chamwino pamoja na vituo vya kulelea watoto wenye uhitaji, "alisema Waziri Bashungwa.​
 
Pongezi kwa amiri Jeshi Mkuu na Jeshi letu kwa kutimiza miaka 60, Jeshi imara zaidi lenye weledi na ari kubwa.
 
Weledi wa kucheza ngoma na kupasua tofali kwa vichwa huku nchi ikiingia mikataba mibovu inayopelekea iuuzwe?
 
Back
Top Bottom