Rais Samia: Serikali haijafunga mipaka kuuza mazao nje ya Nchi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki kilele cha sikuku ya Nane Nane jijini Mbeya, leo Agosti 8, 2023.



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson amesema wakazi wa Mbeya wanaunga mkono uwekezaji unaofanywa na Serikali kwenye Bandari ya Dar es Salaam kupitia kampuni ya DP World.

Amesema Jiji la Mbeya ni jiji pekee linalopatikana nyanda za juu kusini, hata hivyo barabara zake sio nzuri hivyo zinapaswa kutazamwa ili kuliongezea hadhi jiji hilo.

Akizungumza kwenye Maadhimisho hayo, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema uzalishaji wa chakula umeongezeka sana msimu huu kwa zaidi ya tani milioni 3. Aidha, kutokana na ruzuku ya dawa za kuua fangasi kwenye Parachichi iliyotolewa na Rais, zao hilo limepanda ubora wake pamoja na kiasi cha uuzaji nje ya nchi.

Mwaka huu wa kilimo, Serikali itatumia zaidi Bilioni 200 kwa ajili ya ruzuku ya mbolea nchini ili kuongeza uzalishaji wa mazao kwa wakulima.

Waziri Bashe amebainisha pia uwepo wa uvamizi kwenye maeneno ya utafiti wa kilimo, amewaomba wananchi kuacha tabia hiyo na wale waliovamia wanapaswa kuachia maeneo hayo ili yafanye kazi iliyokusudiwa.

Rais Samia anazungumza
Lengo la maadhimisho haya ni kutambua na kuenzi mchango wa sekta za kilimo, uvuvi na ufugaji pamoja na kutangaza shughuli mbalimbali za uzalishaji pamoja na kutoa fursa ya kutafakari na kutathimini sekta hizi muhimu.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni Vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula, kwa kutambua umuhimu wa makundi haya, Serikali inaongeza jitihada za makundi haya katika kushiriki shughuli za kilimo.

Serikali haijafunga mipaka kuuza mazao nje ya nchi bali tunataka kuwa na mfumo rasmi ili uwezeshe serikali kujua kiasi cha mazao yanayouzwa nje ya nchi.

Uzoefu wa sasa unasema Magari yanatoka nje ya nchi na kuingia moja kwa moja kwa wakulima, wanalipa kwa fedha za ndani. Haya ni mazao yanayoweza kuuzwa kwa fedha za nje

Taasisi za utafiti zilinde vizuri maeneo yao, na waliomiwa wanapaswa kufahamika ili tatizo liondolewe. Kilimo bila itafiti hatuwezi kwenda vizuri. Tukiachia maeneo haya yachukuliwe tunaenda kudumaza utafiti na uzalishaji wa mbegu.

Niwaombe washirika wetu wa maendeleo bado tunahitaji msaada kwenye sekta ya miundombinu ya umwagiliaji.
 
Mnataka rais anayesimama njiani na kugawa pesa kwa wenye mahitaji mbalimbali na kula mahindi ya kuchoma?.

Kila kinachotokea duniani kina msimu wake na ndio maana kinaweza kuwasisimua na kuwasikitisha watu wengi kila kinapokuwa machoni mwao.

Haiwezekani watu wawili waliotoka tumboni mwa mwanamke wakawa na tabia sawa kwa asilimia mia moja, hakuna kitu kama hicho.
 
hii nchi imejaaa wapumbafu sana. mtu aangalii raisi anafanya mambo gani ya maendeleo , anakalia kusema raisi hana mvuto. afu wanajiita wasomi. watu weusi akili zetu sijui zipoje. walimchagua kikkwete eti kisa mzuri. watu wenye akili wanapima utendeji wa mtu sio mvuto wala uzuri wa mtu.
 
UNGEPENDA KUTOA MAONI GANI KUELEKEA SIKUKUU YA WAKULIMA, ILI KUENDELEA KIJIKWAMUA KIUCHUMI KUPITIA KILIMO???
IMG_20230808_103649.jpg
 
hii nchi imejaaa wapumbafu sana. mtu aangalii raisi anafanya mambo gani ya maendeleo , anakalia kusema raisi hana mvuto. afu wanajiita wasomi. watu weusi akili zetu sijui zipoje. walimchagua kikkwete eti kisa mzuri. watu wenye akili wanapima utendeji wa mtu sio mvuto wala uzuri wa mtu.
Nchi ya mazuzu
 
Mi najiuliza tu hii ni coincidence au ni nini.?

Kesi ya kupinga mkataba wa kishenzi wa kugawa rasilimali za Tanganyika imefunguliwa mkoa wa Mbeya, hukumu ilitakiwa itolewe tarehe 7/8/2022 lakini ikaahirishwa mpaka tarehe 10/08/2022. Pia nane nane ikapangwa kilele chake kiishie Mbeya na mgeni rasmi awe rais wa nchi.

Je hili halitaifanya mahakama isitende haki kwa upande wa walalamikaji ambao kiuhalisia ndiyo wako sahihi?
 
Naomba Serikali iangalie bidhaa zinazoagizwa toka nje ya nchi. Kwa mfano mafuta ya kula toka nje ya nchi, serikali iache kuagiza ama mafuta hayo yatozwe kodi kubwa ili kumpa unafuu wa soko mkulima wa alizeti wa Tanzania. Alizeti imeshuka sana bei mwaka huu sababu kubwa ni kuingiza mafuta ya kula toka nje.
 
Back
Top Bottom