Rais Samia: Tuache alama ili nchi yetu ipate maendeleo ya haraka

Baraka Mina

JF-Expert Member
Sep 3, 2020
581
574
Je tutaacha alama hapa duniani pale muda wetu wa kuishi kulingana na wito na kusudi la kuwepo kwetu hapa duniani utakapokuwa umefikia ukomo? "Haijalishi umeishi miaka mingapi bali umeweka alama gani katika miaka uliyoishi" ni moja ya mstari ambao huwa tunausikia katika misiba na mafundisho mbalimbali ya kututataka tufanye mema na kuacha kumbukumbu hapa duniani. Tukiwa katika kipindi hiki cha simanzi kufuatia kifo cha mhandisi Mfugale Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Samia Suluhu Hassan anatukumbusha wajibu ambao ni vema kila mmoja wetu akatimiza.

Leo tarehe 02 Julai 2021 Ndg. Samia Suluhu Hassan amewaongoza viongozi wa Serikali na, taasisi na waombolezaji katika shughuli ya kuaga na kutoa heshima za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick A.L. Mfugale katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar Es Salaam. Mhandisi Mfugale alifariki dunia Juni 29, 2021 katika hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Akitoa salamu za rambirambi Ndg. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imempoteza (Mhandisi Mfugale) mtumishi na kiongozi muadilifu, makini, shupavu na mchapakazi hodari. Taifa letu limempoteza mhandisi mahiri na mzalendo wa kweli ambaye daima alikuwa tayari kuitumikia nchi yake kwa moyo wake wote." Sambamba na hilo amesisitiza kuwa Mhandisi Mfugale ameacha alama kubwa kwa nchi yetu. Ametoa mchango mkubwa sana hususan katika sekta ya miundombinu; alikuwa ni baba wa madaraja, barabara, viwanja vya ndege na miradi ambayo haikuwa chini ya sekta yake. Pia amesema Mfugale alikuwa mjumbe wa timu za wataalamu wa Serikali kwenye miradi ya kimkakati kwenye bwawa na reli; hadi umauti unamkuta alikuwa tayari ameshakamilisha michoro ya barabara ya mzunguko na njia nne kule Dodoma pamoja na uwanja wa ndege wa Msalato; taifa limepoteza mtu muhimu sana.

Rais ameeleza kuwa Marehemu Mfugale alimueleza na kumpa matumaini yake jinsi ya kulijenga na kulikamilisha daraja la Busisi/JPM lakini kwa bahati mbaya tunachopanga wanadamu Mungu hapangi hichohicho, amemchukua kabla ya matumaini yake kutimia. Ndg. Samia amesema anaungana na familia, watanzania na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na masikitiko makubwa na anamuomba Mwenyezi Mungu awajalie moyo wa faraja na uvumilivu.

Ndg. Samia Suluhu Hassan amesema funzo tunalolipata kutokana na maisha ya Mhandisi Mfugale hapa duniani ni kuacha alama. Amesema "ukibahatika kupata umri hapa duniani ni lazima uache alama. Kila mmoja wetu anapaswa kutumia fursa au kipawa alichopewa na Mwenyezi Mungu kuacha alama." Mwisho akasisitiza kuwa anaamini endapo kila mtu ataishi maisha ya kuacha alama; nchi yetu itapata maendeleo kwa haraka.

Mhandisi Mfugale amekuwa mtumishi wa umma kwa takribani miaka 45, tangu mwaka 1977 ambapo ameongoza TANROADS kwa takribani miaka 12 tangu mwaka 2009. Atakumbukwa kwa kubuni na kusimamia ujenzi wa Daraja la Umoja (Mtambaswala) linalounganisha Tanzania na Msumbiji, Daraja la Nyerere (Kigamboni), Daraja la Mkapa katika Mto Rufiji, Daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi, Daraja la Magufuli katika Mto Kilombero, Daraja la Mfugale (TAZARA), Daraja la Kijazi (Ubungo), Daraja la Tanzanite (Selander), Daraja la Kigongo – Busisi (JPM) pamoja na Miradi mingine ya kimkakati.
Hatukuumbwa kufanya kila kitu, unaweza kuwa na kitu kimoja tu ambacho utaambatana nacho katika maisha yako yote na mwisho wa siku dunia itakutambua kwa hicho ulichoamua kufanya kwa muda mrefu. Tafuta na jielekeze katika kuishi kwenye kusudi lako la kuwepo duniani ili uache alama kumbuka tuishi kwa kupendana kwa sababu duniani tunapita.

#RIPMfugale
#DaimaTutakukumbuka

SAMIA.jpeg

b1fd001d146fb395c7e7ac6c8914d6a9.jpeg
eaa2af68fc8c9eeed5bc6624f45a1339.jpeg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 02 Julai 2021 amewaongoza viongozi wa Serikali na, taasisi na waombolezaji katika shughuli ya kuaga na kutoa heshima za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick A.L. Mfugale katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar Es Salaam. Mhandisi Mfugale alifariki dunia Juni 29, 2021 katika hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Akitoa salamu za rambirambi Ndg. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imempoteza (Mhandisi Mfugale) mtumishi na kiongozi muadilifu, makini, shupavu na mchapakazi hodari. Taifa letu limempoteza mhandisi mahiri na mzalendo wa kweli ambaye daima alikuwa tayari kuitumikia nchi yake kwa moyo wake wote. Sambamba na hilo amesisitiza kuwa Mhandisi Mfugale ameacha alama kubwa kwa nchi yetu. Ametoa mchango mkubwa sana hususan katika sekta ya miundombinu; alikuwa ni baba wa madaraja, barabara, viwanja vya ndege na miradi ambayo haikuwa chini ya sekta yake. Pia amesema Mfugale alikuwa mjumbe wa timu za wataalamu wa Serikali kwenye miradi ya kimkakati kwenye bwawa na reli; hadi umauti unamkuta alikuwa tayari ameshakamilisha michoro ya barabara ya mzunguko na njia nne kule Dodoma pamoja na uwanja wa ndege wa Msalato; taifa limepoteza mtu muhimu sana.

Rais ameeleza kuwa Marehemu Mfugale alimueleza na kumpa matumaini yake jinsi ya kulijenga na kulikamilisha daraja la Busisi/JPM lakini kwa bahati mbaya tunachopanga wanadamu Mungu hapangi hichohicho, amemchukua kabla ya matumaini yake kutimia. Ndg. Samia amesema anaungana na familia, watanzania na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na masikitiko makubwa na anamuomba Mwenyezi Mungu awajalie moyo wa faraja na uvumilivu.

Ndg. Samia Suluhu Hassan amesema funzo tunalolipata kutokana na maisha ya Mhandisi Mfugale hapa duniani ni kuacha alama. Amesema "ukibahatika kupata umri hapa duniani ni lazima uache alama. Kila mmoja wetu anapaswa kutumia fursa au kipawa alichopewa na Mwenyezi Mungu kuacha alama." Mwisho akasisitiza kuwa anaamini endapo kila mtu ataishi maisha ya kuacha alama; nchi yetu itapata maendeleo kwa haraka.

Mhandisi Mfugale amekuwa mtumishi wa umma kwa takribani miaka 45, tangu mwaka 1977 ambapo ameongoza TANROADS kwa takribani miaka 12 tangu mwaka 2009. Atakumbukwa kwa kubuni na kusimamia ujenzi wa Daraja la Umoja (Mtambaswala) linalounganisha Tanzania na Msumbiji, Daraja la Nyerere (Kigamboni), Daraja la Mkapa katika Mto Rufiji, Daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi, Daraja la Magufuli katika Mto Kilombero, Daraja la Mfugale (TAZARA), Daraja la Kijazi (Ubungo), Daraja la Tanzanite (Selander), Daraja la Kigongo – Busisi (JPM) pamoja na Miradi mingine ya kimkakati.

Tuishi kwa kupendana kwa sababu duniani tunapita.
#RIPMfugale
#DaimaTutakukumbuka
SAMIA.jpeg
 
Mtoa hoja umetoa mada nzuri,ni kipindi cha huzuni kwa watanzania wote sio wanaccm pekee,was no need to mention uenyekiti wa ccm ,hapo hakuna ccm kuna watanzania wanamsindikiza mtanzania mwenzao
 
Asante nashukuru.
Niliandika hivyo kwa sababu Rais ni Mwenyekiti wa CCM pia.
 
Nchi ni yetu sote kwanini kuhasimiana.
Kuna wachache wetu wanakosa kuwa na uvumilivu.
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameomba tumpe muda aweke sawa uchumi wa nchi. Huenda kuna mambo ambayo hajakaa sawa anatamani kuona yakisimama vema na nchi kuwa na ustawi.
Wapinzani wanasema hawataki wakati ni suala linalowezekana na linajadilika.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 02 Julai 2021 amewaongoza viongozi wa Serikali na, taasisi na waombolezaji katika shughuli ya kuaga na kutoa heshima za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick A.L. Mfugale katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar Es Salaam. Mhandisi Mfugale alifariki dunia Juni 29, 2021 katika hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Akitoa salamu za rambirambi Ndg. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imempoteza (Mhandisi Mfugale) mtumishi na kiongozi muadilifu, makini, shupavu na mchapakazi hodari. Taifa letu limempoteza mhandisi mahiri na mzalendo wa kweli ambaye daima alikuwa tayari kuitumikia nchi yake kwa moyo wake wote. Sambamba na hilo amesisitiza kuwa Mhandisi Mfugale ameacha alama kubwa kwa nchi yetu. Ametoa mchango mkubwa sana hususan katika sekta ya miundombinu; alikuwa ni baba wa madaraja, barabara, viwanja vya ndege na miradi ambayo haikuwa chini ya sekta yake. Pia amesema Mfugale alikuwa mjumbe wa timu za wataalamu wa Serikali kwenye miradi ya kimkakati kwenye bwawa na reli; hadi umauti unamkuta alikuwa tayari ameshakamilisha michoro ya barabara ya mzunguko na njia nne kule Dodoma pamoja na uwanja wa ndege wa Msalato; taifa limepoteza mtu muhimu sana.

Rais ameeleza kuwa Marehemu Mfugale alimueleza na kumpa matumaini yake jinsi ya kulijenga na kulikamilisha daraja la Busisi/JPM lakini kwa bahati mbaya tunachopanga wanadamu Mungu hapangi hichohicho, amemchukua kabla ya matumaini yake kutimia. Ndg. Samia amesema anaungana na familia, watanzania na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na masikitiko makubwa na anamuomba Mwenyezi Mungu awajalie moyo wa faraja na uvumilivu.

Ng. Samia Suluhu Hassan amesema funzo tunalolipata kutokana na maisha ya Mhandisi Mfugale hapa duniani ni kuacha alama. Amesema "ukibahatika kupata umri hapa duniani ni lazima uache alama. Kila mmoja wetu anapaswa kutumia fursa au kipawa alichopewa na Mwenyezi Mungu kuacha alama." Mwisho akasisitiza kuwa anaamini endapo kila mtu ataishi maisha ya kuacha alama; nchi yetu itapata maendeleo kwa haraka.

Mhandisi Mfugale amekuwa mtumishi wa umma kwa takribani miaka 45, tangu mwaka 1977 ambapo ameongoza TANROADS kwa takribani miaka 12 tangu mwaka 2009. Atakumbukwa kwa kubuni na kusimamia ujenzi wa Daraja la Umoja (Mtambaswala) linalounganisha Tanzania na Msumbiji, Daraja la Nyerere (Kigamboni), Daraja la Mkapa katika Mto Rufiji, Daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi, Daraja la Magufuli katika Mto Kilombero, Daraja la Mfugale (TAZARA), Daraja la Kijazi (Ubungo), Daraja la Tanzanite (Selander), Daraja la Kigongo – Busisi (JPM) pamoja na Miradi mingine ya kimkakati.

Tuishi kwa kupendana kwa sababu duniani tunapita.
#RIPMfugale
#DaimaTutakukumbuka
View attachment 1838016
Mama anahudhuria misiba yule mwingine naona mganga wale alimkataza
 
Kuna wachache wetu wanakosa kuwa na uvumilivu.
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameomba tumpe muda aweke sawa uchumi wa nchi. Huenda kuna mambo ambayo hajakaa sawa anatamani kuona yakisimama vema na nchi kuwa na ustawi.
Wapinzani wanasema hawataki wakati ni suala linalowezekana na linajadilika.
ndio maana tunsema kama ana mambo mengine sawa. Lakini kisingizio cha uchumi haina mashiko
 
Back
Top Bottom