Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akihutubia Wananchi wa Kizimkazi, Zanzibar leo Agosti 13, 2026, wakati akizindua rasmi Mradi wa Maji wa Kizimkazi, amesisitiza wananchi kulinda amani ili kuwepo maendeleo.
"Na vile vile nisisitize kwamba uwepo wa miradi hii tumeweza kuijenga na kuileta kwa sababu nchi yetu ina amani. Na ninawashukuru waliocheza ngoma pale, wamesema Kizimkazi ni amani, Kusini ni amani. Niombe sana ndugu zangu tuendelee kutunza amani yetu ili tupate maendeleo zaidi.
Na hii ndiyo maana ya Mapinduzi. Tunaposema Mapinduzi Daima, Mapinduzi yalishafanyika, sasa Mapinduzi ni ya maendeleo. Tunapindua yaliyokuwepo ambayo tulikuwa nyuma, tunaleta maendeleo bora zaidi. Hiyo ndiyo maana ya Mapinduzi, naomba tutunze Mapinduzi yetu."- Amesema Rais Samia