Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941
Rais Samia Suluhu Hassan anaipaisha Tanzania kimataifa kisiasa na kiuchumi.

Rais Samia Suluhu Hassan alianza na ‘Royal Tour’ kama sehemu ya kui - brand Tanzania katika uso wa dunia, na sasa safari hii ya New York pamoja na kuhudhuria Baraza la Umoja wa Mataifa na mikutano mingine, itatumika kama sehemu muhimu ya kuitangaza Tanzania kimataifa.

Katika dunia ya leo, kuvutia wawekezaji, kuongeza watalii ni masuala ya kibiashara zaidi kuliko siasa, ndiyo maana nchi lazima ijitangaze kama bidhaa yenye ubora na inayovutia kuliko zote.

Wataalamu wa masoko wanajua umuhimu wa jina la bidhaa kutajwa tajwa mara kwa mara kwa wateja waliodhamiriwa huifanya bidhaa hiyo kuzoeleka kwa wateja kiasi kwamba kila inapotokea mtu anahitaji bidhaa hiyo harakaharaka humuijia jina au ‘brand’ anayoisikia mara kwa mara.

Vivyo hivyo kwa utalii na uwekezaji, mtalii anapotaka kufanya safari yake kama nchi zina vivutio vinavyofanana, mara nyingi huamua kwenda kule ambapo amekusikia zaidi kuliko kule ambako hajawahi kupasikia. Kwa sababu mtalii siyo mfumbuzi mfano wa kina Christopher Columbus, hupenda anapotumia pesa zake awe na uhakika wa kile atakachokipata, ni vigumu sana kwenda kubahatisha sehemu asiyoijua au kusikia chochote kuihusu.

Vivyo hivyo mikutano ya wawekezaji wakubwa pamoja na mambo mengine wanapoamua kwenda kuwekeza mahali wanataka wawe na uhakika na aina ya nchi wanayokwenda kufanya nayo kazi, wanaijua na wanawafahamu viongozi wake na labda wamewahi kukutana kwenye pembezoni mwa mikutano mikubwa ya kimataifa.

Ndiyo maana pamoja na Toyal Tour, safari hii ya New York itaongeza ushawishi wa kutajwa Tanzania kwenye maskio ya dunia, na kuingozea Tanzania ‘visibility’ katika masuala ya kimataifa.

Rais akiwa katika mikutano mikubwa namna hiyo ya kiwango cha dunia, anakutana ana kwa ana na viongozi wenzake na wakubwa wa mashirika na taasisi muhimu duniani ambapo ni rahisi kufanya ushawishi kwa manufaa ya Tanzania kuliko pengine popote.

Septemba 23, Rais Samia atakapokuwa analihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kama Rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania, mtazamo wa dunia kuhusu Tanzania hautabaki kuwa ule ule, uko ushawishi atakaouongeza hasa kutegemea na aina ya hotuba atakayotoa.

Kwa kufanya hivyo ziara hiyo hasa kwa kuwa inakwenda sanjari na uandaaji wa makala za runinga za Royal Tour kutaiongeza Tanzania ‘visibility’ kimataifa na kuiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuvutia watalii na wawekezaji wengi zaidi.

Kwa hatua hizi anazochokua Rais Samia kuelekea ujenzi wa Taifa imara na uchumi wenye nguvu, tunahitaji kumuunga mkono na kumtia moyo ili kwa pamoja tuisogeze Tanzania Mbele

Tanzania Unforgettable
Kazi Iendelee
 
Nadhani tuje na hoja jakaya alizurura DUNIA YOTE akapewa na fursa ya kuwa rais kutokea africa aliye enda kumuona obama

Lakini hakuna alichofanya mimi nakueleza kuwa hakuna mtu anayezurura akawa anaipenda nchi yake

Mtu anayependa kwake hazururi ila anakuwa na maono ya kwake

Nchi yetu itashuka kiuchumi MAGUFULI HII NCHI ALIJARIBUBKUIOMBOA

alikuwa shupavu sasa tunaona mambo magumu sana

Mfano serikali ya awamu ya sita sijaona mbiu kazi yake au hii serikali inalega kipi nadhani
Tusianze kusifia jakaya

Alizurura kote aliacha masikini haina hata ndege hakuna meli

Kila kitu kilikuwa hovyo kuvaa tu tshirt ya ccm kariakoo ilikuwa laana

Lakini sasa tunawaona na hizo nguo kila mahali

Hivyo tunaomba rais aache ziara nyingi
 
Rais Samia Suluhu Hassan anaipaisha Tanzania kimataifa kisiasa na kiuchumi.

Rais Samia Suluhu Hassan alianza na ‘Royal Tour’ kama sehemu ya kui - brand Tanzania katika uso wa dunia, na sasa safari hii ya New York pamoja na kuhudhuria Baraza la Umoja wa Mataifa na mikutano mingine, itatumika
Unaweza ukavutia wawekezaji sana kwa kuzurura na ukajitangaza sana....lakini ikiwa una katiba mbovu isiyo wahakikishia wawekezaji usalama wa mitaji yao. Ikiwa ni pamoja na sera, sheria mbovu ambazo haziwapi assurance ya sustainability ya biashara zao. Unapoteza muda....Samia anapoteza muda. Arekebishe hilo kwanza

Wawekezaji hawaangalii amani/au utulivu wa nchi. Mfano ni Kenya ijapokuwa wanajua nyakati za uchaguzi kenya huwa katika hatihati ya kulipuka, huwa wnaona ni heri waende mapumziko kwao au waje Tanzania au Serengeti lakini si kuhamishia mitaji yao Tanzania.

Kikwete aliwavutia wawekezaji wengi , kosa alilofanya hakubadilisha katiba ili isimamie utawala bora, sheria za uwekezaji zikawa zilezile mbovu, na ikaonekana nchi inasonga kwa sababu he did not care about the Law, wawekezaji walikuja wakiwa wanamfuata yeye.

Magufuli alipoingia, akataka sheria zifuatwe, kilichotokea kila mtu anajua.
 
Rais Samia Suluhu Hassan alianza na ‘Royal Tour’ kama sehemu ya kui - brand Tanzania katika uso wa dunia, na sasa safari hii ya New York pamoja na kuhudhuria Baraza la Umoja wa Mataifa na mikutano mingine, itatumika kama sehemu muhimu ya kuitangaza Tanzania kimataifa.

Nairobi, Kenya
Makala ktk Gazeti pendwa la Taifa Leo

Screenshot-2021-09-18-at-11.29.31-875x500.png

  • Sep 18, 2021

DOUGLAS MUTUA: Rais Suluhu Hasuluhishi, Anavuruga.

Na DOUGLAS MUTUA
HIVI Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania anasuluhisha mambo au anayavuruga kwa raha zake?

Watanzania wanapumua kwa njia huru au bado wamebanwa kama ilivyokuwa enzi ya mtangulizi wa Bi Suluhu, marehemu dikteta John Pombe Magufuli?

Nimesalitika kujiuliza maswali haya hadharani kwa kuwa Rais huyo amedai kuitetea demokrasia ilhali amewafunga jela wapinzani na kuzuia magazeti kuchapishwa.
Hizo si ishara tu za kutokuwapo kwa demokrasia bali ithibati tosha kwamba demokrasia kamwe haipo!

Ni sharti tuambizane ukweli hata tukisalitika kwa mama kiasi gani.
Nchi ya Tanzania ni kubwa kumziki mtu yeyote yule, hivyo yote tuliyomtamkia kweupe marehemu Magufuli alipojiona Mungu tutayakariri kwa marudio ili naye Suluhu ayasikie.

Demokrasia, ambayo hakika ni uhuru wa kimsingi wa binadamu, si hisani ambayo wananchi hupewa na viongozi wao wakionyesha tabia njema, la hasha!

Ni stahiki ya mtundu na mtiivu; mnyonge na mwenye maguvu hata ikiwa hawapendi viongozi wake.
Hahitaji kupendwa nao pia ila wana jukumu la kumhakikishia demokrasia. Wao si uhusiano wa kimapenzi bali uhalisia wa maisha yenye mustakabali angavu.

Watanzania wote – wawe wa Chama cha Mapinduzi (CCM); Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema); Alliance for Change and Transparency (ACT) Wazalendo na vinginevyo – wana haki ya kutendewa usawa.

Rais Suluhu alinishtua sana pale serikali yake ilipomkamata na kumzuia kinara wa Chadema, Bw Freeman Mbowe, na viongozi wengine wa Upinzani mnamo Julai 2021.

Kosa lao? Ati kujiandaa kufanya kikao cha kujadili na kuishinikiza serikali ikubali Tanzania ipate katiba mpya. Walichotwa wote hata kabla ya kikao kuanza!
Bw Mbowe alifululizwa mpaka mahakamani akafunguliwa mashtaka mabaya sana ya kufadhili ugaidi na kula njama.

Ni mtindo wa kileo kwa serikali dhalimu kumsingizia mtu makosa ya ufisadi ili kumpaka tope kimataifa, nchi za nje zimkimbie kama anayenuka, asitue popote pale.

Lakini Tanzania inapaswa kujua Bw Mbowe anasifika kimataifa, hawi wa kiwango hicho hata! Kujaribu kubana usemi wake ni kuupa kipaza-sauti hasa, kumvumisha bila kujua.

Hebu tafakari Raila Odinga akifunguliwa mashtaka ya kubambikiziwa kama hayo uniambie Kenya itakuwaje. Hofu kote-kote, sikwambii wawekezaji wataiambaa kama jini.

Hata baadhi yetu tusioziamini siasa zake za ubinafsi, ujanja na vitendawili bandia tutamwagika barabarani kuishinikiza serikali imwachilie huru mara moja!

Unatambua demokrasia imekomaa si haba pale watu wasiokupenda wanapojitoa mhanga kutetea haki yako ya kusema mambo ambayo masikioni mwao yanaudhi ajabu.
Rais Suluhu anapaswa kukomaa kiasi hicho, apinge vikali jaribio la wahafidhina wa chama chake, CCM, kumshawishi amwogope Bw Mbowe na Upinzani kwa jumla.

Vigogo wa siasa kama vile Bw. Freeman Mbowe, wakili machachari na jasiri Tundu Antipas Lissu na wengineo ni watu wa kuitwa faraghani wampe maoni yao kuhusu utawala kwa jumla.

Hata hivyo, inaonekana wanyonge wa CCM wamefaulu kumkumbusha Rais Suluhu kuwa ni mwanamke, wakamsadikisha kuwasikiza wapinzani ni kuhatarisha urais wake.

Na ameingia woga kiasi kwamba hata magazeti ya CCM yenyewe ameanza kuyafungia kuchapishwa!
Uliza gazeti la Uhuru, linalomilikiwa na CCM, lilipigwa kumbo kiasi gani liliporipoti kuwa huenda Bi Suluhu asiwanie urais ifikapo 2025. Ana hofu kupindukia; anang’ata hapulizi!

Liulize lile gazeti la Raia Mwema yaliyolipata lilipomhusisha na CCM gaidi aliyewaua watu wanne jijini Dar es Salaam mwezi jana.

Bi Suluhu anapaswa kuelewa kuwa woga wa aina hii husababisha udikteta, haumpi mtu umaarufu wa kuchaguliwa bali humpa sifa za nduli mnyanyasaji wa kutemwa.

Watanzania nao, ikiwa Bi Suluhu atawanyima haki za msingi ili achaguliwe tena, wanapaswa kumnyima kura kwa fujo na kumsomba mbali pamoja na CCM yake.

mutua_muema@yahoo.com

Source : DOUGLAS MUTUA: Rais Suluhu hasuluhishi, anavuruga – Taifa Leo
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
21 September 2021

# LIVE : MBATIA ANAONGEA KUHUSU:

  • HISTORIA YA VYAMA VINGI
  • HALI YA KISIASA NA KIJAMII TANZANIA.
  • DEMOKRASIA
  • MALENGO 17 YA MAENDELEO ENDELEVU (SDGs THE 17 GOALS | Sustainable Development )
  • UMASIKINI WA RAIA
  • DENI LA TAIFA KUPAA
  • GHARAMA ZA MAISHA
  • TOZO ZA KODI, JE NI RAFIKI NA ZINALIPIKA ?
  • SERIKALI KUENDESHA IKULU TATU (3) ; CHATO, ZANZIBAR, DAR NA DODOMA
  • UTAWALA BORA UNATOA NAFASI RAIS KUWA MFARIJI NA MUUNGANISHA TAIFA
  • "MKOSI" / "HIYANA" YA BUNGE LA CHAMA KIMOJA NDANI YA KATIBA YA VYAMA VINGI
  • ELIMU YA KUJITEGEMEA ILI VIJANA WAJIAJIRI
  • AFYA NA SIHA ZA RAIA
  • UWEKEZAJI TOKA NJE WAPOROMOKA TOKA US$ 2bn mpaka kufikia US$ 0.900bn
  • UFUKARA UMEZIDI
  • UWEZO WA VIONGOZI KIUONGOZI
  • NINI JIBU AU DAWA YA KUREKEBISHA MAPUNGUFU HAYA YOTE
  • RASILIMALI UTU, RASILIMALI KISIASA, RASILIMALI KIUCHUMI, RASILIMALI UTULIVU WA FIKRA, KATIBA HAI NDIYO MAPIGO YA MOYO YA TAIFA (KATIBA MPYA NDIYO NYEZO YA KILA KITU )

Source : E Digital
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mtu kusema anaitangaza Tanzania ndio najua kabisa mnaomtetea chief Hagaya hamna akili kabisa, zero brain.

Tanzania nani asie ijua? Kikwete aliwaleta hapa Bush na mkewe, Clinton na Mkewe, Obama na Mkewe, Rais wa China Hu Ji Ntao na team kutoka china, rais wa Korea na viongozi wengi wakubwa, nani asie ijua Tanzania? Media zote za Dunia zimewahi kuiandika Tanzania. Hakuna asieijua Tanzania.

Tatizo la Tanzania halijawahi kua eti haijulikani, mtu anaesema anaitangaza Tanzania ndio inaonyesha hana akili kabisa.

Hivi leo mtu atasema chirf Hagaya ni maarufu kuliko Mbuga ya Serengeti hadi aitangaze, hivi kuna kitu maarufu nchi hii kama Serengeti National park? Tatizo la nchi hii haijawahi kua eti haijulikani, shida iko kwenye unpredictability yetu, gharama kubwa za kutalii na sio kwamba hatujulikani.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Nadhani tuje na hoja jakaya alizurura DUNIA YOTE akapewa na fursa ya kuwa rais kutokea africa aliye enda kumuona obama

Lakini hakuna alichofanya mimi nakueleza kuwa hakuna mtu anayezurura akawa anaipenda nchi yake

Mtu anayependa kwake hazururi ila anakuwa na maono ya kwake

Nchi yetu itashuka kiuchumi MAGUFULI HII NCHI ALIJARIBUBKUIOMBOA

alikuwa shupavu sasa tunaona mambo magumu sana

Mfano serikali ya awamu ya sita sijaona mbiu kazi yake au hii serikali inalega kipi nadhani
Tusianze kusifia jakaya

Alizurura kote aliacha masikini haina hata ndege hakuna meli

Kila kitu kilikuwa hovyo kuvaa tu tshirt ya ccm kariakoo ilikuwa laana

Lakini sasa tunawaona na hizo nguo kila mahali

Hivyo tunaomba rais aache ziara nyingi
Jakaya alifanya vema sana acha uongo.
 
UPUUZI MTUPU!!!

Rais Samia Suluhu Hassan anaipaisha Tanzania kimataifa kisiasa na kiuchumi.

Rais Samia Suluhu Hassan alianza na ‘Royal Tour’ kama sehemu ya kui - brand Tanzania katika uso wa dunia, na sasa safari hii ya New York pamoja na kuhudhuria Baraza la Umoja wa Mataifa na mikutano mingine, itatumika kama sehemu muhimu ya kuitangaza Tanzania kimataifa.

Katika dunia ya leo, kuvutia wawekezaji, kuongeza watalii ni masuala ya kibiashara zaidi kuliko siasa, ndiyo maana nchi lazima ijitangaze kama bidhaa yenye ubora na inayovutia kuliko zote.

Wataalamu wa masoko wanajua umuhimu wa jina la bidhaa kutajwa tajwa mara kwa mara kwa wateja waliodhamiriwa huifanya bidhaa hiyo kuzoeleka kwa wateja kiasi kwamba kila inapotokea mtu anahitaji bidhaa hiyo harakaharaka humuijia jina au ‘brand’ anayoisikia mara kwa mara.

Vivyo hivyo kwa utalii na uwekezaji, mtalii anapotaka kufanya safari yake kama nchi zina vivutio vinavyofanana, mara nyingi huamua kwenda kule ambapo amekusikia zaidi kuliko kule ambako hajawahi kupasikia. Kwa sababu mtalii siyo mfumbuzi mfano wa kina Christopher Columbus, hupenda anapotumia pesa zake awe na uhakika wa kile atakachokipata, ni vigumu sana kwenda kubahatisha sehemu asiyoijua au kusikia chochote kuihusu.

Vivyo hivyo mikutano ya wawekezaji wakubwa pamoja na mambo mengine wanapoamua kwenda kuwekeza mahali wanataka wawe na uhakika na aina ya nchi wanayokwenda kufanya nayo kazi, wanaijua na wanawafahamu viongozi wake na labda wamewahi kukutana kwenye pembezoni mwa mikutano mikubwa ya kimataifa.

Ndiyo maana pamoja na Toyal Tour, safari hii ya New York itaongeza ushawishi wa kutajwa Tanzania kwenye maskio ya dunia, na kuingozea Tanzania ‘visibility’ katika masuala ya kimataifa.

Rais akiwa katika mikutano mikubwa namna hiyo ya kiwango cha dunia, anakutana ana kwa ana na viongozi wenzake na wakubwa wa mashirika na taasisi muhimu duniani ambapo ni rahisi kufanya ushawishi kwa manufaa ya Tanzania kuliko pengine popote.

Septemba 23, Rais Samia atakapokuwa analihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kama Rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania, mtazamo wa dunia kuhusu Tanzania hautabaki kuwa ule ule, uko ushawishi atakaouongeza hasa kutegemea na aina ya hotuba atakayotoa.

Kwa kufanya hivyo ziara hiyo hasa kwa kuwa inakwenda sanjari na uandaaji wa makala za runinga za Royal Tour kutaiongeza Tanzania ‘visibility’ kimataifa na kuiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuvutia watalii na wawekezaji wengi zaidi.

Kwa hatua hizi anazochokua Rais Samia kuelekea ujenzi wa Taifa imara na uchumi wenye nguvu, tunahitaji kumuunga mkono na kumtia moyo ili kwa pamoja tuisogeze Tanzania Mbele

Tanzania Unforgettable
Kazi Iendelee
 
Fukuzia TEUZI ongeza speed wakusikie kwa karibu. Mtu usiye na msimamo.
Kiukweli nashangaa sana, ninaposikia watu wanao onekana kama they are intelligents lakini wanawaza kama vilaza.

Japo kwa sasa ni kweli nimepigika, ils ni wajinga tuu na vilaza tuu, wasio na uwezo to read in between the lines ndio wanaodhania Pasco Mayalla anafukuzia teuzi.

Kama una mtu TRA, mwambie aangalie TIN number yangu, imelipa kodi kiasi gani 2010 -2015, then calculate mtu mwenye kulipa kodi hiyo, autafute u DC/RC/DED for what ?!. Kinachotakiwa ni Kampuni yangu tuu ya PPR, irudishiwe zile tenda zake tumsaidie Samia kulipa mishahara ya watumishi 10 wa umma, wakiwemo ma DC 5, ma RC 3, na Wakurugenzi 2.
P
 
Uongo huu peleka kwingine. Wachumia tumbo hapa JF wanajulikana wazi kabisa. Ni watu ambao hawajitambui na hawana misimamo hata chembe. Unakuwaje msomi halafu huoni udikteta, dhuluma na udhalimu wa dikteta mwendazake/Chifu hang ya? Kila leo ni kuunga mkono hoja tu za kipuuzi kusifia yasiyostahili kusifiwa. Nchi iko njia panda kila kitu hovyo uchumi ulianza kuyumba tangu 2016 lakini wewe mchumia tumbo hukuliona hilo na COVID-19 ikaumalizia kabisa. Sera MUFILISI zilizoua uchumi bado zinaendelezwa lakini bado hujastuka tu!!! 😩😩😩

Back
Top Bottom