Rais Samia Suluhu awaapisha Mabalozi Ikulu. Asema Tozo za Miamala zitaendelea ila zitarekebishwa

Muache Togolani wa watu. Alikaa benchi miaka 6.
Hakuwa bench mzee, alikuwa bado anahudumu private office ya JK na analipwa na serikali kama kawaida pia bado ni mtumishi wa Foreign Affairs.

Kimsingi alimuepuka bwana yule kwake naona ilikuwa afadhali maana watuwa JK aliwatoa kwenye reli kabisa.
 
Bila shaka wapo wamekaribia kustaafu
Kwanini awateue kipindi hiki, ili waanze kula mishara ya bure wakisubiri waliopo wastaafu? Rubbish.

Inamaana nchi ina pesa nyingi zisizo na kazi hivyo ameamua kuzitafutia matumizi. Wote watahiji magari ya hadhi ya 'kibalozi', nyumba, mishahara na kila stahiki za wadhifa huo. Stupidity.

Ngoja twende naye hivyo hivyo kigagula wetu, labda ndiyo bado anaupiga mwingi(as if I know what the shit means).
 
Ahsante sana Rais wangu kwa msimamo THABITI kwa mwendo huu tutafika vizuri.

nadhani wanao pima kina cha maji kwa rula bado hawajui kina vizuri.

nafurahia sana makato haya yaendelee kama kawaida watazania wengi wanataka kero zao za maji, elimu, afya na miundombinu itatuliwe na sote tuko tayari kuchangia maendeleo yetu, marekebisho kidogo tu.

kazi iendeleee.

tulipe tozo kwa maendeleo yetu ss wenyewe.

Mungu ibariki Tanzania
 
Ahsante sana Rais wangu kwa msimamo THABITI kwa mwendo huu tutafika vizuri.
nadhani wanao pima kina cha maji kwa rula bado hawajui kina vizuri....
Tatizo wao wanalegeza mikanda sisi tunakaza.Matumizi mabaya ya Kodi zetu
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan awaapisha Mabalozi 13, Ikulu Dar es Salaam

==========

Anaeongea kwa sasa ni waziri wa mambo ya nje, balozi Mulamula ambae anamshukuru kwa Imani kubwa ambayo amewekeza kwao na wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki. Amesema ameishi katika wizara hiyo kwa miaka mingi na hakumbuki kama ishawahi kutokea hivyo.

Amesema mabolozi sita katika walioapishwa leo ni wanawake hivyo uwiano wa kijinsia umezingatiwa na wengi wao wana umri chini ya miaka 45 na tuezi zimengatia pande zote za muungano, wapo mabolozi wametoka nje ya wizara kuleta utaalamu na uzoefu tofauti.

Waziri Mulamula anasema wizara kwasasa inaongozwa na wanadiplomasia na amewafilisi visingizio

Amesema wakati Rais Samia anakutana na mkurugenzi wa CDC leo, ameelezea umuhimu wa diplomasia ya afya

Baada ya waziri Mulamula kutoa nasaha, anamkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Samia Suluhu: Ni uteuzi wa vijana wengi wenu chini ya miaka 45, hatujawapa mkale ujana bali sasa ni mtandao na vijana waweza zaidi kupekua pia imani yetu mtakuwa wepesi zaidi kuliko wazee. Pia tumechukua kutoka maeneo tofauti, fani tofauti.

Niwape hongera na nna uhakika kazi iliyo mbele yenu mtaiweza tu. Kuteuliwa kwenu kunaonyesha kwa viwango vya uaminifu mmevionyesha kwa serikali yenu. Wakati nnawapongeza mkumbuke mna majukumu makubwa mbele yenu. Toka nimekuwa Rais nyie ndio mabalozi wa kwanza nnawateua, kazi iendelee msiniangushe.

Dunia yetu leo inakumbwa na janga la covid19, asubuhi ya leo tulikuwa na mkurugenzi wa CDC na akasema ndani ya jumuiya kuna misaada mingi kwa ajili ya Covid lakini sijasikia kutoka kwenu, mjifunze kutafuta kwaajili ya nyumbani.

Kuhudumia ofisi ya kidiplomasia ni gharama lakini tunafanya kushirikiana na wengine na kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini, tunabadilisha sera za uwekezaji

MIAMALA

Tulianza huu mfumo Julai lakini wananchi walilaalmika na tulitumia kama wiki na baadae nikawataka mawaziri wawili wakae walifanyie kazi, tunatarajia maoni ya kamati keshokutwa.

Tuliyaweka kwa nia njema, njia za vijijini hakuna na sehemu kubwa ya fedha hii itaenda kwenye njia za vijijini wakulima wasiozewe na mazao pia kwenye maji.

Tumesikia vilio lakini tozo zipo, tutaangalia njia nzuri.

MBOLEA

Kuna kilio cha kupanda bei mbolea kutoakana na makumpuni mengi yalikuwa yamefungwa nje baadae ikajulikana hili janga lipo kazi iendelee hivyo wakafata Magufuli Philosophy hivyo kuna kunyang'anyana mbolea, serikali inajitahidi kuhakikisha mbole iko hapa, pia kuna kiwanda Dodoma kinamalizika, tutatoa msukumo.


Mama Ushungi anaupiga mwingi sana
 
Anakomalia Utalii wakati amekwishaleta hofu ya Corona nchini, anategemea watalii wa kutoka wapi?

Tatizo ni corona ktk nchi zinazoleta watalii Tz.

Utalii utakuja kukaa sawa mwaka 2023 kama dunia itaweza kuidhibiti corona.

Badala ya kukomaa na utalii tulipaswa kukomaa na kilimo, ufugaji, na uvuvi.
 
Back
Top Bottom