Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, akiwa Igunga mkoani Tabora leo, Jumatano Septemba 10, 2025, ametoa wito kwa wafugaji wa mkoa huo kupeleka mifugo yao kwenye chanjo na utambuzi ili kuiweka Tanzania katika viwango vinavyokubalika kimataifa katika soko la mifugo...