Rais Samia Suluhu ahutubia Mabunge ya Kenya: Biashara kushamiri, Vikwazo Mipakani kutatuliwa, Udugu kudumishwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Analihutubia Bunge la Kenya litakalojumuisha Wabunge wa Mabunge yote mawili ya nchi hiyo.

=======



Rais Samia Suluhu Hassan
Nina furaha kubwa kupata nafasi ya kuhutubia kikao cha pamoja cha Bunge la Seneti na la Kitaifa Nchini Kenya - Tanzania tuna Bunge moja. Kwangu, ndio mara ya kwanza kuhutubia Bunge lenye chemba mbili. Sio jambo dogo na ni heshima iliyoje

Tumeguswa sana na Heshima na Ukarimu mliotuonesha. Sisi Tanzania tutalipa wema huu - Namshukuru Kaka yangu Rais Uhuru Kenyatta kwa kupiga simu na kutufariji tulipofiwa na Dkt Magufuli. Hatutasahau kitendo chake cha kutukumbusha kuheshimu Dini za wengine

Nilikwenda Uganda kusaini Mkataba lakini haikuwa ziara rasmi. Ziara yangu rasmi tangu kushika Uongozi nimeanzia Kenya - Nimeanza Kenya sio kwasababu ni karibu kijiografia lakini ni kwasababu ya Umuhimu wa Kenya ndani ya Tanzania

Busara inaelekeza kuwa ukiwa mpangaji mpya lazima ujitambulishe kwa majirani - Nami nimekuja Kenya kuitikia mwito wa Rais Uhuru Kenyatta. Nimebaini sehemu kubwa ya ujumbe nilioambatana nao wanajua vichochoro vya Nairobi, wanajua nyama choma inapatikana wapi

USHIRIKIANO WA TANZANIA NA KENYA
Rais Uhuru Kenyatta ni mtu wa kutimiza ahadi. Ili kuondoa mitazamo hasi tumepanga kukutana mara kwa mara, kwa maana ndugu wanaotembeleana undugu na uhusiano wao unaimarika - Umbali hujenga mashaka na ukaribu huondoa mashaka

Ushirikiano wa Tanzania na Kenya sio wa hiari. Wanyamapori wanakuja kupata mimba Kenya wanarudi kuzaa Tanzania. Kama Wanyama wana udugu sisi wanadamu tunatengana wapi? - Ushirika na ujirani vinatufanya tuwe pamoja. Tupendane au tuchukiane hatuwezi kukwepa kuwa pamoja

Iwe kheri au shari, iwe neema au dhiki tunategemeana. Panapotokea ukame Tanzania, njaa inabisha hodi Kenya - Panapotokea uzalishaji ukasimama Kenya bidhaa zinakosekana Tanzania. Hivyo, hapana budi tupatane, tushikane ili tuishi kwa neema na furaha.

Binafsi huwa nashangazwa sana na wale ambao wanadhani kuwa eti Kenya na Tanzania ni washindani na kwamba uhusiano wetu unapaswa kuwa wa kukamiana - Mbaya zaidi ni kule kuamini kwao kwamba hilo linawezekana tu mmoja wetu kumwangusha mwenzake

Binafsi huwa nashangazwa sana na wale ambao wanadhani kuwa eti Kenya na Tanzania ni washindani na kwamba uhusiano wetu unapaswa kuwa wa kukamiana - Mbaya zaidi ni kule kuamini kwao kwamba hilo linawezekana tu mmoja wetu kumwangusha mwenzake

WAFANYABIASHARA/BIASHARA
Wafanyabiashara nendeni mkashirikiane na sio kushindana, mna bahati kwamba katika Nchi zetu hizi mbili upande mmoja kuna Uhuru wa kufanya biashara na upande mwingine kuna Suluhu ya kuondosha vikwazo vya biashara, hapo mshindwe nyinyi tu.

Tunavyo vituo vya pamoja mipakani ambavyo vimerahisisha shughuli katika mipaka ya Kenya na Tanzania - Ktk ushoroba wa Pwani tuko mbioni kukamilisha kipande cha Pangani Bagamoyo na Uhuru ameniambia yuko mbioni kukamilisha mazungumzo ya kupata fedha ili tumalizie.

Vyovyote itakavyokuwa, lazima tushirikiana na majirani zetu wakiwemo Kenya - Tuna miradi mikubwa inayotaka ushirikiano kati ya Mataifa haya mawili. Yeyote anayedhamiria kuleta uhasama kati yetu, aelewe tulikuwepo, tupo na tutaendelea kuwepo.

Tumekuwa na mazungumzo mazuri na yenye kuamsha matarajio makubwa sana kwa Nchi zetu mbili. Kwa yale tuliotofautiana, hayakuwa na misingi ila tu ni mitazamo tofauti ya Watu - Uchungu wowote uliojitokeza ulikuwa uchungu wa uzazi na sio wa maradhi.

JANGA LA CORONAVIRUS
Dunia inakabiliwa na janga kubwa la Corona ambalo limeathiri kwa ukubwa ukuaji wa Uchumi wetu. Leo Corona imebadili mfumo wa maisha yetu na kutufanya tufunge midomo na pua kama tulivyokuwa tukiwafunga Mbuzi tukiwapeleka kwenda kula.

Sisi Tanzania sio Kisiwa, tunaishi kama sehemu ya Jumuiya ya Kimataifa hivyo kupitia Kamati ya Wataalamu niliyoiunda tumeanza mchakato wa kutafakari mbinu zaidi za kukabiliana na janga hili huku tukisubiri mapendekezo na hatua zaidi za kuchukua.

Badala ya kunyang'anyana idadi ya watalii, busara itumike tumshawishi mtalii aongeze siku za kukaa Kenya na Tanzania. Kenya ikiwa salama, Tanzania iko salama, pia Tanzania ikiwa salama na Kenya iko salama.

Chini ya uongozi wangu, tutafanya kila tunachoweza ili kuimarisha uhusiano wetu. Dira ya Serikali yangu ni kudumisha ya Awamu iliyopita na kuendeleza mapya. Kama kuna ambalo linalega au uhusiano wetu unasuasua nimekuja kuyanyoosha yale yaliyojipinda pinda.

Mwl. Nyerere alisema tukipoteza muda mwingi kunyang'anyana kibaba, tutapoteza muda mzuri sana wa kuvuna kikubwa zaidi.

Mabunge yenu ya Kenya yanatusisimua kwa mengi, tunafurahia upana wa Demokrasia yake, uzito wa mijadala na hamasa ya Wabunge.

Tulifurahishwa zaidi na uamuzi wenu wa kuanza kutumia lugha ya Kiswahili Bungeni, na-enjoy Kiswahili chenu kina vionjo vingi.

=====

Habri zaidi...

MHESHIMIWA SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ALIHUTUBIA BUNGE LA KENYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 05 Mei, 2021 amehutubia Bunge la Kenya lililojumuisha Bunge la Taifa na Bunge la Seneti ambapo ametoa wito kwa Wabunge hao kuchochea uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na Kenya. Mhe. Rais Samia ambaye anakuwa Rais wa pili wa Tanzania kuhutubia Bunge la Kenya akitanguliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewashukuru Maspika na Wabunge wa Kenya kwa kukubali awahutubie na amebainisha kuwa huo ni uthibitisho wa udugu, urafiki, ujirani na nia njema ya Wabunge na Mhe. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kukuza zaidi uhusiano uliopo na Tanzania.

Katika hotuba hiyo, Mhe. Rais Samia amesema haoni sababu ya Tanzania na Kenya kushindana bali anaona fursa ya kushirikiana zaidi katika uchumi kwa kuwa uhusiano wa nchi hizi ilioanza miaka 56 iliyopita sio wa hiari kutokana na kufungamanishwa uhusiano wa damu kwa jamii zilizopo pande zote, historia kutokana na kuwepo uhusiano hata kabla ya uhuru na jiografia kutokana na kuwa na mpaka mrefu na maeneo yenye rasilimali zilizoungana ikiwemo hifadhi na wanyama. Ameahidi kuwa katika kipindi chake cha uongozi atahakikisha uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na Kenya unaimarika zaidi na ametoa wito kwa viongozi na watumishi wa Serikali kuendana na kasi ya ushirikiano waliyonayo wananchi kwani hivi sasa hali inaonesha wananchi wa Tanzania na wananchi wa Kenya wanashirikiana zaidi ikilinganishwa na namna viongozi na wafanyakazi wa Serikali wanavyoshirikiana.

Pia, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuendeleza miradi ya ushirikiano ikiwemo ujenzi wa barabara, ujenzi wa bomba la gesi la Dar es Salaam – Mombasa, ujenzi wa njia ya umeme ya kilovoti 400 kutoka Singida Tanzania kwenda Kenya, kukamilisha vituo vya huduma za pamoja mpakani (One Stop Border Post) na amesisitiza kuwa yeyote anayefikiria kuichonganisha Tanzania na Kenya ajue kuwa uhusiano wa nchi hizi ulikuwepo, upo na utakuwepo sana. Amewataka Wabunge hao kuwaongoza wananchi katika kuimarisha uhusiano huo badala ya kuudhohofisha na kwamba hata yeye amefanya ziara hiyo ili kurekebisha maeneo yote ambayo yalikuwa yanalegalega jambo ambalo limefanikiwa sana baada ya mazungumzo yake na Mhe. Rais Kenyatta. “Kuongoza ni kuonesha njia sio kufunga njia” amesisitiza Mhe. Rais Samia na kubainisha kuwa pale kunapotokea tatizo kati ya pande hizi dawa iwe ni kulitatua badala ya kuliendeleza.

Kabla ya kuhutubia Bunge, Mhe. Rais Samia amekutana na wafanyabiashara wa Tanzania na Watanzania waishio Kenya (Diaspora) na amewaambia kuwa katika kipindi chake cha uongozi amedhamiria kukuza uchumi kwa haraka na hivyo ametoa changamoto kwa sekta binafsi kujipanga vizuri kutumia fursa mbalimbali ambazo Serikali ya Awamu ya Sita itazifungua na kuondoa vikwazo mbalimbali vya biashara. Ametaja baadhi ya fursa hizo kuwa upanuzi wa huduma za bandari zitakazokidhi mahitaji na kwendana na kasi ya kukua kwa uchumi, kuanzishwa kwa maeneo maalum ya viwanda (industrial parks) yatakayozalisha bidhaa na kuajiri Watanzania wengi, kukuza na kuendeleza kilimo na amewaonya wale ambao wameshikilia maeneo makubwa ya mashamba lakini hawayaendelezi kuwa Serikali itayatwaa maeneo hayo na kuwapatia waliotayari kuzalisha mazao.

“Nataka kwenda faster, nataka kufuangua nchi, yeyote anayetaka kuwekeza aje awekeze yeye apate na sisi tupate, najua wawekezaji wengi watakuwa wa nje lakini nawaomba na nyie mchangamke na mtumie vizuri fursa za ndani zitakazojitokeza (local content)” amesisitiza Mhe. Rais Samia. Mhe. Rais Samia ameitaka sekta binafsi ya Tanzania kumuunga mkono katika dhamira hiyo na amewaomba wafanyabiashara na wawekezaji waliowekeza nje ya Tanzania kurudi kuwekeza Tanzania kwani nyumbani kumenoga.

Pia amewataka kuijulisha Serikali pale watakapoona jambo lolote halipo sawa zikiwemo sheria kandamizi ili zifanyiwe kazi. Mhe. Rais Samia ameagwa na Mhe. Rais Kenyatta na amerejea Jijini Dodoma nchini Tanzania akitokea Jijini Nairobi nchini Kenya baada ya kumaliza Ziara Rasmi ya siku 2 nchini humo.
 
Mwanzo kulikuwa na uhuru na makufuli mfunga biashara za watu.
 
Mmh... keep your friends close and your enemies closer!....bonge moja la speech,kama humuelewi mama basi utamuelewa baadae.
 
Hongera sana kwa mhe. Rais mama Samia.

waswahili husema Uungwana ni Vitendo, umeonyesha vitendo vya muungwana sana kwa Taifa la Kenya.

Amethibitisha kuwa kweli Tanzania na Kenya sio tu Majirani bali sisi ni ndugu.

Amefufua Matumaini mapya kwa wananchi wa mataifa yote, Hongera sana kwa Mhe. Rais wa Kenya Uhuru.

Mmeimarisha Ujirani wetu.

Sasa tuchape kazi, tufanye biashara, tuwekeze kwa masilahi ya wananchi.
 
Mama Samia is on a Diplomatic Charm Offensive from the word GO.

Watanzania kwa kwei tumefurahu, sasa tunaongea na wenzetu majirani na dunia nzima kwa wavelength moja inayoeleweka.

Kuwa na uhusiano mzuri na jirani yako si tu jambo la msingi bali vile vile ni hesabu nzuri kibiashara.

Kuna watu wanlaumu kila step ya Mama , lakini hao tuwasamehe kwani hawajui potential ya urafiki, inavyoweza kuibua biashara ambazo hata wao hawakutazamia.

Go, Samia! GO!
 
Mama Samia is on a Diplomatic Charm Offensive from the word GO.

Watanzania kwa kwei tumefurahu, sasa tunaongea na wenzetu majirani na dunia nzima kwa wavelength moja inayoeleweka.

Kuwa na uhusiano mzuri na jirani yako si tu jambo la msingi bali vile vile ni hesabu nzuri kibiashara.

Kuna watu wanlaumu kila step ya Mama , lakini hao tuwasamehe kwani hawajui potential ya urafiki, inavyoweza kuibua biashara ambazo hata wao hawakutazamia.

Go, Samia! GO!
Kwa kweli Mama Samia anatoa moyo katika kuendeleza ushirikiano na nchi jirani.
 
mMadui ndiyo nguzo ya maendeleo, tujitahidi tupate walau nchi moja ya kuichimba mkwara na ninapendekeza iwe Chad.
 
Mama Samia is on a Diplomatic Charm Offensive from the word GO.

Watanzania kwa kwei tumefurahu, sasa tunaongea na wenzetu majirani na dunia nzima kwa wavelength moja inayoeleweka.

Kuwa na uhusiano mzuri na jirani yako si tu jambo la msingi bali vile vile ni hesabu nzuri kibiashara.

Kuna watu wanlaumu kila step ya Mama , lakini hao tuwasamehe kwani hawajui potential ya urafiki, inavyoweza kuibua biashara ambazo hata wao hawakutazamia.

Go, Samia! GO!
Amekunogeshaeh! Ngoja waweke dole kwenye karatasi
 
CRDB wamfungulie Rostam akaunt isiyo na makato (bank charges) na mama wamfungulie Malkia akaunti. Pesa ya kufungulia akaunti nitaleta mimi kama zawadi. They have done a very nice job in Nairobi.
 
Rais Samia amemshukuru Spika wa Bunge la Kenya kwa kumpa heshima ya kuhutubia Mabunge mawili ya nchi hiyo kwa pamoja.

Rais Samia amesema yeye ni Rais wa pili kutoka Tanzania kupewa heshima ya kuhutubia bunge hilo linaloheshimika duniani akiwa ametanguliwa na Mstaafu Jakaya Kikwete.

Rais Samia amesema Bunge la Kenya linavutia kwa upana wa demokrasia yake.

Kazi Iendelee!
 
Back
Top Bottom