Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,991
Moja ya kauli za mwanzo kabisa za Rais Samia ambazo zilileta msisimko nchini ni kusudio lake la kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani.
Msisimko ulitokana na ukweli kwamba Rais Magufuli hakuwa na mpango wa aina hiyo kabisa, badala yake mkakati wake ulikuwa kuviua kabisa vyama vya upinzani. Na kwa kweli alitumia muda na nguvu nyingi kuvisambaratisha: kesi kila kukicha, mapambano yasiyokwisha na jeshi la polisi, hujuma mahakamani, hujuma za Tume ya Uchaguzi, kupora wanachama wa upinzani, nk. Serikali ya Magufuli iliwaandama pia viongozi wa vyama vya upinzani, kwa kutumia TRA, mabenki, ikiwa ni pamoja na kuvuruga mapato yao binafsi, kufunga akaunti zao, nk.
Kwa hiyo kauli ya Rais Samia ya kukutana na hawa viongozi, iliashiria mwanzo mpya. Pia chama kikuu cha Upinzani, CHADEMA , walimwandikia barua Rais kuomba kukutana naye. Barua hiyo ilijibiwa na Ikulu kwa jibu la ndiyo.
Ishara ya mwanzo kwamba nia ya Rais kukutana na viongozi wa vyama vya Upinzani kwa ujumla, na CHADEMA, imeingia doa, ni pale hakugusia tena suala hilo, kila mara aliporejea mikakati yake kuhusiana na Demokrasia na Utawala Bora.
Upo uwezekano mkubwa kwamba mara baada ya Rais kutamka nia yake kukutana na viongozi wa vyama vya Upinzani, Wahafidhina ndani ya CCM walifaulu kumshawishi aachane kabisa na "mchezo huo wa hatari".
Ni wazi kwamba jaribio la CCM chini ya uenyekiti wa Kikwete, kuviacha vyama vya Upinzani kufanya siasa kwa kiwango fulani cha uhuru, kwa maoni ya Wahafidhia wa CCM, kiliwagharimu vikubwa. Vyama vya upinzani vilijiimarisha sana, na CCM iliporomoka vibaya.
Na kilichofanyika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2019 na pia uchaguzi mkuu 2020, ilikuwa ni sawa na kuvifunga kamba mikono na miguu, kitambaa usoni, na kuvipambanisha na CCM kwenye ulingo. Wapo wanaoamini kwamba CCM imepanda chati. Kama ilihitajika kuvifunga kamba vyama vya Upinzani ili kuvipunguza nguvu, hiyo ni habari mbaya sana kuhusu hali ya CCM kama chama cha siasa.
Ishara ya pili kwamba Rais Samia kapata kigugumizi katika azma yake ya kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani pamoja na CHADEMA , ni ule ukimya wake.
Hata pale viongozi hawa walipoanza kulalamikia ukimya huu, Rais alibakia kimya. Kauli yake leo kuwataka "wananchi wajiepushe na wanaotaka kuleta chokochoko" ni msumari wa mwisho kwenye jeneza la mkakati wa kukutana na viongozi wa upinzani.
Hoja zote mbili: Kukutana na wapinzani , na suala la katiba mpya, zinaashiria habari mbaya kwa CCM. Kukutana na wapinzani maana yake CCM na serikali yake wafuate sheria za mchezo. Uchaguzi halali, Tume Halali ya uchaguzi . Lakini CCM ni waoga mno!
Katiba Mpya, angalau kwa mujibu wa Rasimu ya Warioba, inaelekeza kupunguzwa madaraka ya Rais, Tume huru ya uchaguzi , kwa uchache. Hizi zote siyo habari njema kwa CCM.
Kwa hiyo, ni kama Rais Samia hana njia isipokuwa kuendeleza Umagufuli, kuwaziba mdomo na kuwafunga kamba viongozi wa upinzani, nakutokukubali kabisa mchakato wa Katiba Mpya.
Njia pekee ni CCM kukubali kuheshimu sheria za mchezo, hata kama itamaanisha "kushuka chati"