KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,601
Wahenga walisema Kwa 'shujaa uenda kilio ila Kwa mwoga huenda kicheko' ,huu msemo unaweza kutumika kuelezea Kwa kirefu maisha ya vyama vya siasa vya upinzani Tanzania.
Kwa mtazamo wangu kulingana na siasa zetu, Kuna makundi matatu ya vyama vya upinzani.
Kundi la kwanza, vyama majasiri
Kundi la pili, vyama vioga
Kundi la tatu, kundi la kati halipo kwenye majasiri au waoga.
Makundi yote matatu ya vyama vya upinzani ,yanaamini aduo yao ni mmoja ambaye ni CCM. Ni adui mwenye nguvu lakini anaongezeka nguvu maradufu anapopambana au anapolinda himaya yake. Makundi yote matatu yanajaribu kupambana naye bila kujua watapambana naye vipi, ukizingatia kundi la waoga linaogopa kabisa na kundi la kati haliaminiki maana halijulikani ni muda gani watakuwa majasiri au waoga.
Yote Kwa yote Kila kundi limetafuta namna yake ya kupambana kivyake.
Kundi la waoga linapambana kiuogauoga na mkakati huu utawasaidia sana. Wanapamba Kwa namna ya kumchosha adui upande mmoja na hapa ndio wahenga wanatukumbusha kwamba Kwa muoga huenda kicheko. Kwa kuwa wanapambana kiuogauoga ,wameona njia pekee ni kumuunga mkono Rais Samia kwenye Urais Kwa maana ya kwamba wameogopa nguvu ya CCM kwenye eneo hili na wameamua kujikita kwenye ubunge.
Kundi la vyama majasiri ndio kundi linaloelezewa na wahenga kwamba Kwa shujaa huenda kilio. Kundi hili linaamini litaishinda CCM Kila eneo na huu ujasiri ndio utakuwa anguko lao. Kwa kuwa CCM ni adui mwenye nguvu na nguvu zake zinaongezeka maradufu anapopambana basi inawezekana kundi hili likakutana na mpambano mkali mno .
Kundi la kati Sina mengi ya kulizungumzia Kwa sababu lenyewe halina athari za Moja za Moja zaidi ya kujimaliza lenyewe.
Kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 mengi yatashuhudiwa lakini linalosisimua zaidi ni kundi la vyama vioga vinavyopamba na CCM kiuogauoga kuibuka mashujaa na kicheko ila Lile kundi lingine lihesabu maumivu na kilio.
Kama ukikutana na adui mwenye nguvu kuliko wewe, chukua maamuzi yafuatayo:
Kwanza, kimbia bila kupambana
Pili, pambana ukijiandaa kukimbia muda wowote
Tatu, mchoshe kwenye eneo lake dhaifu