Rais Samia kutoka nia ya kukutana na vyama vya upinzani hadi "Ngoja tuimarishe uchumi kwanza"

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,446
2,000
Moja ya kauli za mwanzo kabisa za Rais Samia ambazo zilileta msisimko nchini ni kusudio lake la kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani.

Msisimko ulitokana na ukweli kwamba Rais Magufuli hakuwa na mpango wa aina hiyo kabisa, badala yake mkakati wake ulikuwa kuviua kabisa vyama vya upinzani. Na kwa kweli alitumia muda na nguvu nyingi kuvisambaratisha: kesi kila kukicha, mapambano yasiyokwisha na jeshi la polisi, hujuma mahakamani, hujuma za Tume ya Uchaguzi, kupora wanachama wa upinzani, nk. Serikali ya Magufuli iliwaandama pia viongozi wa vyama vya upinzani, kwa kutumia TRA, mabenki, ikiwa ni pamoja na kuvuruga mapato yao binafsi, kufunga akaunti zao, nk.

Kwa hiyo kauli ya Rais Samia ya kukutana na hawa viongozi, iliashiria mwanzo mpya. Pia chama kikuu cha Upinzani, CHADEMA , walimwandikia barua Rais kuomba kukutana naye. Barua hiyo ilijibiwa na Ikulu kwa jibu la ndiyo.

Ishara ya mwanzo kwamba nia ya Rais kukutana na viongozi wa vyama vya Upinzani kwa ujumla, na CHADEMA, imeingia doa, ni pale hakugusia tena suala hilo, kila mara aliporejea mikakati yake kuhusiana na Demokrasia na Utawala Bora.

Upo uwezekano mkubwa kwamba mara baada ya Rais kutamka nia yake kukutana na viongozi wa vyama vya Upinzani, Wahafidhina ndani ya CCM walifaulu kumshawishi aachane kabisa na "mchezo huo wa hatari".

Ni wazi kwamba jaribio la CCM chini ya uenyekiti wa Kikwete, kuviacha vyama vya Upinzani kufanya siasa kwa kiwango fulani cha uhuru, kwa maoni ya Wahafidhia wa CCM, kiliwagharimu vikubwa. Vyama vya upinzani vilijiimarisha sana, na CCM iliporomoka vibaya.

Na kilichofanyika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2019 na pia uchaguzi mkuu 2020, ilikuwa ni sawa na kuvifunga kamba mikono na miguu, kitambaa usoni, na kuvipambanisha na CCM kwenye ulingo. Wapo wanaoamini kwamba CCM imepanda chati. Kama ilihitajika kuvifunga kamba vyama vya Upinzani ili kuvipunguza nguvu, hiyo ni habari mbaya sana kuhusu hali ya CCM kama chama cha siasa.

Ishara ya pili kwamba Rais Samia kapata kigugumizi katika azma yake ya kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani pamoja na CHADEMA , ni ule ukimya wake.

Hata pale viongozi hawa walipoanza kulalamikia ukimya huu, Rais alibakia kimya. Kauli yake leo kuwataka "wananchi wajiepushe na wanaotaka kuleta chokochoko" ni msumari wa mwisho kwenye jeneza la mkakati wa kukutana na viongozi wa upinzani.

Hoja zote mbili: Kukutana na wapinzani , na suala la katiba mpya, zinaashiria habari mbaya kwa CCM. Kukutana na wapinzani maana yake CCM na serikali yake wafuate sheria za mchezo. Uchaguzi halali, Tume Halali ya uchaguzi . Lakini CCM ni waoga mno!
Katiba Mpya, angalau kwa mujibu wa Rasimu ya Warioba, inaelekeza kupunguzwa madaraka ya Rais, Tume huru ya uchaguzi , kwa uchache. Hizi zote siyo habari njema kwa CCM.

Kwa hiyo, ni kama Rais Samia hana njia isipokuwa kuendeleza Umagufuli, kuwaziba mdomo na kuwafunga kamba viongozi wa upinzani, nakutokukubali kabisa mchakato wa Katiba Mpya.

Njia pekee ni CCM kukubali kuheshimu sheria za mchezo, hata kama itamaanisha "kushuka chati"
 
Halaiser

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
2,999
2,000
Awe makini na baadhi ya wale walionzunguka kwani ndio hao hao waliokuwa hawapendi kuongozwa na Rais Mwanamke. Hivi sasa wanafanya kila liwezekanalo kuhakikisha mama anagombana na makundi mbali mbali kisha akose pakupumulia akawaangukie wao.
 
mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
2,270
2,000
Sijui kitu gani kilimshinda Madam hata kwa kuanzia tu, kuruhusu mikutano ya wazi ya vyama vya kisiasa ifanyike katika siku za mwisho wa juma, hasa siku za Jumamosi na Jumapili tena kuanzia saa tisa alasiri mpaka saa kumi na mbili jioni!?
 
ikashi2

Member
Feb 28, 2020
24
75
Alijitahidi kukutana nao katika mfumo wa sheria hasa pale aliporuhusu sheria kuchukua mkondo wake. Au ulitaka amkaribishe Mdude Ikulu?
 
jailos mrisho

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
405
1,000
Samia alikuwa anawaheshimu wapinzani wakati akiwa bado hajakaa vzur kwenye system..baada ya kukaa na kuona upuuzi wa vyama vya upinzani akayatupa mafail yote na kuyachoma motooo hawezi kukutana na wachumia tumbo.
 
Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,446
2,000
Alijitahidi kukutana nao katika mfumo wa sheria hasa pale aliporuhusu sheria kuchukua mkondo wake. Au ulitaka amkaribishe Mdude Ikulu?
Hajakutana nao. Ni kweli amechukua hatua kadhaa kufuta kesi chache za kubambikiza, kufungua akaunti zilizofungwa kwa kodi za kubambikiza. Pia ameachia kidogo kwenye vyombo vya habari. Lakini alichofanya ni cosmetic. Anahofia kuweka uwanja sawa sababu kama alivyowahi kusema Polepole, CCM haiwezi kushinda katika uchaguzi huru na wa haki
 
Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,446
2,000
Hakuna haja ya msingi ya kukutana na hao vibweka wadogowadogo.
Hata asipokutana nao, inakuwaje anaogopa kuwaacha wafanye siasa kama Katiba na sheria zinavyotaka? Maana cha msingi tufuate sheria. CCM hawawezi kutoboa kama kweli wakifuata sheria. Hivi visingizio vya "uchumi ukue kwanza" ni danganya toto
 
Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,446
2,000
Awe makini na baadhi ya wale walionzunguka kwani ndio hao hao waliokuwa hawapendi kuongozwa na Rais Mwanamke. Hivi sasa wanafanya kila liwezekanalo kuhakikisha mama anagombana na makundi mbali mbali kisha akose pakupumulia akawaangukie wao.
Hiyo nayo hoja. Japo mpaka sasa hajagombana na kundi lingine lolote zaidi ya wapinzani. Au kuna taarifa imenipita?
 
Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,446
2,000
Sijui kitu gani kilimshinda Madam hata kwa kuanzia tu, kuruhusu mikutano ya wazi ya vyama vya kisiasa ifanyike katika siku za mwisho wa juma, hasa siku za Jumamosi na Jumapili tena kuanzia saa tisa alasiri mpaka saa kumi na mbili jioni!?
Ni uwoga, na pia CCM inaogopa sana upinzani. Ila naamini mama mwenyewe alikua tayari kuwaacha wapinzani wafanye siasa
 
Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,446
2,000
Samia alikuwa anawaheshimu wapinzani wakati akiwa bado hajakaa vzur kwenye system..baada ya kukaa na kuona upuuzi wa vyama vya upinzani akayatupa mafail yote na kuyachoma motooo hawezi kukutana na wachumia tumbo.
Sidhani kwamba hawajui wapinzani. Ameingia siasa muda sasa. Pia miaka 5 kama makamu wa Rais imempa uzoefu. Huyu atakuwa kapigwa stop.
Wachumia tumbo walishahamia CCM. CHADEMA hata ruzuku hawaitaki. Wanachumiaje tumbo?
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
41,647
2,000
Hata asipokutana nao, inakuwaje anaogopa kuwaacha wafanye siasa kama Katiba na sheria zinavyotaka? Maana cha msingi tufuate sheria. CCM hawawezi kutoboa kama kweli wakifuata sheria. Hivi visingizio vya "uchumi ukue kwanza" ni danganya toto
CCM wanawazidi strategy na ndio maana kila msimu wanawapiga dafrau 😅
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom