meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674

Habari za Kazi wana JamiiForums,

Katika thread hii nategemea tutaangazia ziara mbalimbali(Za nje ya nchi) za Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan na manufaa kwa taifa.

Leo tarehe 11 April 2021 Mhe Samia anafanya ziara yake ya kwanza nje ya Tanzania na ziara hii ina lengo la kusaini makubaliano ya ujenzi wa bomba la mafuta.

Tarehe 4 mei2021 Mhe Samia amezuru nchi ya Kenya na kuwahitubia wananchi wa Kenya.
Ni ziara yenye tija kwa uchumi wa Nchi. Aidha ikumbukwe mtangulizi wake Hayati Dr. John Pombe Magufuli hakuwa mpenzi wa ziara za nje ya nchi na mara nyingi alimtuma Mhe Samia Suluhu kumuwakilisha.

TUTAENDELEA KUTOA UPDATES YA ZIARA ZA NJE ZA MH RAIS SAMIA.

=====

1). Rais Samia afanya ziara yake ya kwanza nchini Uganda mnamo 11 Aprili 2021 kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa nchi mbili na kumaliza makubaliano ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka nchini Uganda.

2). Rais Samia afanya Ziara ya Siku Mbili Nchini Kenya, kuanzia 04 Mei 2021

3). Rais Samia tarehe 16 Julai, 2021 afanya ziara ya Kitaifa ya siku mbili nchini Burundi kwa mwaliko wa Rais Evariste Ndayishimiye.

4). Rais Samia tarehe 02 Agosti, 2021 afanya ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini Rwanda kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Paul Kagame.

5). Rais Samia tarehe 16 Agosti, 2021 aelekea nchini Malawi kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika kuanzia tarehe 17 – 18 Agosti, 2021.

6). Rais Samia Tarehe 24 Agosti, 2021 aelekea nchini Zambia kuhudhuria sherehe za kuapishwa Kwa Rais Mteule wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema.

7). Rais Samia tarehe 18 Septemba, 2021 aondoka nchini kuelekea New York nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo tarehe 23 anatarajiwa kulihutubia Baraza hilo.

8). Rais Samia tarehe 30 Oktoba, 2021 aelekea Glasgow, Scotland kuhudhuria Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP 26).

9). Rais Samia tarehe 10 Novemba, 2021 aelekea Cairo nchini Misri kwa ziara ya Kiserikali ya siku tatu.

10). Rais Samia tarehe Januari 28, 2022, atembelea Msumbiji. Akiwa Pemba-Msumbiji, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu ameeleza kuwa lengo ya ziara hiyo ni kudumisha Diplomasia kati ya nchi hizo mbili.

11). Rais Samia afanya ziara ya Kikazi Nchini Ufaransa na Ubelgiji kuanzia tarehe 09-19 Februari 2022.

12). Rais Samia Februari 24, 2022 aelekea Dubai Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kushiriki maonyesho ya Expo 2020

13). Rais Samia Aprili 13, 2022 aenda Marekani kwa ziara ya kikazi. Pamoja na mambo mengine anatarajiwa kushiriki uzinduzi wa filamu ya ‘Tanzania Royal Tour’ itakayozinduliwa Aprili 18, 2022 jijini New York. Alikaa siku 8

14). Rais Samia 10 May 2022 afanya ziara ya Kiserikali nchini Uganda kwa siku mbili

15). Rais Samia 23 Mei 2022 ameondoka Nchini Kuelekea Accra, Ghana kwa ajili ya Ziara ya kikazi ya siku tatu Nchini Humo

16). Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan awasili Muscat nchini Oman kwa ajili ya Ziara ya Kikazi ya Siku tatu tarehe 12 Juni, 2022

17). Leo tarehe 06 Julai, 2022 Rais Samia aelekea Dakar Senegal kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kimataifa (IDA Summit for Africa)"

18). Rais Samia 16 Agost 2022, aondoka Nchini kwenda DR Congo kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

19). 13 Sep 2022 — Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliwasili nchini Kenya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais mteule wa Kenya, William Ruto

20. Septemba 17,2022 Rais Samia alifika Uingereza ili kuhudhuria mazishi ya malikia Elizabeth II yaliyopangwa kufanyika September 19. Rais Samia kuhudhuria mazishi ya malikia Elizabeth II

21. Septemba 21, 2022 Rais afanya ziara ya kikazi Msumbiji. Rais Samia akiwa katika ziara ya Kiserikali nchini Msumbiji leo Septemba 21, 2022

22. Oktoba 4, 2022 Rais Samia ashiriki ufunguzi wa Mkutano wa World Innovation Summit for Health 2022, Qatar

23. Novemba 2, Rais Samia atembelea Beijing China Rais Samia amewasili salama China, hii hapa picha akiwa Uwanja wa Ndege Beijing

24. Desemba 13, Rais ahudhuria mkutano wa Biden na viongozi wa Africa Rais Dkt. Samia yuko Marekani kuhudhuria Mkutano wa Rais Biden na Viongozi wa Africa

25. Januari 16 -20, Rais Samia ahudhuria mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Uchumi, Nchini Uswizi Rais Samia atasafiri kwenda Uswisi Kushiriki Mkutano wa Uchumi wa Viongozi wa Dunia

26. Rais Samia afanya ziara Namibia kwa mkutano wa dharura wa SADC Rais Samia Ziarani Namibia

27. Rais Samia ahudhuria uapisho wa Rais nchini Nigeria LIVE - Rais Samia akishiriki Sherehe za Kuapishwa Rais Mteule wa Nigeria, Bola Tinubu, leo Mei 29, 2023

28. Julai 5, 2023, Rais Samia awasili Lilongwe kwa ziara ya siku 3: Rais Samia awasili Lilongwe kwa ziara ya siku 3

29. 04 Sept 2023 Rais Samia Suluhu awasili Kenya kuhudhuria mkutano kuhusu hali ya hewa barani Afrika. Rais Samia Suluhu awasili Kenya kuhudhuria mkutano kuhusu hali ya hewa barani Afrika

30. Rais Samia awasili nchini Zambia kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu. Rais Samia awasili nchini Zambia kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu

31. Novembe 4, 2023: Rais Samia Ashiriki Mkutano Maalum wa Dharura SADC Picha: Rais Samia Ashiriki Mkutano Maalum wa Dharura SADC

32. Rais Samia ashiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi unaojadili kuharakisha Mageuzi ya Kiuchumi Afrika, Jijini Marrakech-Morocco, leo Novemba 8, 2023 Rais Samia ashiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi unaojadili kuharakisha Mageuzi ya Kiuchumi Afrika, Jijini Marrakech-Morocco, leo Novemba 8, 2023

33. Rais Samia ashiriki Mkutano wa nchi, Saudi Arabia, Novemba 10, Rais Samia Ashiriki Mkutano wa Saudi Arabia na Nchi za Afrika jijini Riyadh, Saudi Arabia

34. Rais Samia aelekea Dubai kushiriki Mkutano wa Mzingira, December 3. Rais Samia aondoka nchini akielekea Dubai Kushiriki Mkutano wa Mazingira wa COP28

35. Rais Samia asafiri kwenda nchini Indonesia, January 26, 2024.

36. Rais Samia aitwa Vatican kuwa na mazungumzo na papa Francis Rais Samia aalikwa na Baba Matakatifu Francis Mjini Vatican kwa mazungumzo rasmi ya siku mbili

37. Rais Samia afanya ziara nchini Norway, Februari 13, 2024 Ziara ya Rais Samia Nchini Norway baada ya kuwasili katika Kasri la Kifalme Jijini Oslo, Februari 13, 2024

38. Rais Samia afanya ziara ya kikazi nchini Ethiopia, Februari 18, 2024. Rais Samia awasili nchini Ethiopia

39. Rais Samia atua Namibia kumzika Hayati Dkt. Geingob
 
Mama Samia ana kazi sana. Wengi wanampima huku reference point ikiwa JPM. Ndiyo shida ya kukamata uongozi huku mtangulizi wako akiwa amefanya mambo makubwa makubwa.
Hasa yale ya kuteka watu, kupiga marisasi, kufunga watu bila hatia, kuharibu uchaguzi na wizi wa Mali za umma.
 
Back
Top Bottom