Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,055
- 3,502
Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Nishani za Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuzindua Kitabu cha Miaka 60 ya Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais katika Viwanja vya Ikulu - Chamwino Dodoma tarehe 24 Aprili 2024.
View: https://www.youtube.com/live/EmRN8w3uk7w?si=SMHMMsNu_3_zvd_f
View attachment 2972854
Rais Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mama Salma Kikwete Nishani ya Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere aliyoipokea kwa niaba ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
View attachment 2972855
Rais Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mama Janeth Magufuli Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo aliipokea kwa niaba ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika halfa iliyofanyika lkulu Chamwino, Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
View attachment 2972856Rais Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Samwel Malecela kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024
View attachment 2972858Rais Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Awamu ya Tatu Mhe. Fredrick Sumaye kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
View attachment 2972923
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein vitabu vya Miaka 60 ya Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Kitabu cha Safari za Picha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 60 kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
View attachment 2972924
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Makamu Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mohamed Gharib Bilal kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
View attachment 2972926
Yaani Magufuli ni rais mstaafu halafu unajiita mwandishi wa shughuli za Ikulu?