robinson crusoe
JF-Expert Member
- Oct 22, 2020
- 740
- 1,214
Wa-TZ wenzangu!
Wakati wa Wikileak nilitambua walioendelea na hasa US wanatumia maafisa wa ubalozini ili kuzifahamu nchi walimo. Balozi zao zinatumika sana kuwaelewesha tabia za viongozi wetu; uwezo na udhaifu wao.
Ina maana Peter Greenberg alikuja akiwa director wa film lakini naaamini kupitia ubalozi wake alishafahamu tabia za rais wetu hadi mambo ya ndani, na ukiangalia film hii, rais alichotwa akili hadi akamuona ni rafiki kuliko hata sisi wa-TZ.
Ukiangalia Film ya Royal Tour kiutu uzima, (Siyo kama mtoto anayefurahia wanyama) inatia kichefu-chefu jinsi rais wa nchi alivyopunguziwa thamani hadi kufikia kuwa mcheza film akiwa ikulu. Walifikia hatua ya kuitana majina kama wana mahusiano ya ziada. Peter! Mama Samia!
Haya yangeondolewa wakati wa ku-edit! Nadhani yaliachwa makusudi na naamini kwa uhusiano huu Peter sasa atatumika kiurafiki kuwasiliana na rais moja kwa moja.
Kule twitter Maria Sarungi kaibua jingine nami nimethibitisha. Wamasai wanaitwa ni 'PRIMITIVE' na huyo director wa film na ikaachwa kama sehemu ya maelezo ya film ya Tanzania! Yaani tuna raia PRIMITIVE! Rais Samia anaambiwa Magufuli alipatwa na COVID anakubali, Yeah! wakati wa-TZ hatujawahi kuambiwa jambo kama hilo. Kwa nini haya yote yametokea?
Ikulu yetu haina usalama. Namaanisha watu wanaostahili kumulazimisha rais aendane na matakwa ya taifa na siyo uamuzi wake, hawapo na hawana nguvu hizo. Ina maana rais mzembe anaweza angamiza taifa. Tabia zake binafsi zinatambaa na anazungukwa na watu wa aina yake bila kizuizi.
Very, Very Sorry!