Ni kweli kutokana na Sera za PBS, Peter wa Royal Tour hakutakiwa kulipwa hata senti 5? Mchanganuo wa Bil. 7 zilizotumika ukoje?

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Wakuu Kwema?

peter samia.jpg

Nimekutana na habari X huko inasema kutokana na Sera za PBS (Public Broadcasting Service) wanaofanya kipindi cha Royal Tour, Peter hakutakiwa kulipwa pesa yoyote kutoka serikali ya Tanzania, sababu uhusika wake unakuwa umelipiwa kutoka kwa ufadhili wa kampuni kwenye kipindi hicho.

Sasa, kwanza Peter alilipwa Tsh. ngapi kutoka kwenye zile Bilioni 7 zilizotumika?

Na mchanganuo wa matumizi ya ukoje kwenye filamu ile yote? Kwanini hatuna taarifa hii? Kusema tu zilikusanywa bilioni 11 na kutumika bilioni 7 haitoshi.

Filamu ya Royal Tour alioneshwa kwa mara ya kwanza April 18, 2022 nchini Marekani, huku waigizaji wakuu wakiwa Rais Samia na Bwana Peter Greenberg.
 
Hata ukijua haitakusaidia kitu..
Wewe ni kijana unayetegemea kuishi maisha bora, pamoja na kizazi chako lakini hutaki kufatilia uadilifu kwa uliowapa dhamana ya kusimamia rasilimali na nchi kwa niaba yako? Wao wakidhulumu, wakipanya rasilimali ovyo, wakiwa wezi na wauaji unafikiri wewe utabaki salama?

Wewe ni moja ya wale vijana wa hovyo wenye mchango 0 waliosemwa na bwana yule!
 
Roho Tour tulipigwa kama taifa, kwanza maza alitupiga sound eti atatutajia majina ya wafadhili hadi leo kimyaaa...nadhani anajua watz woote ni mazuzu tumesahau!.
 
Roho Tour tulipigwa kama taifa, kwanza maza alitupiga sound eti atatutajia majina ya wafadhili hadi leo kimyaaa...nadhani anajua watz woote ni mazuzu tumesahau!.
Kweli tunasau haraka, likizuka jambo tunalivalia njuga upepo ukiisha na sisi tumesizi, ni huzuni. Ni muhimu kufatilia maana nchi ni yetu sote, tukikaa na kuangalia tu wote tunaharibikiwa
 
Back
Top Bottom