Royal Tour ya Rais Samia yaipaisha AICC

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), Ephraimu Mafuru amesema Tanzania imepanda hadi kuwa nchi ya tano kutoka nchi ya 11 barani Afrika kwa utali wa mikutano hatua iliyochangiwa na uzinduzi wa filamu ya The Royal Tour iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza katika banda la kituo hicho katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dares Salaam (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere maarufu kama Sabasaba, Mafuru alisema kituo kinaandaa na kuendesha mikutano ya kimataifa Afrika.

"Baada ya janga la Corona, Rais Samia alizinduaFilamu ya The Royal Tour na akazunguka duniani kuifungua kimataifa, hiyo imeweza kutupa fursa ya kuwakaribisha na kuandaa mikutano ya Kimataifa. Mwaka jana wa 2022 taasisi inayosimamia viwango vya ubora wa mikutano ya kimataifa ilitoa ripoti inayoonesha Tanzania imepanda kutoka nafasi ya 11 hadi nafasi ya tano kwa Afrika," alisema Mafuru.

Alisema hatua hiyo ina maana kubwa katika uchumi wa nchi kwani ukiangilia matumizi ya washiriki unaonesha wastani wa matumizi ya mtalii wa mikutano anayekuja Afrika anatumia Dola za Marekani 420 kwa siku.
Mafuru alisema kwa mwaka wa fedha ulioisha, AICC iliratibu mikutano zaidi ya 150 ya ndani ya nchi na ya nje zaidi ya 15 na wanaendelea kuratibu na wiki mbili zilizopita walikuwa na mkutano mkubwa duniani wa ,asuala ya Afya

"Tulikuwa na washiriki zaidi ya 1,200 kati ya hao walitoka nchi 107 duniani, tulikusanya mapato ya zaidi ya Dola za Marekani 380,000 kwa muda wa siku sita, hii inaonesha kuratibu mikutano kama hii inasaidia kunyanyua uchumi wa taifa na wadau katika mnyororo wa thamani," alisema Mafuru.

Alisema kwa kuona hilo wanaendelea na maboresho ya kumbi zake ukiwemo wa Julius Nyerere (NICC) wa
Dar es Salaam na huo wa Arusha sambamba na kuwekeza katikla kituo kikubwa cha kisasa kinachoitwa Mount Kilimanjaro Convection Center na kinajengwa Arusha.

Screenshot 2023-07-09 at 12.40.22.png
 
Back
Top Bottom