Rais Samia alijifunza wapi kuvumilia wanaomkosoa na kutweza utu wake? Uvumilivu wake una baraka kwa Taifa au aachana nao?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Hayati Magufuli alikuwa ni mwafrika tena mwenye mfumo dume. Alikuwa baba ambaye amekuzwa katika kusema ukweli na kushinikiza kutendeka kila anachotaka yeye. Alikuwa mzazi asiyependa kukosolewa na kila aliye nyanyuka kumkosoa alichapwa na kuambiwa acha utovu wa nidhamu.

Tuliokulia kwenye familia za kiafrika na tukakosa exposure wakati wote tunaamini ukiwa mkubwa wewe unafahamu kila kitu na waliochini yako hawana mamlaka ya kuhoji chochote hadi pale watakapokuwa wakubwa

Mfumo wa JPM wakuona yeye tu ndiye yupo sahihi ulipelekea atumie dola kupambana na wakosoaji wake hata wale waliokosoa kama washauri. Alifanikiwa kutengeneza kundi kubwa la watu wasifikiri kinyume na kiongozi na hivyo wasomi wengi wakageuka kuwa chawa na leo tunaona madhara yake. Wakina makamba, Nape, Bashiru, Kabudi na wengineo wamebadili Gia angani wanaomkosoa akiwa hayupo.

Kikawaida huwezi kutegemea Daktari kama Naibu waziri wa Afya asema amani ya Tanzania inatokana na Mhe. Rais tena akimtaja kwa jina. Huyu amefika mahali amemweka mama yetu nafsi ya kwanza huku Mama yetu mwenyewe kwa kinywa chake katika hotuba zake akijiweka nafasi ya chini baada ya Mungu.

Rais Samia anapongezwa leo na Dunia kwa sababu ameweza kwa kiasi kikubwa kuvumilia ukosoaji. Anatambua kwamba asipokuwa mvumilivu wasaidizi wake watatumia mamlaka vibaya kupambana na wakosoaji jambo linaloweza kupelekea aache njia yakutafuta mafanikio kama Rais aanze usuluhishi na kuwekewa kikwazo.

Rais Samia anapongezwa kwa kutumia sayansi ya siasa kukabiliana na mapungufu kama mwanadamu. Rais Samia anatumia mbinu shirikishi kukabiliana na changamoto za wakosoaji wake ikiwemo kuwasikiliza na kuzifanya kosoa zao kama daraja lakuvuka.

Moyo wa mama Samia hakuna kiongozi wa Upinzani mwenye Nao. Mdogo wetu Lissu, Mbowe na akina Zitto wote hawana uvumilivu wakusikiliza ukosoaji wa watoto wadogo na vijana ambao kwa umri wao wangeweza kuwazaaa.

Naamini Rais Samia anaongozwa na Falsafa kwamba hii nchi siyo mali ya Rais, Wazee ,vijana wala watoto ni mali ya wote. Anaongozwa na Falsafa kwamba kila raia wa Tanzania ana haki ya kuhoji na kusikilizwa. Falsafa hizi zikijengwa miongoni mwetu naamini tutaweza kukimbia kiuchumi kwani tutawataja wale wanaiba na hakuna wanaweza kutufanya.

Niwaombe wale wanaoamini kwamba kazi ya Rais ni kupambana kisheria na wakosoaji wake waanze kujifunza kwa Mama Samia. Hakuna mkosoaji aliyewahi kukamatwa kisiasa Rais akawa salama. Siku zote Rais anakuwa salama pale anaowaongoza wanapopumua na kutoa nyongo zao.

Hongera Mama waambie vijana wako wasikimbilie kunikamata kisa nakosoa, wachukue ukosoaji wangu waniprove wrong kama ambavyo wewe umeweza kuwa mvumilivu. Kukamata wakosoaji nikuwapa uhuru wakupiga kelele zaidi.....ogopeni sana hashtag ya FREE somebody
 
Niwaombe wale wanaoamini kwamba kazi ya Rais ni kupambana kisheria na wakosoaji wake waanze kujifunza kwa Mama Samia. Hakuna mkosoaji aliyewahi kukamatwa kisiasa Rais akawa salama. Siku zote Rais anakuwa salama pale anaowaongoza wanapopumua na kutoa nyongo zao.
Unatama kusemaje?
 
Acha ujingaa wako.

Nimesoma tu Kichwa Cha habari.

Inamaana Hujui ukishakua Kiongozi ,Kila takataka utatupiwa?.

Kwan HAYATI JPM hakutweza? Hakutukanwa?? Sialiitwa Mshamba??. Na aliamua kiwasamehe watu mbele ya hadhira.


Uwe mvumilivu uwe mwenye kuchukua hatua , TAIFA LINATAKA MAENDELEO YA UHAKIKA ,MAENDELEO YA VITU NA WATU.


SASA uvumilivu wake, umesaidia nn??.

Afterall huyo Mama SIO mvumilivu, ni MUOGA Tena woga wake umezidi kiasi Cha Kumfanya kua mnafiki.
 
Back
Top Bottom