Nguvu ya ushawishi wa Rais Samia imeongezeka maradufu mpaka inatishia uwepo wa upinzani na kutamani asigombee

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,601
Sikutaka kusema haya lakini ni bora niyaseme Sasa ili 2025 baada ya kampeni ndefu ninayokusudia kuifanya inayokwenda kwa jina la 2025 MPE MAMA TABASAMU kukamilika na matokeo kuonekana ,isije ikatokea watu wakapotoshwa na upotoshaji ukageuka ukweli, Kwa hiyo mada hii inabaki kuwa kumbukumbu ya rejea ya yatakayo tokea mbeleni.

Kampeni ya 2025 MPE MAMA TABASAMU ni sehemu ya mpango mkakati wa kujitolea kuufahamisha Umma juu ya kazi nzuri za Rais Samia, mara nyingine Umma unatakiwa kujulishwa ili ujue zaidi maana isipofanyika hivyo Kuna mwingine anaweza kuchukua nafasi ya kufanya hivyo.

2025 MPE MAMA TABASAMU imezingatia vigezo na sifa zifuatazo:
Kwanza, imezingatia uchapakazi wa Rais Samia, kama Rais Samia asingekuwa mchapakazi kampeni hii isingekuwa na maana na ingekosa uhalali.

Pili , imezingatia uongozi bora wa Rais Samia. Kila Kona ya dunia inatambua Rais ni kiongozi bora. Kiongozi bora ni lazima apewe TABASAMU.

Tatu, imezingatia nguvu ya ushawishi aliyonayo Rais Samia Kwa Sasa. Ni kubwa sana si tu Kwa hapa Tanzania bali Afrika na Dunia Kwa ujumla hivyo nguvu hiyo itakuwa ni msingi mkubwa wa utekelezaji wa kampeni hiyo adimu.

Kwa Leo, tuziweke kando sifa namba 1 na 2 na tujikite zaidi kwenye sifa namba 3 ambayo ni nguvu ya ushawishi.

Sitaki kujitia upofu kwamba sioni hata yanayoonekana, ninaona wala sisimuliwi. Ninaona nguvu ya ushawishi ya Rais wetu imeongezeka maradufu na inazidi kukua Kila siku na nguvu yake imekuwa ni tishio Kwa wapinzani wake wa kisiasa.

Kutokana na kuongezeka nguvu yake maradufu, Rais wetu anatazamwa kama mtu aliyeshinda 2025 kabla ya shindano kuanza. Nguvu hiyo ni tishio kweli kweli.

Ili wapinzani wake waonekane nao wamo na nguvu ya ushawishi ya Rais si lolote wameanzisha kampeni ya kuonesha Kila kinachofanywa na Rais Samia si chochote na zaidi wanatamani 2025 ASIGOMBEE.

Kwa kuwa utaratibu, utamaduni ,desturi na miiko ya CCM inajulikana kwenye suala la kugombea Kwa kiongozi anayeendelea ili kumalizia kipindi cha awamu ya pili basi 2025 MGOMBEA WA CCM NI RAIS SAMIA kama hakutakuwa na sababu yoyote itakayokuja nje ya uwezo wa kibinadamu.

Nguvu ya ushawishi wa Rais Samia inachagizwa na unyenyekevu, upole, uwezo wa kufanya maamuzi, ufuatiliaji na utendaji wake.

Kwa kuwa nguvu ya ushawishi ya Rais wetu ni kubwa sana hivyo si vema kushindana nayo maana kufanya hivyo ni sawa na jaribio la kujitoa muhanga.
 
Mkuu ingalikuwa ni vyema kama hoja yako ingalishadadiwa na takwimu ili kuweza kuthibitisha ongezeko hilo la mara dufu la ushawishi wake katika "clusters" tofauti za watu, mathalani, wafanyakazi, wakulima, wafanyabiashara, na maeneo mengine.
 
Kobe ana nguvu gani sa .hadi arudie mala nyingi ndo hoja zifanyiwe kazi .Rais inabidi uwe na kauli moja tu watu wana fyata
 
Nyie endeleeni kumdanganya Maza

Haya yalitokeaga Rombo kwa Mramba
Mramba aliamini mikopo ya Sido na Maroli aliyo wapa Warombo angepata Ubunge lakini alipoenda Slaa siku tatu kabla ya uchaguzi upepo ulibadilika hakuamini kilicho tokea

Hivyo endeleeni kumdanganya Maza hivyo hivyo!
 
Ubunge ni tofauti na Urais, itatolewa fomu Moja tu mchezo umeisha
 
Sikutaka kusema haya lakini ni bora niyaseme Sasa ili 2025 baada ya kampeni ndefu ninayokusudia kuifanya inayokwenda kwa jina la 2025 MPE MAMA TABASAMU kukamilika na matokeo kuonekana ,isije ikatokea watu wakapotoshwa na upotoshaji ukageuka ukweli, Kwa hiyo mada hii inabaki kuwa kumbukumbu ya rejea ya yatakayo tokea mbeleni.

Kampeni ya 2025 MPE MAMA TABASAMU ni sehemu ya mpango mkakati wa kujitolea kuufahamisha Umma juu ya kazi nzuri za Rais Samia, mara nyingine Umma unatakiwa kujulishwa ili ujue zaidi maana isipofanyika hivyo Kuna mwingine anaweza kuchukua nafasi ya kufanya hivyo.

2025 MPE MAMA TABASAMU imezingatia vigezo na sifa zifuatazo:
Kwanza, imezingatia uchapakazi wa Rais Samia, kama Rais Samia asingekuwa mchapakazi kampeni hii isingekuwa na maana na ingekosa uhalali.

Pili , imezingatia uongozi bora wa Rais Samia. Kila Kona ya dunia inatambua Rais ni kiongozi bora. Kiongozi bora ni lazima apewe TABASAMU.

Tatu, imezingatia nguvu ya ushawishi aliyonayo Rais Samia Kwa Sasa. Ni kubwa sana si tu Kwa hapa Tanzania bali Afrika na Dunia Kwa ujumla hivyo nguvu hiyo itakuwa ni msingi mkubwa wa utekelezaji wa kampeni hiyo adimu.

Kwa Leo, tuziweke kando sifa namba 1 na 2 na tujikite zaidi kwenye sifa namba 3 ambayo ni nguvu ya ushawishi.

Sitaki kujitia upofu kwamba sioni hata yanayoonekana, ninaona wala sisimuliwi. Ninaona nguvu ya ushawishi ya Rais wetu imeongezeka maradufu na inazidi kukua Kila siku na nguvu yake imekuwa ni tishio Kwa wapinzani wake wa kisiasa.

Kutokana na kuongezeka nguvu yake maradufu, Rais wetu anatazamwa kama mtu aliyeshinda 2025 kabla ya shindano kuanza. Nguvu hiyo ni tishio kweli kweli.

Ili wapinzani wake waonekane nao wamo na nguvu ya ushawishi ya Rais si lolote wameanzisha kampeni ya kuonesha Kila kinachofanywa na Rais Samia si chochote na zaidi wanatamani 2025 ASIGOMBEE.

Kwa kuwa utaratibu, utamaduni ,desturi na miiko ya CCM inajulikana kwenye suala la kugombea Kwa kiongozi anayeendelea ili kumalizia kipindi cha awamu ya pili basi 2025 MGOMBEA WA CCM NI RAIS SAMIA kama hakutakuwa na sababu yoyote itakayokuja nje ya uwezo wa kibinadamu.

Nguvu ya ushawishi wa Rais Samia inachagizwa na unyenyekevu, upole, uwezo wa kufanya maamuzi, ufuatiliaji na utendaji wake.

Kwa kuwa nguvu ya ushawishi ya Rais wetu ni kubwa sana hivyo si vema kushindana nayo maana kufanya hivyo ni sawa na jaribio la kujitoa muhanga.
Najiuliza tu hapa kama hii ni ID ya muda mrefu ya yule kijana Lucas! Au la.
 
Samiah Hana ushawishi kabisa. Ndipo maana kaanza kampeni mapema kabla ya muda. Mara Samiah Queens mara chawa wa Samiah BLA BLA nyingi, wakati upinzani wapo kimya. Ila kwenye siasa wiki moja ni kubwa Sana.
 
SAMIA HANA USHAWISHI.

SAUTI YA HOTUBA ZAKE, INAJIELEZA.
Kwa kuwa Rais Samia sio muimbaji hivyo hashawishi watu Kwa sauti, ushawishi wake unapimwa na ubora na uzuri wa kazi na maamuzi yake na ya Serikali Kwa ujumla. Tutumie kigezo kumpima na sio hiko Cha Sauti
 
Usilolijua ni kama usiku wa kiza. Hakuna kikundi chochote kilichoanzishwa na Rais Samia bali vikundi hivyo wameanzisha watanzania wenye mapenzi mema ambao wanashawishika kuelezea kazi nzuri za Rais wetu.

Tofautisha kati ya kuanza kufanya kampeni mapema na kufanya siasa. Kuanza kampeni mapema ni kitendo ambacho kinafanyika kipindi ambacho kisheria, kikanuni na kikatiba mchakato wa kampeni umeanza na mtu inasemwa ameanza kampeni mapema ikiwa tu kabla ya mchakato Fulani kumaliza yeye kaanzisha mchakato mwingine.

Mfano, wakati wa uchaguzi mkuu kulingana na ratiba ya NEC Kuna kipindi cha kuchukua fomu ,kurejesha fomu ,kuteuliwa kugombea na kufanya kampeni. Ikitokea mtu kabla ya kuteuliwa kugombea akaanza kujinadi hapo ndipo tunasema kaanza kampeni mapema.

Ila Kwa Sasa ,Kwa sababu hakuna ratiba ya uchaguzi iliyotoka wala hatupo kipindi cha uchaguzi hapo tunasema anafanya siasa.
 
Back
Top Bottom