Jokate Mwegelo: Bila Rais Samia kuwa na falsafa ya 4R katika uongozi wake, kuna watu wasingekuwa na jeuri ya kuandamana

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
"TUENDELEE kumuunga mkono Mwenyekiti wetu wa CCM na Rais Dkt. Samia katika kuongoza nchi yetu, amekuwa mfano kwa kuwezesha wanawake kisiasa, kiuchumi na alipewa nchi katika kipindi kigumu lakini alionesha ujasiri na uwezo wa uongozi mkubwa na kupita kwenye mapito tukiwa wamoja na kupelekea kuwa salama."

"Bila Mama yetu Rais Samia kuwa na falsafa ya 4R basi kuna watu wasingekuwa hata na jeuri ya kuandamana huko barabarani wanaipata jeuri hiyo kutoakana na ustahimilivu wa Mama yetu, Rais Samia anajiamin ndio maana chokochoko zao na maneno yao hayamsumbui na jeuri inakuja sababu wanawake wote manamuunga mkono pamoja na Wanaume wote nchini"

"Tunaomba sana wanawake wote tuendelee kumuunga mkono Rais Samia, Viongozi wa Chama na UWT tuendelee kusema kazi njema ambayo Rais Samia anainfanya kwaajili ya watanzania,tusichoke kuwasikiliza, kuwaelemisha na kuwaonesha Wananchi kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu nasi UWT tunaendelea kuwasisitiza wanawake kumuunga mkono wakati wote.

Ndugu. Jokate Mwegelo
Katibu Mkuu wa UWT - Taifa

📍Lumumba - DSM
🗓️ 7 Machi, 2024

IMG-20240307-WA1366.jpg
Pia soma:
 
Ndio shida ya kuwa na society isiyojali merit.

Huyu utajiuliza amepitaje hadi kuwa kiongozi kama anashindwa tu kutambua .

Article 20 ya Universal declaration of human rights ya 1948.

Inajieleza vizuri tu :-
  1. Everyone has the right to freedom of peaceful assembly and association.
  2. No one may be compelled to belong to an association

Tanzania ilisaini na mikataba mingine ya kimataifa kuhusu haki za binadamu inaruhusu kuandamana /mikusanyiko.

Maandamano sio utashi wala upendeleo wa Samia wala mtangulizi wake aliyeyazuia huku misaada& mikopo akipokea kupitia mikataba mingine ya kimataifa.

Samia hawezi kutumia kigezo cha watu kuruhusiwa kufanya maandamano kama turufu ya umaarufu wa kisiasa.
 
Huwa nasema na narudia kusema, siku Tanzania itaanza kuendelea kwa kasi pale tu wengi wa Watanzania watapotokwa na ujinga akilini mwao...

Bahati mbaya sana, wanaotuongoza wamejaa ujinga mwingi zaidi...

Na wanaoongozwa wamekata tamaa kwa sababu hawana fikra mbadala sababu ya ujinga kiasi...
 
Kuna msemo unasema,PATA cheo/ fedha tujue tabia Yako au kosa pesa tujue kipaji chako.

Huyu dada ameibuliwa na JPM ambaye hakuwa na tabia ya kuheshimu katiba. Anasahau hiyohiyo katiba anayoidharau ndivyo imempa huyo mama yake urais pamoja na dharau zao.

Samia ni mwanadamu,japo imewahi kutokea naye akajisahau kuita katiba na kajikitabu, lakini naamini alikaa akatulia anajua yeye leo ni Rais kupitia hakohako kakitabu.

Hawa vijana ambao wamefuruku hayo madaraka wanajisahau sana na wanajipendekeza mpaka kumuaibisha Mwenyekiti wao, kwamba ule ujinga wa kupuuza katiba uliofanywa awamu ya tano yeye anaona ni sawa.

Wakati Mickail Gorbachev wa Urusi enzi 1991(sina hakika kama nimepatia jina) anakukusudia kuleta mageuzi urusi wakati huo ni Soviet union, alikutana na kizingiti kikubwa cha kikatiba, akafikiria kuandaa muswada wa kubadilisha katiba itakakayompa madaraka makubwa Rais ili imuwezeshe kufanya mageuzi aliyoyataka, nakumbuka aliyekuwa rafiki yake mkubwa ambaye wakati huo ni waziri wa nje, Edward Shervananzdze alimpinga,kwa kigezo kuwa ikitokea yeye akaondoka madarakani ataingia mtawala wa hovyo ambaye atatumia kigezo cha katiba hiyohiyo kuumiza watu, Gorbachev hakumsikiliza na huyu rafiki aliamua kujiudhuru ili asiwe sehemu ya historia iliyounda katiba ya kumpa madaraka mtu wa hovyo na watu wakateseka.

Samia ametambua huo ujinga wa kujipa umungu mtu kwa kisingizio cha katiba mbovu tuliyonayo,ila tatizo amezungukwa na wanafiki na wajinga wanaofikiri wanamsaidia kumbe wanamuingiza shimoni kwa maslahi yao. Huyu dada awali alionekana ni kiongozi wa kutumainiwa sana siku zijazo kumbe yeye, Sabaya na Bashite ni walewale.
 
"TUENDELEE kumuunga mkono Mwenyekiti wetu wa CCM na Rais Dkt. Samia katika kuongoza nchi yetu, amekuwa mfano kwa kuwezesha wanawake kisiasa, kiuchumi na alipewa nchi katika kipindi kigumu lakini alionesha ujasiri na uwezo wa uongozi mkubwa na kupita kwenye mapito tukiwa wamoja na kupelekea kuwa salama."

View attachment 2927493
Wajinga ndio wanatamba saa hizi 4R nayo ni falsafa ya kujivunia? Nchi imetekwa hadi karibu bandari ziende uarabuni halafu mjinga anamsifia huyu mwanamke eti 4R. Jpm ameacha nchi na nidhamu rushwa imepungua sana. Anakuja mtu anawaambia watumishi wa umma kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake ya malisho. Huu ni ujinga unatawala nchini sasa.
 
Ndio shida ya kuwa na society isiyojali merit.

Huyu utajiuliza amepitaje hadi kuwa kiongozi kama anashindwa tu kutambua .

Article 20 ya Universal declaration of human rights ya 1948.

Inajieleza vizuri tu :-
  1. Everyone has the right to freedom of peaceful assembly and association.
  2. No one may be compelled to belong to an association

Tanzania ilisaini na mikataba mingine ya kimataifa kuhusu haki za binadamu inaruhusu kuandamana /mikusanyiko.

Maandamano sio utashi wala upendeleo wa Samia wala mtangulizi wake aliyeyazuia huku misaada& mikopo akipokea kupitia mikataba mingine ya kimataifa.

Samia hawezi kutumia kigezo cha watu kuruhusiwa kufanya maandamano kama turufu ya umaarufu wa kisiasa.
Kipindi mnalalamika hiyo article haikuwepo?
 
"TUENDELEE kumuunga mkono Mwenyekiti wetu wa CCM na Rais Dkt. Samia katika kuongoza nchi yetu, amekuwa mfano kwa kuwezesha wanawake kisiasa, kiuchumi na alipewa nchi katika kipindi kigumu lakini alionesha ujasiri na uwezo wa uongozi mkubwa na kupita kwenye mapito tukiwa wamoja na kupelekea kuwa salama."
Mwendazake alikua halali kisa chadema , sasa uyu anaongea nini, maandamano yangefanyika tu maana yapo kikatiba , elewa watu wakishafika point of no return, Dunia sio salama tena unafanya ujinga unaishia ICC ,
 
Haki ya kuandamana ipo kikatiba, mpangaji mkuu wa pale magogoni hana haki ya kuzuia hili, Tanzania ina kila elements kuwa ni police state, uoga uliopandikizwa kwa watanzania wengi, akachanganywa na ujinga ndio mtaji mkubwa wa Lumumba street, push back haipo mbali na itakapoanza kutakua sio rahisi kusimamisha,ccm bila vyombo vya dola ni chama cha kawaida tu
 
"TUENDELEE kumuunga mkono Mwenyekiti wetu wa CCM na Rais Dkt. Samia katika kuongoza nchi yetu, amekuwa mfano kwa kuwezesha wanawake kisiasa, kiuchumi na alipewa nchi katika kipindi kigumu lakini alionesha ujasiri na uwezo wa
Naunga mkono hoja
 
"TUENDELEE kumuunga mkono Mwenyekiti wetu wa CCM na Rais Dkt. Samia katika kuongoza nchi yetu, amekuwa mfano kwa kuwezesha wanawake kisiasa, kiuchumi na alipewa nchi katika kipindi kigumu lakini alionesha ujasiri na uwezo wa uongozi mkubwa na kupita kwenye mapito tukiwa wamoja na kupelekea kuwa salama."
Ni ujasiri na Moyo mweupe wa Samia tuu ndio umewapa hao wasio na shukrani kurudi kuungana na familia zao na kuropoka kama wanavyofanya Sasa.

Bila Samia saizi wengine wangekuwa jela,kaburini au uhamishoni na Kila siku wangekuwa wanalalama huko Twitter.

Uungwana wa Samia analipwa matusi ila uzuri wa ccm ni kwamba inajua kucheza nao,subirieni moto baada ya Samia kutoka.
 
Nimemshangaa sana Katibu Mkuu wa Wanawake wa CCM Jokate kuamini Maandamano ni hisani ya Rais!

Jokate anamtofautisha Dikteta Magufuli kuwa alizuia maandamano na Rais Samia karuhusu maandamano kama ni watu wawili tofauti.

Jokate anashindwa kuelewa kuwa Magufuli alikuwa anavunja Katiba!

Napenda nimshauri Jokate asome Katiba ya nchi inasema nini kuhusu maandamano. Kwa kumsaidia tu Maandamano yapo Kisheria kwa mujibu wa Katiba, alichokuwa anakifanya Magufuli ni ukiukwaji wa Katiba na ndiyo maana kitendo hicho Mahakama ilisema Magufuli alivunja Katiba.

Suala la Rais Samia kuruhusu Maandamano ni suala la Kikatiba Rais Samia ametekeleza Takwa la Katiba tofauti na Magufuli. Wapinzani Kuandamana ni Takwa la Kikatiba sio la mtu ili mradi wanaotaka kuandamana wakidhi vigezo vilivyowekwa Kikatiba.

Ushauri kwa Jokate; jitahidi sana kuisoma Katiba kabla ya kutoa matamko yako.
 
Back
Top Bottom