Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,488
- 13,608
Kusifu serikali hakujaandikwa kwenye katiba ni maamuzi ya watu kwa mapenzi yao. JPM alikuwa na nidhamu ya kazi alikuwa na uwezo mkubwa wa kufuatilia masuala anayoanzisha.Hujui shirika la anga liko taabani hadi sasa! Nani muhusika na anayepaswa kuhojiwa na kulipa hasara ya billioni 60??
Kulikua kuna sababu gani chanya za kiuchumi kupeleka route ya ndege Chato?
Unaongelea habari za SGR je hufahamu ule ni mkopo wa $1.46 Billion ambao wewe pia utaulipa kwa kodi unazochangia kwenye kuuza au kununua huduma kadhaa?
Je Jiwe alitoa pesa yake mfukoni kufinance ujenzi wa Reli? Alikatwa hata asilimia 5% ya mshahara wake kusaidia ujenzi wa hii reli! ?
Hata angekuwepo Mzee Mwinyi ndio mtawala kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia nchi ilihitaji kuwa na reli ya mwendokasi na bado angetafuta vyanzo vya kusaidia ujenzi na ndio mikopo itakayolipwa na kodi za wananchi ila mwisho wa siku wananchi watafaidika na reli kupitia hizo kodi zao!
Sijawahi kusikia huku kwa wenzetu wanaisifu serikali mara imewajengea daraja mara sijui barabara! Ila kwa kua watanzania wengi bado wapo usingizini wanashindwa kujua zipi ni haki zao na zipi ni hisani.....
Link hii hapo kaone tulivyokopeshwa ila MATAGA mmegeuzwa praise team
Kuna suala la kipaji cha mtu cha kufanya kazi, hayati alikuwa nacho. Kuhamia Dodoma ni suala la tangu 1973 wamepita marais wakilishindwa.
Suala la ndege ni la kiuchumi zaidi wewe umeliongelea kimtaani zaidi. Hasara ilanza mwaka 2016 ikiwa ni bilioni 300 mwaka jana imefikia bilioni 55 kumbuka kuwa inakwenda inashuka na kama sio corona kuipiga dunia sasa hivi isingekuwepo kabisa.
Ni rahisi kumkejeli JPM lakini wapo wengi wanaoujua uwezo wake wa kung'ang'ana mpaka jambo likaweza kufanyika.