Rais Samia Afanya Mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC)

Hapa ndipo tunapoanza kuchukiana na kuwahisi mnatuibia
Heading inasema 373 bil
Content inasema 273 bil

Naweka record sawa msije mkatupiga changa la macho, hatutaki ujanjaujanja

Mwandish wa hii thredi ameshapiga b100 km masihara
 
Mkuu kweli wewe ni jingalao!! ipi ni kweli, 373 au 273?
Mkuu na ndiyo aina ya watendaji wengi tulionao serikalini hawakumbuki jana alipewa kiasi gani, ametumia kiasi gani, amebaki na kiasi gani, anachojua zipo na zimekwisha basi
 
Ingekuwa bora hako ka hela kangemalizia hiki kipande cha Dar-Moro ili watu angalau waanze kuonja matunda ya SGR kwa safari za Dar-Moro.
 
TRC ...are you guys organized? Majengo yenu ya ofisi ni kama mapagale. Hamfanyi hata painting?
Mbona kama ni maghala ya vyuma chakavu? Mtaweza kweli kuendesha SGR kwa ufanisi?
 
Ila mambo yakiharibika kulaumu ni wajibu!!!. hizi ndio mentality za kiafrika siku zote zinahalalisha malalamiko.
Kukosolewa ni sehemu ya uongozi pia kupongezwa ni sehemu ya uongozi

Je watu wanajua wapi pa kupongeza na wapi pa kukosoa??

Mfano huwezi kuipongeza serikali kwa kuleta maji mtaani kwenu sababu unalipa kodi na kodi hiyo inaangukia kwa serikali kuwasogezea huduma wananchi wake kama hayo maji!

Je serikali isipoleta maji mfanyeje jibu ni inakosolewa kwa kushindwa kufanya jukumu lake la msingi kwa kusogeza huduma muhimu ya maji kwa walipa kodi!

Bad enough washamba na mkuu wao waliwafanyia watu brainwashing na kupongeza pongeza hata vitu vya kijinga hivi mlifikiri serikali inajiongoza kwa pesa zake mfukoni?? Izitoe wapi kama sio kwa hao wananchi wanaoipongeza kwa kutimiza majukumu yake!
 
Napinga utamaduni wa kukosoa kupitiliza mpaka mtu anasahau kuweka mipaka ya ukosoaji. Hayati JPM alifanya sana kazi, alijituma vilivyo.

Aliweza kuwa watu nafasi kwa kuangalia uwezo kuliko kuongozwa na majungu, kama sio JPM leo hii sekta ya anga ingekuwa hoi, leo hii treni isingefika Moshi baada ya miaka 25.

Leo hii kitu kinachoitwa gawio la mashirika kwa hazina kisingekuwepo. SGR isingekuwa inajengwa.

Umechemka hapo mwishoni kujaribu kumponda JPM kama sehemu ya kumalizia hoja yako.
 
Hakika KAZI IENDELEE
Masanja Kadogosa amekiri kuwa wamepokea kiasi cha Tsh bilioni 273 ambazo zinaenda kujenga mradi wa reli SGR kutoka Mwanza hadi Isaka.
Ingekuwa awamu ya tano ungeandika Magufuli ametoa!

Shithole!
 
Angeweza kupeleka kwenye posho za wabunge huko
Hivi wabunge hawa tulio nao, ambao zaidi ya robotatu hawakuchaguliwa na wananchi, chini ya huyu spika kigeukigeu, ni asset au liability?

Unapokuwa na many redponsibiloties but limited resources, unatakiwa kupunguza au kuondokana na liabilitiesm
 
Napinga utamaduni wa kukosoa kupitiliza mpaka mtu anasahau kuweka mipaka ya ukosoaji. Hayati JPM alifanya sana kazi, alijituma vilivyo.

Aliweza kuwa watu nafasi kwa kuangalia uwezo kuliko kuongozwa na majungu, kama sio JPM leo hii sekta ya anga ingekuwa hoi, leo hii treni isingefika Moshi baada ya miaka 25.

Leo hii kitu kinachoitwa gawio la mashirika kwa hazina kisingekuwepo. SGR isingekuwa inajengwa.

Umechemka hapo mwishoni kujaribu kumponda JPM kama sehemu ya kumalizia hoja yako.
Hujui shirika la anga liko taabani hadi sasa! Nani muhusika na anayepaswa kuhojiwa na kulipa hasara ya billioni 60??

Kulikua kuna sababu gani chanya za kiuchumi kupeleka route ya ndege Chato?

Unaongelea habari za SGR je hufahamu ule ni mkopo wa $1.46 Billion ambao wewe pia utaulipa kwa kodi unazochangia kwenye kuuza au kununua huduma kadhaa?

Je Jiwe alitoa pesa yake mfukoni kufinance ujenzi wa Reli? Alikatwa hata asilimia 5% ya mshahara wake kusaidia ujenzi wa hii reli! ?

Hata angekuwepo Mzee Mwinyi ndio mtawala kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia nchi ilihitaji kuwa na reli ya mwendokasi na bado angetafuta vyanzo vya kusaidia ujenzi na ndio mikopo itakayolipwa na kodi za wananchi ila mwisho wa siku wananchi watafaidika na reli kupitia hizo kodi zao!

Sijawahi kusikia huku kwa wenzetu wanaisifu serikali mara imewajengea daraja mara sijui barabara! Ila kwa kua watanzania wengi bado wapo usingizini wanashindwa kujua zipi ni haki zao na zipi ni hisani.....

Link hii hapo kaone tulivyokopeshwa ila MATAGA mmegeuzwa praise team
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom