Rais Mwinyi wa Zanzibar naye atakuwa anamuachia Mama awe anaenda Safari zake kama Mama afanyavyo Kwake?

Ninapoanzisha ' Mada ' hapa Jamvini ( JamiiForums ) kisha nikiona ninaanza Kueleweka vyema na JF Intelligent Members ( kama Wewe hivi ) huwa nafurahi sana. Ulichokiandika ndiyo sahihi 100% na ' Mama ' awe makini mno na ' Utaratibu ' huu kwani utazalisha ( unazalisha ) Visununu na ataanza ' Kuhisiwa ' kuwa ana ' Uzanzibari ' mwingi kuliko ' Katiba ' ya JMT inavyotaka.
Na ndivyo ilivyo!
 
Nafkiri ieleweke kwanza Mh.Rais ana haki ya kumchagua yeyote kumuwakilisha katika ziara za nje, Dr Mwinyi ni Rais wa SMZ ila pia ni mjumbe wa baraza la mawaziri na katika masuala ya mambo ya nje ni yakimuungano so sio kosa yeye kwenda kama mwakilishi wa rais wa SMT ila tu znz haiwezi ikajiwakilisha yenyewe kwenye mambo ya nje.Pia yawezekana kwakuwa viongozi wakuu wa SMT kwa sasa Rais,VP na PM wapo busy na kuunda serikali yao ya awamu ya sita, pia waziri nje tunaona yupo busy kurejesha mahusiano ya kidiplomasia (tunaona ugeni mwingi) yawezekana ndio maana mh SSH anaona ni busara wawepo halafu kuwe na uwakilishi.
nawasilisha
Upo sahihi asilimia zote mkuu.

Akili fupi tu ndio zitashindwa kufkiria hili
 
na hiyo ndio maaana halisi ya Muungano wa nchi mbili.

lkn jambo zuri zaidi muungano wetu ni bora zaidi kuliko miungano yoyote duniani.
 
Mama 'anakulipa' nini 'Kumpigania' hivi?
Sisi Watanzania wenye mapenzi ya dhati na nchi hii tunajua Mama anatupeleka tuliko takiwa tuwe tumefika many years ago.

Sisi wapenda maendeleo tumedhamiria kumuunga mkono mama ili tufikie maendeleo ya kweli na sio maendeleo ya mitandaoni ya uchumi wa kati usio na tija.

Hatutaki kuangalia sijui ametokea wapi wala wapi tunachotaka ni kujua je kiongozi huyu atatuletea maendeleo au laa?? The sign kwa mama ni kwamba baada ya miaka 2 mbele nchi hii itatoka kwenye lindi la umaskini.

Nendeni mkamsikilize Dangote aliyoyasema juzi alipokuwa ikulu. Je Dangote pia ni Mzanzibar na analipwa na Mama.

By the way swali kwenu ni kwamba Mama amewakosea nini mpaka kumsema sema hivi??
 
Jadili Kihoja na siyo Kishabiki unatuboa.
Kwahiyo wewe huoni kwamba account zote zilizofungwa kionevu na TRA wakati wa mwendazake na sasa kuachiwa ili watu wafanye biashara na Watanzania wapate ajira sio hoja??

Tunasisitiza kwamba Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu
 
Kwahiyo wewe huoni kwamba account zote zilizofungwa kionevu na TRA wakati wa mwendazake na sasa kuachiwa ili watu wafanye biashara na Watanzania wapate ajira sio hoja??

Tunasisitiza kwamba Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu
Ni wapi GENTAMYCINE nimesema kuwa ninamchukia Rais wangu wa JMT Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan?

Tena kwa Taarifa huenda Mimi ndiyo nikawa nampenda zaidi kuliko Damn Fool Wewe kiasi kwamba nikiona anakengeuka kwa baadhi ya Mambo namkosoa ili asiharibu zaidi.

Baadhi ya Watanzania mmekuwa na ' Mentalities ' za ' Kipumbavu ' sana kwamba Mtu yoyote anayemsema Rais basi ni ama Mpinzani CHADEMA au ni Mdini au anatokea Kundi Hasimu kama linalotajwa sasa la SUKUMA GANG.

Kuna Member Mmoja hapa ameelezea vyema kabisa tena Kikatiba na Kidiplomasia kuhusu hili 'Suala Mjadala' nililolileta hapa na kusema kwa hili la Mama Kuwakilishawa na Rais Mwinyi wa Zanzibar kwa Mambo ya Kijamuhuri anakosea sana tu.

Na bahati nzuri sasa labda nikutaarifu tu Rais ( Mama ) Samia Suluhu Hassan ni " Follower ' wangu mkubwa tu hapa JamiiForums na 24/7 haachi kunisoma GENTAMYCINE na hili kwa Kujiamini kabisa nina uhakika nalo kwa 100%.

Kuna ' Threads ' kadhaa za Kumsifu na hadi Kumletea Rais ( Mama ) Samia Suluhu Hassan na moja ni ya Juzi tu mbona sikuona unasema kuwa namchukia na katika Uzi huo huo Wewe umeuchangia zaidi huku ukinipa ' Likes ' zako za kutosha tu?

GENTAMYCINE sipo hapa JamiiForums kuwa Mnafiki au Kujipendekeza ila nipo ' very Neutral ' katika ' thorough analysis ' zangu na nimekuzwa katika Misingi ya Kusimamia Ukweli na kuzingatia Utaratibu, Sheria na Kanuni zilizopo.

Mimi ni mwana CCM sana tu ila wakikosea ' nawakaanga ' vizuri tu. Mimi ni mwana Simba SC nao pia ' wakilikoroga ' tu ' ninawasiliba ' vizuri tu. CHADEMA wakipatia nawasifu na Klabu ya Yanga ikifanya Jambo jema nawapongeza.

Mimi ndiyo GENTAMYCINE Mkuu sawa?
 
Mtaongea katiba na sheria ila kiukweli hii nchi inaongozwa kadri rais atavyotaka.

Naona wazenji wameshika usukani..
Haya uliyoandika ndio mawazo waliyokuwa nayo baadhi ya watu kipindi cha hayati JPM.

Maana ya umoja wa kitaifa ni kutanguliza kwanza kule kuwa wamoja katika shida na raha.

Akitoka Mama ikulu ataingia Rais wa kabila jingine atakayekuwa na “watu” wake na wao watafurahia maisha.

Ndio siasa zetu zilivyo, tumshukuru Mungu utaifa wetu unadumu kwa sisi wenyewe kuwa na sifa ya kuvumiliana.
 
Huyu mother Theresa aambiwe ukweli aache ujanja wake wa kuipa fursa zenji, kwenye mambo ya msingi ya JMT.
Haya mambo haya,kila kitu nchi Ni kama Jana,sera za BOT na mabenki ziko hovyo system inachelewa kuchukua hatua,Benki mifumo imeshikiliwa, na wakubwa wapo tuu,hivi kuna laana inatutafuna?
 
Back
Top Bottom