Rais Mwinyi wa Zanzibar naye atakuwa anamuachia Mama awe anaenda Safari zake kama Mama afanyavyo Kwake?

Mtaalamu, inawezekana umeupenda huo utaratibu ila ukasahau muundo wa serikali ya JMT.

Hussein Mwinyi ni nani katika serikali ya JMT?

WaZNZ wameshaona fursa ya kushika hatamu, SMZ haina kiti popote isipokuwa EAC, raisi wa SMZ hawezi kumuwakilisha raisi wa JMT.

Anamuwakilisha kwenye yale mambo 22 ya Muungano?

Raisi wa SMZ hawezi kuendesha Baraza la mawaziri mbele ya VP kama raisi wa JMT hayupo, iweje awakilishwe na naye nje? Protokali hapa imekaaje?

Nafasi ya raisi wa SMZ kuwa VP kwenye JMT ilishaondolewa kwa kuzingatia mkanganyiko wake, viongozi wakubwa 3 wa JMT wanapaswa kuwa juu ya raisi wa SMZ, sasa inawezekana vipi? Msaidizi wa raisi wa JMT ni VP, kwanini amtume raisi wa SMZ?

Kazi iendelee.
Bado! tutulie tusiwe na haraka kazi inaendelea!
Rais anaweza kuwakilishwa na yeyote hata mimi au wewe!
 
Bashite kama mkuu wa mkoa alimwakilisha wapi raisi wa JMT nje ya mipaka ya nchi ya Tanzania? Kama kwenye mkoa aliokabidhiwa sawa, napo mamlaka yake yana mipaka, wanasema bila kuathiri vifungu vingine vya sheria mama.

Wajuvi wa sheria ya katiba wa wanaweza kuweka neno sahihi hapo, kama imevunjwa au imetamatishwa. Ila kwa maono yangu, sioni mwanga ukiingia kwenye karavati(tunnel) nililopo, hivyo bado ni giza mno, ngoja niendelee kukaza mwendo, pengine mbele huko nitaanza kuona mwangaza na kupata tumaini la kutoka kwenye hili tunnel na kujua huko nje kukoje ili nichague mwelekeo utakaonipendeza.

Wanafunzi wanapiga kelele darasani, monitor wa darasa hajulikani, mwalimu aliwaambia wanafunzi yeye hawezi kutumia fimbo wala ukali wa sauti, wanafunzi ni waelewa, hivyo akiwaambia wataelewa na wamuelewe hivyo.

Andika majina ya wapiga kelele darasani, waliofeli ni viboko, watoro waadhibiwe, mimba za utotoni fukuza mwanafunzi na weka jela mtia mimba, usafi wa mwanafunzi ukikaguliwa kila alhamisi, mchaka mchaka kila asubuhi kujiweka fiti kwa masomo ya siku nzima, wimbo wa taifa kuimbwa kila siku tukiwa mstarini kuongeza hamasa na ile sense of ownership, uzalendo.....n.k

Nimekumbuka enzi za shule ya msingi Nanjilinji.

Kazi iendelee
Hivi nanjilinji siku hizi kunafikika bila tabu ?
 
Na ukiona nimeanzisha Uzi jua kuna ' nilichokibaini ' na nakiona ama hakija kaa sawa au kina ' Ulakini ' hivyo ' nawachokozeni ' tu Great Thinkers ninaowapendeni ( JF Members ) ili tujadili na kwa marefu na mapana yake. Ubunifu huu ' Mama ' nahisi utaanza ( au umeshaanza ) kuzaa ' Visununu ' kwa upande wa Tanzania Bara na najua akina Mpango ( VP ) na Majaliwa ( PM ) linawauma mno ila ' wanajikausha ' tu.
VP na PM wamekabidhiwa mikasi ya kuzungukia mikoani na kukata utepe,
 
Huyu Mama tumuache,sababu shida Ni CCM na sio Kiongozi,kama tukimpigia kelele anaonyeaha uso wa kuumiza mchana kweupe,kazi ya kupambana nae tuwaache Lumumba,kila mtu ajue tumekaa miaka saba bila increament,In fact,nchi Haina dira.kila mja anakuja na kudemka kivyake.
Huu ndiyo Ukweli tena 100% tu Mkuu.huyu
 
Back
Top Bottom