Rais Dkt. Mwinyi arejea Zanzibar

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
478
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amerejea Zanzibar baada ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la Doha (Doha Forum) ambalo alishiriki ufunguzi wake pamoja na mdahalo wa majadiliano kuhusu kujenga uchumi wa kidijitali.

Baada ya kumalizika Jukwaa hilo alielekea Nairobi, Kenya katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Kenya (Jamhuri Day) zilizofanyika uwanja wa Uhuru Gardens ambapo pia alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sherehe hizo.

Rais Dk. Mwinyi amepokewa na Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Hemed Suleiman Abdulllah pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, Wazee wa Chama na Vyombo vya ulinzi na usalama.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani leo tarehe: 13 Desemba, 2023.

IMG-20231213-WA0037.jpg
 
View attachment 2841351
Kwa nini amepokelewa na Makamu wa Pili wa Rais wakati Makamu wa Kwanza wa Rais yupo??? Au Mimi sielewi vizuri Muundo wa Uongozi wa Serikali ya Zanzibar?
 
alienda kumwakilisha rais wa JMT? duh ina maana hapa TZ makamu wa rais anatumwa kufanya kazi ya kificho mwezi mzima halafu mtu ambaye hana mamlaka yoyote ndani ya muungano anatumwa kumwakilisha rais wa muungano? WTF
 
Ndio maana hawataki kabisa kusikia kitu kinachoitwa Katiba Mpya.
 
Back
Top Bottom