Rais Museveni amteua mwanae Muhoozi Kainerugaba kuwa CDF

Saaafi sana hii kitu, maana Waafrica bado hawajapata akili na hata wakiwa nayo, hawana uwezo wa kutofautisha kitu kizuri na kibaya

Na wakiweza kutofautisha, bado hawawezi kuchukua hatua! Mlitaka M7 afanye nini katikati ya jamii isiyojitambua na isiyoweza kuchukua hatua?
 
Hapana,Inatagemea tu nchi na nchi. Kuna nchi unaweza kuteua hata ukoo wako mzima madarakani ukakuzunguka na mkarithishana hayo madaraka, kuna nchi mifumo yake haitakuwezesha kufanya hivyo.
Sio mifumo ishu ni kwamba Africa tunaishi kwa kuangalia mapungufu zaid kuliko faida so hatutakaa tupate maendeleo maana kila binadamu ana mapungufu.
 
Hongera yake.Lakini kijana mtata.Maana huwa anatishia hata kumpindua Baba yake.Ni kama vile yuko karibu zaidi ya mama yake kwa namna anavyotoaga mkwala dhidi ya baba yake.
 
Huwa najiuliza kwanini Rais usiachie madaraka muda wako unapopita then uendelee kula bata kama maraisi wetu hapa bongo,hawaoni mifano wakina JK wanavyofurahia maisha yao,mtu yuko huru anajichanganya mpk na watu wa kawaida hana hofu hata kidogo...
Inategemea namna na kiwango ulichokwapua na kuumiza watu ukiwa mamlakani na pia uhakika wa kulindwa na mwingine atakayekurithi.
 
Rais Yoweri Museveni amemteua mtoto wake General Muhozi Kainerugaba kuwa Mkuu wa Jeshi la Uganda

Halafu kuna Watu hapa Tanzania utawasikia wanadai Freeman Mbowe anapendelewa na mh Edwin Mtei

Jumaa Mubarak 😄🔥
Wanaolalamika Mtei kumpendelea Mbowe watakuwa hawana akili, maana chama ni cha kwake na nyumbu wote ni wa kwake. Yeye ndo aliemkabidhi Mbowe hao nyumbu ili aendelee kuwatumia mitandaoni kwa ajili ya masilahi yake ya kisiasa.
 
Sio mifumo ishu ni kwamba Africa tunaishi kwa kuangalia mapungufu zaid kuliko faida so hatutakaa tupate maendeleo maana kila binadamu ana mapungufu.
Faida ya kuwaweka ndugu na watoto zako katika nafasi nyeti za mamlaka ni zipi?
 
Huwa najiuliza kwanini Rais usiachie madaraka muda wako unapopita then uendelee kula bata kama maraisi wetu hapa bongo,hawaoni mifano wakina JK wanavyofurahia maisha yao,mtu yuko huru anajichanganya mpk na watu wa kawaida hana hofu hata kidogo...
Sio kazi rahisi, hata hapa Bongo ni katiba imewabana. Embu atokee mbunge apendekeze mihula minne. Rais atakubali na atampa uwaziri kipindi chake chote
 
Jen. Muhoozi Kainerugaba

AFPCopyright: AFP
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amemteua mtoto wake, Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF).Gazeti la Daily Monitor la Uganda limeripoti.

Anachukua nafasi ya Jenerali Wilson Mbasu Mbadi ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa biashara katika mabadiliko mapya ya safu ya Baraza la mawaziri lililotangazwa karibuni.

Jenerali Muhoozi alikuwa akihudumu nafasi ya mshauri mkuu wa Rais katika masuala ya operesheni maalumu.

Source;BBC
 
Back
Top Bottom