Safari ya Jenerali Muhoozi Kainerugaba hadi kuwa CDF wa Uganda, tuna cha kujifunza kuhusu watoto wa Marais

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
431
626
Hii ndio Safari aliyoipita Jenerali MUHOOZI KAINERUGABA Mtoto wa Rais wa Uganda Yowery Kaguta Museven hadi kuwa Mkuu wa Majeshi wa Nchi Hiyo

2000: Aliteuliwa kuwa Luteni wa pili, Kitengo cha Ulinzi wa Rais (PPU)

2001: Alipandishwa cheo kuwa Kapteni

2003: Alipandishwa cheo kuwa Meja na urekebishaji wa PPU katika Kikosi cha walinzi wa Rais (PGB)

2008: Alipandishwa cheo kuwa Luteni-Kanali na kuteuliwa kuwa Kamanda wa Vikosi Maalum katika UPDF

2010: Aliteuliwa kuwa kamanda wa Kwanza wa Kikundi Cha Vikosi Maalum (SFG)

2011: Alipandishwa cheo na kuwa Kanali

2012: Alipandishwa cheo na kuwa Brigedia Jenerali

2016: Alipandishwa cheo na kuwa Meja Jenerali

2017: Ateuliwa kuwa Mshauri Mkuu wa Rais wa Majukumu maalumu

2020: Aliteuliwa kuwa Kamanda wa vikosi maalumu

2023: Alipandishwa cheo na kuwa jenerali

2024 Machi: Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Uganda

NB: Rais Museven ALIWAHI kusema kuwa Ikulu aliipata kupitia mapambano ya msituni hivyo basi kama kuna mtu anayeona anakosea basi naye aende msituni.
 
Museveni ana mipango ya muda mrefu hapo ujue anajiwekea ulinzi ko dogo huko PSU aliweka watu wake yaani kote alikopita huko jeshini plan ya miaka 26 museveni ni mjanja sana
 
Hii ndio Safari aliyoipita Jenerali MUHOOZI KAINERUGABA Mtoto wa Rais wa Uganda Yowery Kaguta Museven hadi kuwa Mkuu wa Majeshi wa Nchi Hiyo

2000: Aliteuliwa kuwa Luteni wa pili, Kitengo cha Ulinzi wa Rais (PPU)
2001: Alipandishwa cheo kuwa Kapteni
2003: Alipandishwa cheo kuwa Meja na urekebishaji wa PPU katika Kikosi cha walinzi wa Rais (PGB)
2008: Alipandishwa cheo kuwa Luteni-Kanali na kuteuliwa kuwa Kamanda wa Vikosi Maalum katika UPDF
2010: Aliteuliwa kuwa kamanda wa Kwanza wa Kikundi Cha Vikosi Maalum (SFG)
2011: Alipandishwa cheo na kuwa Kanali
2012: Alipandishwa cheo na kuwa Brigedia Jenerali
2016: Alipandishwa cheo na kuwa Meja Jenerali
2017: Ateuliwa kuwa Mshauri Mkuu wa Rais wa Majukumu maalumu
2020: Aliteuliwa kuwa Kamanda wa vikosi maalumu
2023: Alipandishwa cheo na kuwa jenerali
Machi
2024: Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Uganda

NB: Rais Museven ALIEWAHI kusema kuwa Ikulu aliipata kupitia mapambano ya msituni Hivyo Basi Kama Kuna mtu anaye ona Yowery Museven anakosea Basi naye aende msituni
Funzo:
Viongozi wengi wanatamaa, wakishika nafasi
wanataka uzao wao uendelee kutawala.

Yanayofanyika kwa wenzetu na kwetu yapo:

1. Viongozi kuwa na ubinafsi, kuwahadaa wananchi kuwa bila wao nchi haiwezi kuendelea kwa amani, kiuchumi, kijamii na kiutawala.

2. Viongozi kutumia mifumo ya kiusalama kuendelea kukandamiza wananchi na viongozi wenye fikra tofauti.

3. Viongozi kuendelea kuona wananchi hawawezi kujitawala bila wao, na hivyo kuzuia kila aina ya viongozi wanaokubalika na wananchi wasitawale kwa kuiba kura, kuzuia katiba yenye usawa na inayoweka vipengele visivyopendelea upande wowote.

4.Watawala waliopo madarakani kuifanya nchi kama mali yao binafsi, kuwaweka watoto kwenye nafasi za madaraka ya kiasa kwa upendeleo wa kujuana, ili waendelee kuwa karibu na keki ya taifa.
 
Kuna funzo gani hapo hapo amewekwa kimaslahi na kulinda madaraka yao akistafu au akifa mseveni mwanaye anakalia kitu, we unadhani mseveni hamwogopi bob wine?

NB mwanaye anawenge sana ya madaraka mzee anaweza pinduliwa au wakatengeneza mapinduzi ya mchongo mwanae awe rais na atakuwa katili kuliko mseveni, huko Rwanda kagame nae anaanda mwanae afrika ni hovyo sana maslahi ya wananchi kidogo wao ndio makubwa.
 
Rais Museven ALIEWAHI kusema kuwa Ikulu aliipata kupitia mapambano ya msituni Hivyo Basi Kama Kuna mtu anaye ona Yowery Museven anakosea Basi naye aende msituni
emoji4.png
Funzo kubwa hapa, Uganda itaendelea kumwaga damu ili kustawisha haki za kuchagua na kuchaguliwa kwa raia wa nchi hiyo.
 
Viongozi wa Afrika ni lazima uwazuie kwa nguvu ili wasigeuze uongozi wa nchi kuwa biashara ya familia.

Mimi nitasema wazi, kuna tofauti kubwa kati ya familia ya mwalimu nyerere, Ben Mkapa na JPM ukilinganisha na familia ya Mwinyi, Kikwete na huyu wa sasa linapokuja suala zima la kutaka kurithisha watoto wao uongozi wa nchi.

JPM alijaribu kuvunjavunja hii kitu kwa kuwapa kipaumbele wasomi wanaostahili, lakini wakamuwahi kabla hajamaliza kazi ya kujenga CCM mpya.

Hili kundi la pili hawana aibu. Ni lazima mifumo iweke utaratibu wa kuwapunguza speed, Uongozi wa nchi sio biashara ya familia.
 
Yuko wapi mugabe,huyo M7 siku akikats moto tujiandae kupokea wakimbizi
 
Watu wapambane halafu we unakuja unapiga domo eti demokrasia!! Hao US wenyewe nchi yao haiendeshwi na Rais mpiga domo.
 
Kuna funzo gani hapo hapo amewekwa kimaslahi na kulinda madaraka yao akistafu au akifa mseveni mwanaye anakalia kitu, we unadhani mseveni hamwogopi bob wine?

NB mwanaye anawenge sana ya madaraka mzee anaweza pinduliwa au wakatengeneza mapinduzi ya mchongo mwanae awe rais na atakuwa katili kuliko mseveni, huko Rwanda kagame nae anaanda mwanae afrika ni hovyo sana maslahi ya wananchi kidogo wao ndio makubwa.
Uliwaza kama mm, watatengeneza mapinduzi fake
 
Museveni ana mipango ya muda mrefu hapo ujue anajiwekea ulinzi ko dogo huko PSU aliweka watu wake yaani kote alikopita huko jeshini plan ya miaka 26 museveni ni mjanja sana
Kumbe Uganda nao Kikosi chao cha Kumlinda Rais kinaitwa PSU kama cha Tanzania? Dunia hii ina mambo kweli kweli.
 
Museveni ana mipango ya muda mrefu hapo ujue anajiwekea ulinzi ko dogo huko PSU aliweka watu wake yaani kote alikopita huko jeshini plan ya miaka 26 museveni ni mjanja sana
Kwenye kufa hakuna ujanja...his days are numbered
 
Unapompangia Mtu kuwahi Kufa Wewe ulishangea na Mwenyezi Mungu na Kukuhakikishia kuwa Utaishi Milele? Very Idiot.
Wewe ndiyo idiot

Kuna sehemu nimeandika mimi sitokufa!?
Huyo mseven afanye yote anayoyafanya ili kifo kipo mlangoni kwake na ataiacha uganda hata kama hataki
 
Wewe ndiyo idiot

Kuna sehemu nimeandika mimi sitokufa!?
Huyo mseven afanye yote anayoyafanya ili kifo kipo mlangoni kwake na ataiacha uganda hata kama hataki
Ulkitangulia Kufa Wewe Pumbavu Mmoja na Yeye akabaki utasemaje? Huwazi Maendeleo yako unawaza Mtu Kufa. Hovyo.....!!!
 
Hakuna kazi ngumu kama kuwa rais, kazi ngumu kama kukaa ikulu..... Alisikika kota pin mmoja nchi fulani
 
Back
Top Bottom