Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,129
- 35,153
Yaani kiongozi wa nchi anaumwa muda mrefu, ugonjwa endelevu, anapotelea hospitalini majuma kadhaa, anapambania maisha yake kufa na kupona, hajiwezi. Lakini katika mazingira hayo hayo, taifa zima halijulishwi chochote, makamu wake hajui, aelezwi na anafichwa kimakusudi asijue chochote. Hatimaye Rais anafariki dunia, bado makamu wake hajui chochote, watu wengine wanakaa chini kujadili namna ya kuendesha mambo ya msiba bila makamu wa rais kujua chochote.
Tuseme ukweli, kuna nchi inaongozwa na kikundi cha watu wasiojulikana na kinyume cha katiba kwa 100%. Kuna kila dalili huenda mambo yakawa magumu zaidi huko mbeleni.
Tuseme ukweli, kuna nchi inaongozwa na kikundi cha watu wasiojulikana na kinyume cha katiba kwa 100%. Kuna kila dalili huenda mambo yakawa magumu zaidi huko mbeleni.