Rais Magufuli, tukalime wapi? Tupeni mashamba tukalime

Rais Magufuli, tukalime wapi? Tupeni mashamba tukalime

Kilimo cha biashara au domestic purpose,kamaanisha kipi ni kipi
 
Eti Watu Wameacha Mashamba Vijijini Na Kukimbilia Kujazana Mijini!! Hivi Hayo Mashamba Mnayoyajua Ninyi Ni Yapi!!?? Ardhi Zenyewe Zimechoka Tokea Mababu Na Mabibi Wanalima Humo Humo Tu, Wazazi Wetu Nao Wakaingia Humo Humo!! Kilimo Chenyewe Cha Jembe La Mkono, Nguvu Kubwa Mafanikio Kiduchu!! Haya Hivi Sasa Kuna Janga La UKAME Kila Kona Ya TANZANIA, Mabadiliko Ya Tabia Nchi, Yamepelekea Uhaba Wa Mvua, Kiasi Cha Vyanzo Vingi Vya Maji Kukauka!! SASA Hao Vijana Ambao Mnaosema Wamekimbilia Mijini Kuuza Maji, Mlitaka Wafe Kwa Njaa Huko Vijijini!!!!!?? Hebu Mtuambie Leo Hii Ni Mikoa, Wilaya, Kata Na Vijiji Vingapi Wameshaomba Msaada Wa Chakula Toka Serikali Kuu, Kitengo Cha Maafa!!! Nendeni Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Pwani, Lindi, Moro, Mtwara N.k. Mjionee Jinsi Ukame Unavyowatesa Wananchi!!!! Wamejitahidi Kulima, Lkn Mvua Hakuna, Wengine Wameuziwa Mbolea Kanjanja!! TUSIDANGANYANE Humu, Kilimo Ni Shughuli Yenye Kuhitaji MITAJI, Uwe Ardhi, Pembejeo Za Uhakika Na Za Kutosha, Kulima Kwa Umwagiliaji Na Uwe Na Vyanzo Vya Maji Vya Uhakika!! Dunia Ya Sasa Si Ya Kulima Kwa Kutegemea Mvua Na Pasipo Na Pembejeo!! Hao Vietnam Ambao Walikuwa Makabwela Wa Kutupa Miaka 70, Hadi Walipoanza Kutafuta Mbegu Za Mikorosho, Kahawa Na Samaki Sato Hapa Tanzania, Na Leo Hii Wamepiga Hatua Kubwa Ktk Sekta Hiyo, Wanalima Kwa Kutegemea Mvua Na Kilimo Cha Jembe La Mkono!!!!!!!??? Serikali Bado Haiko Serious Na Kilimo, Wanachosema Kingine Na Wanachofanya Kingine!! Matokeo Yake Wanataka Kuleta Ubabe Badala Ya Mipango Mkakati, Ili Kuwezesha Wananchi Wake Kushiriki Ktk Kilimo!!!
 
Mashamba ya Mkonge mmemuuzia Dewji harafu mnataka tukalime Wapi??! #TunyoosheMTIsiyoKIVULI
 
Nilivomuelewa jpm sio vijana wakalime tu. Kuna kazi nyingi mno za kufanya mfano kutengeneza tofari, saidia fundi yani kazi nyingi mno sio kijana toka asubuh anashinda kwenye pool table had usiku na baada ya hapo anasuburi kubet bpl. Sioni kama jpm kakurupuka ila sema nyinyi wenye mawazo pinzani kila wakati ndo huwa mnakurupuka.tumechoka na ngonjera zenu kila mara ni kupinga tu kha mnaboa sana nyinyi wazungusha mikono.
 
Magufuli tupatie mashamba tukalime baba, jana umeagiza tukamatwe, tupelekwe kambini tulime kwa lazima.

Hakuna haja ya kukamatwa baba, tupatie tu mashamba tutalima wenyewe, kule vijijini kila pori tunalogusa tunaambiwa la mwekezaji, kila shamba tunaloliona tunaambiwa la mheshimiwa fulani.

Hakuna mashamba ya wazi baba, hata serikali imegawa mashamba yake kwa wadosi.Tukienda kwa nguvu tunaitwa wa wavamizi baba.

Tunavamia katika nchi yetu.Tukienda kuvua samaki tunaitwa wavuvi haramu baba'Tusaidie pia na vitendea kazi, hata majembe ya ngwamba tu baba. Mbolea Na umwagiliaji tutamwachia tu Mungu ataleta neema zake baba.

Tukienda kukopa tunaambiwa tuweke dhamana ya nyumba ama kiwanja baba, tutatoa wapi hizo dhamana sisi wacheza Pool table baba?.

Waangalie na TIB na Benki ya Kilimo baba kama mikopo yao inawafaa vijana . unaowakurupusha leo!Benki zako zinawafaa zaidi wazee kukopa kuliko sisi vijana baba.

Uwakumbushe na wale vijana wa CCM baba, hawataki kulima, hataki kazi,hawataki biashara, kutwa kucha kukusifia wanasubiri uteuzi baba.

Wengine wakilala wanauota U DC, wengine wamebadilisha mpaka miondoko baba kusubiri uteuzi wako baba, wameshakosa U RC bado U DC baba.

Tafadhali sana baba usitufukuze tu bila kujua tutakapoelekea.
Watu hawalazimishwi kufanya kazi bali mazingira yanawalazimisha, tengeneza mazingira hata baba zetu walilima mpaka wakafia shambani hawakupa hata theluth moja ya mafanikio tuliyonayo sasa hivi, kwani mazao yanaozea shambani, bei ndogo na miundombinu mibovu,weka sheria nzuri za biashara, umeme wa uhakika na viwanda hio tu inatosha kuwaweka vijana busy siku 366, na hata sehemu za starehe utawaona weekend tu. haya ni matunda ya kuwa na viongozi wasiojua kuongoza bali kufoka na hawawezi kutumia akili zao kutatua matatizo bali kutengeneza matatizo
 
Ndiyo ninalima

Nilipohitimu chuo niliamua kurudi mashambani kujiajiri kwa kilimo na ufugaji
Soko liko wapi? mbaya zaidi no serikali inapowachanganisha wafungaji na wa kulima umejilimia viheka vyako 50 vinalishwa ngombe, kilimo chenyewe chabkutegemea mvua ikigoma tu msimu mmoja kwisha Habari yako..au unalimaga kwa matumizibya nyumbani tu...tuwekee hapa kama unafanya kilimo cha biashara utuambie hizo changamoto unakabiliananazo vipi...
 
Mbona Vijana wa siku hizi mnaishiwa maarifa!!! Mashamba yako mengi sana na kuna Vijana ambao hawakupewa hayo mashamba na Mh. Rais wala Seeikali wamejikita huko na kufanya shughuli za Kilimo. Tatizo kubwa la Vijana wa zama hizi ni Uvivu uliotukuka na kulalamika kila kukicha. Wewe unaona ni busara kuamka asubuhi na kukimbilia kwenye Pool ukiwa hujanawa hata uso!!?? Hiyo hela unayocheza kamali na kunywa Viroba inatosha sana kununua tenga moja la nyanya na kusambaza majumbani au kwenye majiko ya bar na migahawa.
Mkuu niagizie mahali kwenye shamba zur au niombee kabisa nije nilime bure
 
Ukitaka kulima bure nenda JKT makutupora au JKT Ruvu mkuu. Kwa maelezo zaidi unaweza kufika pale JKT makao makuu.
Tanzania Ina vijana wangapi ambao hawana ajira ? Kwa hiyo hayo mashamba yatawatosha vijana wote na kama mashamba yapo tangazeni mtulipie nauli tuje.
 
Milioni 800+ zimeshaidhinishwa kwa zoezi hilo na muda si mrefu utapata taarifa kwenye vyombo vya habari.
Bro, acha uhuni yaani million 800 kwa vijiji vyote nchini au jimbo moja...
 
Mimi nimechoka kulima nimekuwa nikilima mahindi, Maharagwe na mpunga hakuna mafanikio Magufuli natakabkuanza kuchoma mkaa naomba vipolisi vyako visinikamate....
 
Bro, acha uhuni yaani million 800 kwa vijiji vyote nchini au jimbo moja...
Hizo pesa zinatoka kwa awamu ili kudhibiti na kusimamia matumizi bora. Hiyo milioni 800 ni fungu la kwanza ambalo liko tayari na muda wowote litafikishwa sehemu husika.
 
Back
Top Bottom