Mchange
Senior Member
- Jul 21, 2009
- 158
- 325
Magufuli tupatie mashamba tukalime baba, jana umeagiza tukamatwe, tupelekwe kambini tulime kwa lazima.
Hakuna haja ya kukamatwa baba, tupatie tu mashamba tutalima wenyewe, kule vijijini kila pori tunalogusa tunaambiwa la mwekezaji, kila shamba tunaloliona tunaambiwa la mheshimiwa fulani.
Hakuna mashamba ya wazi baba, hata serikali imegawa mashamba yake kwa wadosi.Tukienda kwa nguvu tunaitwa wa wavamizi baba.
Tunavamia katika nchi yetu.Tukienda kuvua samaki tunaitwa wavuvi haramu baba'Tusaidie pia na vitendea kazi, hata majembe ya ngwamba tu baba. Mbolea Na umwagiliaji tutamwachia tu Mungu ataleta neema zake baba.
Tukienda kukopa tunaambiwa tuweke dhamana ya nyumba ama kiwanja baba, tutatoa wapi hizo dhamana sisi wacheza Pool table baba?.
Waangalie na TIB na Benki ya Kilimo baba kama mikopo yao inawafaa vijana . unaowakurupusha leo!Benki zako zinawafaa zaidi wazee kukopa kuliko sisi vijana baba.
Uwakumbushe na wale vijana wa CCM baba, hawataki kulima, hataki kazi,hawataki biashara, kutwa kucha kukusifia wanasubiri uteuzi baba.
Wengine wakilala wanauota U DC, wengine wamebadilisha mpaka miondoko baba kusubiri uteuzi wako baba, wameshakosa U RC bado U DC baba.
Tafadhali sana baba usitufukuze tu bila kujua tutakapoelekea.