Habari wana JF;
Ninaomba kuja hapa na mawazo yangu tu binafsi, kuhusu matamko ya viongozi wetu wakuu. Rais anapotamka neno, nachukulia kuwa ile ni amri na haina mjadala ni kutekelezwa tu maswali baadaye.
Mheshimiwa Rais wetu alitamka kwamba vijana wasikae bure bila kazi. Ni neno zuri tena la kuungwa mkono. Ila; natamani kuuliza, Hivi Rais wetu hana washauri?? Rais, anaposema neno la maana namna hiyo, hakuna wenye kulifuatilia ili waliwezeshe?
Kilimo chetu Tanzania, kimekuwa cha kubangaiza tu. Mapori yamejaa tele, mito inayotiririsha maji 24/7/52 yaani isiyokauka kabisa.
Wizara ya Kilimo imekuwepo tangu uhuru 1961 hadi leo. Wizara ya Maji imekuweko tangu uhuru. Leo, Tanzania tunathubutu kusema ati vijana wakamatwe, washonewe sare, wapelekwe kwenye makambi ya kilimo?? Yaani kilimo ni adhabu??
Kweli nimekubali ni adhabu kwa sababu; Hatuna maofisa Mipango Tanzania!!! Hatuna hao maofisa mipango bali ni maofisa watabiri tuuu. Hakuna hata mmoja mbunifu. Kwa nadharia hawajambo.
wamesoma mpaka vyuo na vidato wamemaliza. Lakini, Ubunifu hakuna.
Kilimo bila umwagiliaji, kimepitwa na wakati. Mbaazi ikikosa maua husingizia jua. Jua lipo ili wewe mbaazi uzae. Msijitetee na Badiliko la tabia nchi. Badilikeni ninyi. Bunini miradi ya maji ya umwagiliaji, bunini miundo mbinu mizuri ya maji, Barabara za kuingia huko maporini karibu na mito, wekeni masoko tiyari. Haya, muungeni mkono mheshimiwa rais, kuwakamata hao vijana wakalime.
Tafadhali, msikitukanishe kilimo kuwa ni adhabu. Ni adhabu kwa sababu wanaenda kulima vumbi na kukaanga mbegu.