Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 875
- 960
KWA HILI LA VIJANA KULIMA, KUWA WAJASIRIAMALI, RAIS MAGUFULI AUNGWE MKONO
Ndugu zangu watanzania na wapenda mabadiliko wote. Kwanza napenda kutoa pongezi zangu kwa uteuzi alioufanya mh. Rais wa wakuu wa mikoa nchini. Mh. Rais ameonesha kujali na kuthamini sana vijana kwa kuteua vijana wenzetu kama Mh. Antony Mtaka, mh. Paul Makonda na mh. Martine Shigela kushika madaraka makubwa ya ukuu wa Mkoa. Hii ni heshima kubwa kwa vijana wa nchi yetu. Ni matumaini yangu kuwa vijana wenzetu hao hatutamuangusha mh. Rais kwa imani yake kubwa kwenu.
Pili, naomba kupongeza maelekezo yaliyotolewa na Mh. Rais wakati wa kuwaapisha wakuu wa mikoa, hasa eneo la kusimamia watu wafanye kazi na kupiga vita uzembe. Maelekezo hayo ya Mh. Rais yanabeba dhana ya kujitegemea ambayo ndio msingi wa siasa ya nchi yetu tangu uhuru. Kama kijana naunga mkono maelekezo hayo na kwamba hayana budi kushuka hadi ngazi ya chini ili vijana tubadilike na kuhamasika kufanya kazi za uzalishaji mali kama kilimo na ujasiriamali.
Wakati haya yakitokea, mmoja wa viongozi vijana wa chama kichanga cha ACT Wazalendo bwana Mchange ametoa na kusambaza maoni yake juu ya maelekezo hayo ya Mh. Rais. Bwana Mchange anahoji dhana ya vijana kuhimizwa kulima na kufanya kazi za uzalishaji mali akitumia lugha ya kumkejeli na kumbeza Mh. Rais. Nimehamasika kuandika kiasi ili kumuelimisha kijana mwenzangu Habibu Mchange.
Bwana Habibu Mchange anapomuomba Mh. Rais ampatie ardhi ya kulima hajui kuwa mamlaka za vijijini na wilaya zinaweza kutoa ardhi kwa vijana wakalima?
Au anadhani kila ardhi anatoa Rais?
Bwana Mchange anapaswa kufanya utafiti ajue juu ya jambo hili kabla ya kulivamia. Amuulize mh. Kingu alipokua DC wa Igunga vijana walipata wapi yale mashamba ya kulima kwa vikundi? Walipewa na Rais Kikwete au ni ubunifu wa Mkuu wa wilaya?
Anapaswa kujifunza pale wilaya ya Iramba ambapo mh. DC Nawanda alihimiza ufujaji wa kuku wa kienyeji kama njia ya wananchi kujikomboa kiuchumi. Je, kuku wale walitolewa na Rais?
Pengine Mchange anapaswa kuwa mkweli kuwa yeye hajui kuhusu kilimo na hajawahi kulima. Ama ni kwasababu hajakulia kwenye malezi ya wakulima na wafugaji au kwasababu amekua akiona wazazi wananunua kila kitu ikiwemo unga, mchicha, mchele, karanga, mahindi ya kuchoma na maharage. Lakini sisi tuliokulia kwenye kilimo tunamuelewa vizuri Mh . Rais.
Mh. Rais ametoa maelekezo muafaka kabisa kwa wakuu wa mikoa kuhusu vijana kufanya kazi na hasa kujishughulisha na kilimo. Katika kila mkoa yako maeneo yenye fursa nzuri za kilimo na ufugaji. Dhamira ya mh. Rais ni kuona kuwa fursa hizo za mito, mabonde, mabwawa na maziwa zinatumiwa ipasavyo kuwanufaisha wananchi wa eneo husika.
Sote tunafahamu kuwa kumekuwepo na ongezeko la vijana wanaoshinda vijiweni ambao hawataki kufanya kazi za mikono. Hawa lazima wapate msukumo wa dola.
Aidha, nimkumbushe bwana Mchange kiongozi kijana wa Chama kichanga cha ACT kuwa wakati wa kampeni mh. Rais aliwaeleza watanzania juu ya ilani ya CCM inayotoa ahadi ya mikopo ya shilingi milioni 50 kila mtaa na kijiji. Pesa hizi ni kwa ajili ya kuwasaidia wananchi kukopa na kujiajiri katika shughuli za uzalishaji mali wakiwa kwenye vikundi. Wasimamizi wa fedha hizi ni wakuu wa mikoa na wilaya.
Napenda kwenda mbele zaidi kumuelimisha bwana huyu mvivu wa kufikiri kuwa, mh. Rais hakukurupuka kutoa maagizo haya. Anatambua kuwa iko sheria inayozitaka halmashauri kutenga asilimia 5 ya mapato kwa ajili ya vijana na asilimia 5 nyingine kwa ajili ya wanawake kuwezeshwa kiuchumi. Haya yanapaswa kusimamiwa na wakuu wa mikoa na wilaya.
Kila kaya iliyo katila mazingira ya kulima inapaswa kuwa na shamba kwa ajili ya kulima mazao ya chakula. Angalau heka mbili. Hii haipaswi kuwa jambo la kubembeleza. Linapaswa kuwa amri ili tuondokane na aibu ya njaa.
Ni jukumu la Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuhakikisha mipango inawekwa ili vijana watakaounda vikundi vya kilimo wanapata pembejeo za kutosha kwa wakati ili kutekeleza maelekezo ya mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli. Kila mtu atimize wajibu wake katika kujenga taifa letu.
Ni aibu kubwa kuona kuna mtanzania anabeza juhudi njema za mh. Rais katika kuitumikia nchi yetu kwa kujenga nidhamu na kujitegemea. Mwalimu Nyerere alihimiza kilimo, na akasema kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa. Nchi yoyote haiwezi kuwa huru kama haitaweza kujitegemea kwa mahitaji ya chakula kwa watu wake.
Imeandikwa na
Ally S. Hapi
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es salaam