Rais Magufuli, tukalime wapi? Tupeni mashamba tukalime

Rais Magufuli, tukalime wapi? Tupeni mashamba tukalime

Nenda kasaidie (volunteer) kwenye Vituo vya kulea watoto Yatima au kwenye kambi za wakimbizi.
Nitalipwa? Baba yake kwakuwa nao ni wakulima na wanategemea msimu wa mvua huwa wanaenda kusaidia vituo vya watoto yatima? je hivyo vituo vinahitaji watanzania wangapi...
 
Magufuli tupatie mashamba tukalime baba, jana umeagiza tukamatwe, tupelekwe kambini tulime kwa lazima.

Hakuna haja ya kukamatwa baba, tupatie tu mashamba tutalima wenyewe, kule vijijini kila pori tunalogusa tunaambiwa la mwekezaji, kila shamba tunaloliona tunaambiwa la mheshimiwa fulani.

Hakuna mashamba ya wazi baba, hata serikali imegawa mashamba yake kwa wadosi.Tukienda kwa nguvu tunaitwa wa wavamizi baba.

Tunavamia katika nchi yetu.Tukienda kuvua samaki tunaitwa wavuvi haramu baba'Tusaidie pia na vitendea kazi, hata majembe ya ngwamba tu baba. Mbolea Na umwagiliaji tutamwachia tu Mungu ataleta neema zake baba.

Tukienda kukopa tunaambiwa tuweke dhamana ya nyumba ama kiwanja baba, tutatoa wapi hizo dhamana sisi wacheza Pool table baba?.

Waangalie na TIB na Benki ya Kilimo baba kama mikopo yao inawafaa vijana . unaowakurupusha leo!Benki zako zinawafaa zaidi wazee kukopa kuliko sisi vijana baba.

Uwakumbushe na wale vijana wa CCM baba, hawataki kulima, hataki kazi,hawataki biashara, kutwa kucha kukusifia wanasubiri uteuzi baba.

Wengine wakilala wanauota U DC, wengine wamebadilisha mpaka miondoko baba kusubiri uteuzi wako baba, wameshakosa U RC bado U DC baba.

Tafadhali sana baba usitufukuze tu bila kujua tutakapoelekea.

Yote umeandika vizuri, lakini sentensi ya mwisho ni nzuri zaidi.

TUNATAKA VIWANDA NA MILIONI HAMSINI KILA KIJIJI
 
Nitalipwa? Baba yake kwakuwa nao ni wakulima na wanategemea msimu wa mvua huwa wanaenda kusaidia vituo Vya watoto yatima au unawazat je hivyo vituo vinahitaji watanzania wangapi...
Nenda katika hizo sehemu nilizoainisha utapata habari kamili kuhusu taratibu zao. Acha kulia lia na kucheza Pool saa kumi na mbili asubuhi.
 
Ivi ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa hauna umri wa ukomo nama sasa vijana akuna ajira tunakaa kwenye pool table ingawa ni mchezo sasa bao wanataka kuukuza mchezo huo cjui tutacheza kwa style gan mpk kupata ujuzi na mpira ungechelewa kidogo kumpata samatha basi leo vijana wangekamatwa wasicheze mpira mwaka jana mchezaji bora pool table amekula hela ndefu kwa udhamini safari lager sasa cjui itakuaje kwa mwaka huu akuna tena atayekua mzur kwa table tena coz home akuna table na baa ukikutwa ndani na mpira wa miguu kwa umri wetu tena mpk kuonekana miaka 35 hiyo soko akuna na was was naweza cheza nako nikakamatwa pia badae wakitukosa kwenye table baa
 
Mashamba yapo mengi sana nchi hii acheni siasa na kilimo hakiitaji mamilioni ya pesa kuwekeza ni nia tu. Sasa mnwajaza ujinga vijana wasijishughulishe watakaa hivyo mpaka lini?

Wewe Mchange una kampuni yako na Zitto yaitwa Tetere media inatengeneza 5 gear TV show na mna gazeti lenu ni serikali ndio ilikupa hayo au ulirithi kwa wazee wako? Wanasiasa msipotoshe vijana muwape mbinu za kukikwamua. Hakuna serikali inayoweza kuajiri vijana million 20.
Una hekari ngapi na umeajiri vijana wangapi?
 
Kwani lazima kulima, kuna kazi nyingi tu,fundi viatu,kushona nguo ,kusafisha mazingira ,kulima bustani,zipo nyingi tu ambazo hauwezi amini zitakupa fedha za kutosha tu .Ninaviatu vingi tu vimefumuka hapa nimekosa fundi wa kuvitengeneza, ebu kasomee kutengeneza viatu ,utusaidie sisi wewe ajira za maana.
 
Hiyo Tanzania ya viwanda mbona mnaipotezea...
Viwanda huwa vinajengwa siku moja!? Ndio kwanza kazi imeanza. Mtamuelewa tu Mh Rais. Wakati watu makini wanafanya kazi, wengine wako kwenye Pool sasa hivi wanapambana mtandaoni kukashifu Serikali ya awamu ya tano kwa kutumia vifurushi vya Chuo.
 
Mimi kazi yangu kuchezesha pool, tayari biashara yangu ishaharibika
 
Lazima Mnyooke. Mlikuwa kumbe mnasifia utawala wa Nyerere kinafiki. Haya ya kufanya kazi kwa nguvu na kukamata Wazururaji na wazembe mjini yalikuwepo tena kulikuwa na kodi ya Kichwa lazima ulipe.
Kulikuwa na Nyimbo tunaimbishwa kukataa kuuza Njugu na korosho mitaani ikilenga kuhamasisha kilimo. Sasa tukiwa tunafanya analysis kuhusu tulioishi wakati wa Mwl mtakuwa mnaelewa lilikuwa Taifa la namna gani. Blaa blaa za kushinda mnapiga deki barabarani Mwanaume mwenzio apite hazitakuwepo. Unapishana na vijana wana headphone kubwa masikioni kama Marubani akili kichwani kama tunda za ubuyu hawana wanachowaza zaidi ya ku bet ligi kuu ya Uingereza na kucheza pool tena siku hizi hata pool table inachezwa kwa kamari.
 
Mimi kazi yangu kuchezesha pool, tayari biashara yangu ishaharibika
Hizo meza za pool badilisha matumizi yake asubuhi mpaka jioni panga mboga mboga, nyanya, vitunguu n.k ujipatie kipato huku ukiitikia wito wa Mh Rais na kuisaidia jamii. Ikifika muda wa jioni endelea na Pool lako...changamkia fursa BALKIA wa nguvu.
 
Mlimchagua mwenyewe ngoja awanyooshe miaka mitano mtakua mmenyooka alafu akiwaomba tena kura mtampa
 
Yani waafrika kuendelea kazi sana. Hivi wewe mtoa post ushawahi fanya utafiti na ukajiridhisha pasi na shaka kwamba vijana wanashinda kwenye pool table kisa mashamba yao huko kijijini yamechukuliwa na wawekezaji? Kwanini akina mama wanaangaika kwenye kutafuta chochote kile na wengi ndo unawakuta mashambani?
 
Rudi kwenu kaendeleze yale ya familia uliyowachia baba na mama yako. wazee wale nguvu tena za kulima hawana.
Unazani kila mtu kwao wana mashamba, wengine tumezaliwa nyumba za kupanga natumekulia nyumba za kupanga shamba tunasikia tu ila kwa hali ilivyo tukipewa mashamba tutajikwamua
 
ukiwa na iq ya kawaida kabisa inakutosha kujua kuwa tatizo sio pool table.
 
Back
Top Bottom