Rais Magufuli, sasa serikali ihamie Dodoma

Rais Magufuli, sasa serikali ihamie Dodoma

Dodoma ikulu ipo nzuri hawajengi ingine , wizara zote wana ofisi Dodoma ni vyema tujifunze South Africa ile miji ya biashara inaachwa iwe huru Kwa biashara na serikali inakaa kingine.
Acha kudanganya watu ni ofisi ndogo ambazo zinakuwa ni za mawaziri, naibu waziri na maktibu wakuu... ni sub office. Alafu wengine wanakodi nyumba za vyumba vitatu kama ofisi. So labda wahamie mawaziri tu...
 
Alafu ule mjengo wa magogoni ugeuzwe hosteli za watoto wa IFM! Kwa maana kodi za vyumba kigamboni zimepanda.
 
Ni wazo zuri ila nawaza utekelezaji wake.... ninavyofahamu mkuu atatumia ubabe zaidi kupeleka watu dodoma bila kuwalipa na atatengeneza madeni. Kumuhamisha mtu mmoja si chini ya milioni 10... sasa imagine wale wenye familia kubwa.
 
Ni habari njema sana lakini in ngumu sana kutekelezeka
 
sukari imemshinda,..halafu awe wa kwanza kuhamia dodoma...that can't be done sababu hata mamilioni yake ya mshahara hayakatwi kodi!!!!aache zake daslam mpango mzima
 
nakwambia hivi tamko hilo lilikuwa la mwendokasi bila kujua mda umeisha. Nakumbuka rais aliwambia TUCTA wawe wakwanza kuhamia Dodoma.
 
Majengo yote Dar yatakodishwa President naona anaangalia ukusanyaji wa pesa
 
Ni rahisi kuogelea toka Dar mpk Zenji lakini sio CCM na Serikali yake kuhamia Dodoma.

Mimi nitakuwa wa mwisho kuamini hili tamko la kuhamia Dodoma.

Its a matter of time!!
 
Hiyo itasaidiaje kuondoa umaskini wa watanzania? Naona Magu anajaribu kutekeleza kelele za upinzani bila mipango dhabiti! Anyway, basi wajaribu kuhamia, almradi hilo lisifanye maisha yetu yazidi kuwa magumu!
 
Exactly....

Inasikitisha great thinker wanasapoti kwa ushabiki badala ya kuwaza haya...
mkuu unaogopa foleni kuja mkoani kwako nini? waache wahame ili dar ubaki mji wa biashara. majengo ya serikali yageuzwe cooperate HQs. pia Dar ni moja ya fastest growing cities in Africa lazima hatua za kucurb hiyo ishu zichukuliwe. BTW zahanati tunajenga na dodoma tunahamia.
 
Faida kubwa ni kupunguza foleni jijini pia kuepusha gharama posho za kuwalipa madereva na watumishi wanaokwenda Dodoma kikazi , baada ya kuhamia watalipwa mishahara tu, faida ya pili ni kusambaza maendeleo kwenye miji ya njia kuu kuelekea Dodoma na mikoa yote itaendelea Kama ilivyokuwa south afrika, Malawi , Nigeria na India ambapo miji mikuu ipo mbali na miji ya kibiashara , hakuna hasara kabsa .
Yaani umekuja na jibu la moja kwa moja kuwa hakuna hasara kabisa. Nina kushauri ndugu ukichangia jambo usiamini maneno yako ndio msahafu.
Hasara kubwa ni ujenzi wa miundombinu ya kukidhi mahitaji ya wizara na idara za serikali, malipo kwa wafanyakazi watakaohama, kuongezeka kwa safari kati ya Dar na Dodoma maana Dar es Salaam utaendelea kuwa mji wa kibiashara kutoka na kuwa kando ya bahari ya hindi na uwepo wa ofisi nyingi za binafsi licha ya kuwa nyingine zitahama Dodoma.
Ni ndoto za alinacha za mheshimiwa Magufuli kuhamisha nchi ndani ya miaka mitano. Labda angepunguza Wizara Dar es Salaam kama elimu, mali asili, ujenzi nk
 
Watu wengi kuhamia Dodoma kutakuwa na manufaa gani?Huduma za serikali zıtakuwa zimesogea jiranı na wananchi toka pande zote za nchı.Dom ni katı.Mkulima wa ndızi na mvuvı toka Buko ataweza kufikisha bidhaa kwenye soko kwa haraka.Miji km Mwanza itapanuka kwa haraka.Uchumi wa nchi utasambaa!
 
Rais kaliongea kirahis sana hilo jambo
Japo ni zuri ila siyo rahisi
 
Dodoma ikulu ipo nzuri hawajengi ingine , wizara zote wana ofisi Dodoma ni vyema tujifunze South Africa ile miji ya biashara inaachwa iwe huru Kwa biashara na serikali inakaa kingine.
Ni kweli wizara wana ofisi Dodoma lakini zile ni ofisi ndogo
 
Hiyo itasaidiaje kuondoa umaskini wa watanzania? Naona Magu anajaribu kutekeleza kelele za upinzani bila mipango dhabiti! Anyway, basi wajaribu kuhamia, almradi hilo lisifanye maisha yetu yazidi kuwa magumu!
haiwezi ondoa umasikini ila mara nyingi serikali ikianzisha miradi mikubwa kama hii inasaidia kuboost uchumi.
 
Ni rahisi kuogelea toka Dar mpk Zenji lakini sio CCM na Serikali yake kuhamia Dodoma.

Mimi nitakuwa wa mwisho kuamini hili tamko la kuhamia Dodoma.

Its a matter of time!!
Ni rahisi kuogelea toka Dar mpk Zenji lakini sio CCM na Serikali yake kuhamia Dodoma.

Mimi nitakuwa wa mwisho kuamini hili tamko la kuhamia Dodoma.

Its a matter of time!!
ugumu uko wapi kama utashi upo? Tujifunze kuamini.unless mawazo yetu kuhusu maana ya neno serikali yawe ni zaidi ya vile nielewavyo mimi.Tukitambua serikali kwa sasa inaunda upya muundo wake ambao huenda ukawa zaidi pia ya mazoea yetu.
ila nakupongeza kwa kutoa muda hapo mwishoni.
 
Nashangaa sana vipaumbele vilivyopo....
Hivi kuhamia dodoma ni muhimu kuliko hospitali? Leo nimepita mahali kuna zahanati moja hadi huruma......

Kuna umuhimu wa kuhamia dodoma kuliko elimu ya watoto? Maabara zipo za kutosha?????

Vipi kuhusu maji? Watanzania wangapi wanapata maji safi na salama????
Aarrrghh
kuna baadhi ya mambo kwenye maisha hayasubiriani, hizo kero zikiwekewa mkakati zitapata utatuzi huku kuhamia Dodoma nako kukileta utatuzi wa changamoto nyingine. Tuiache DSM makao makuu ya kibiashara na tuifanye Dodoma makao makuu ya serikali.
 
Chonde chonde makonda RC wetu.
Wache akina matonya ,serikali ikienda Dodoma wasiyufuate au vip mwanangu?
 
Back
Top Bottom