Rais Magufuli, sasa serikali ihamie Dodoma

Rais Magufuli, sasa serikali ihamie Dodoma

Natamani ningefungua uzi huu na kukuta mjadala mzito wa faida na hasara.... Mjadala ambao ungezungumzia athari gani zitalikumba jiji la dar baada ya rwizara na serikali yote kuhamia dodoma,...Je na balozi za nchi zitahamia huko?..Ipi itakuwa athari katika uwanja wa ndege wa Dar?...Pia ni faida gani zitapatikana Dodoma na mikoa jirani, ......Tungejifunza mengi sana....Lakini kama kawa wanaJF kazi kujisifu ugreat thinker tu huku wakiongea pumba na kuhusisha siasa katika kila jambo
Hizo gharama za kuhamia dodoma heri wangeboresha hospitali na zahanati......
 
Nigeria , Malawi na south afrika baadhi ya ofisi za balozi hazipo miji mikuu wapo kwenye miji ya zamani na huduma zinapatikana kama kawaida , kwanza balozi nyindi Dsm Viza hakuna mpaka watu waombe Nairobi au south afrika , faida ni kubwa kuliko hasara .

Nashkuru ndugu Ushuzi.....Ubarikiwe na udumu milele.....Tena ulikuwa hapa pembeni yangu muda si mrefu....Naomba ujitahidi kutumia hata perfume kupunguza smell
 
Wazo zuri Dodoma ni katikati, atasaidia kusogeza huduma za serikali jirani zaidi na mikoa mingi.
Hii ya Dodoma kuwa ni katikati haina mashiko yoyote haina maana yoyote kwa karne hii. Kwanza katikati ukitokea wapi? Katika ya Tanzania reference point ni Dar es Salaaam?
Kama ni Dar es Salaam, katikati ni Manyoni!
 
Mbali na kupunguza msongamano Dar hivi bado sababu zile za kipindi cha Nyerere za kuhàmia Dodoma bado zina apply katika zama hizi?
 
Sijui itapunguzaje umaskini kwakuwa ndio adui yetu namba moja!! Tunataka hospitali za rufaa kila mkoa, vyuo vya ufundi vikubwa kila mkoa,maji,umeme,reli,viwanja vya ndege nk. Tunapaswa kuvitathmini vipaumbele vyetu kwanza kwamba nini tunahitaji kabla ya nini tunapenda!! Kuna vitu vya muhimu na vitu vya muhimu zaidi
 
Mbali na kupunguza msongamano Dar hivi bado sababu zile za kipindi cha Nyerere za kuhàmia Dodoma bado zina apply katika zama hizi?
Mkuu, nimejiuliza swali hilo. Kwa karne ya zamani ilikua sawa, kwa sasa haina maana sababu zile. Ila ina maana kwa kupunguza mrundikano wa Ofisi kama walivyofanya Nigeria, issue ya katikati haina mashiko sana.
Mimi nakubaliana suala la Serikali kuhamia Dodoma ili kuifanya Dar ipumue lakini siyo sababu ya eti ni katikati na hivyo Ulinzi na rahisi, hiyo ilikua ni zamani. Siku hizi Drone inafika popote ulipo!
 
Hii ya kuhamia Dodoma makada wa chama hawajaipenda kabisa.

Hivi unadhani hilo linawezekana? Kwa pesa gani serikali hii inayonuka madeni inazo? Kikwazo cha kuhamia Dodoma kwa miongo zaidi ya minne ilikuwa pesa, sasa wanazo? Ni Ukurupukaji tuu.
 
Baada ya Tamko la Mwenyekiti mpya wa CCM, Rais John Pombe Magufuli kuitaka serikali yake ya awamu ya tano kuhamia Dodoma kabla ya awamu yake ya kwanza ya Urais kwisha. Mamlaka ya ustawishaji, Makao makuu (CDA) ni vema sasa ikajiandaa vya kutosha kwa vitendo kuipokea serikali kwa kuongeza kasi ya kuupanga mji wa Dodoma ikiwemo kuongeza kasi ya upimaji wa viwanja katika maeneo ya pembezoni mwa mji ili kuepuka msongamano katikati ya mji pindi serikali itapohamia Dodoma.
 
Juzi tulikuwa tunajadili hili.
Na tulikuwa na mawazo hayahaya.
Nashangaa sana vipaumbele vilivyopo....
Hivi kuhamia dodoma ni muhimu kuliko hospitali? Leo nimepita mahali kuna zahanati moja hadi huruma......

Kuna umuhimu wa kuhamia dodoma kuliko elimu ya watoto? Maabara zipo za kutosha?????

Vipi kuhusu maji? Watanzania wangapi wanapata maji safi na salama????
Aarrrghh
 
Mkuu, nimejiuliza swali hilo. Kwa karne ya zamani ilikua sawa, kwa sasa haina maana sababu zile. Ila ina maana kwa kupunguza mrundikano wa Ofisi kama walivyofanya Nigeria, issue ya katikati haina mashiko sana.
Mimi nakubaliana suala la Serikali kuhamia Dodoma ili kuifanya Dar ipumue lakini siyo sababu ya eti ni katikati na hivyo Ulinzi na rahisi, hiyo ilikua ni zamani. Siku hizi Drone inafika popote ulipo!
Ndio wasiwasi wangu huo, isijekuwa tu eti kwa sababu Nyerere alisema. Nadhani serikali iwe makini sana kuangalia sababu halisi za kuhamia Dodoma
 
Dah... Itakaa poa Sana hii.... Long live JPM [emoji41] [emoji41]
 
Sijui itapunguzaje umaskini kwakuwa ndio adui yetu namba moja!! Tunataka hospitali za rufaa kila mkoa, vyuo vya ufundi vikubwa kila mkoa,maji,umeme,reli,viwanja vya ndege nk. Tunapaswa kuvitathmini vipaumbele vyetu kwanza kwamba nini tunahitaji kabla ya nini tunapenda!! Kuna vitu vya muhimu na vitu vya muhimu zaidi
Exactly....

Inasikitisha great thinker wanasapoti kwa ushabiki badala ya kuwaza haya...
 
Back
Top Bottom