Rais Magufuli, sasa serikali ihamie Dodoma

Rais Magufuli, sasa serikali ihamie Dodoma

mtasubiri mpaka yesu arudi serikali kuhamia dodoma,kwanza pesa hamna
Mkuu usemalo laweza kuwa na Ukweli kutokana na CDA kutafuna Pesa Kwa miaka mingi pasipo kutekeleza lengo, lakini magufuli kaahidi Kwa uwazi tusubirie ahadi yake Kwa vitendo, ni ahadi nzuri kuliko zote alizowahi kuziahidi kutokana ni ahadi yenye kupunguza kero na foleni jijini Dsm sanjari na kusambaza maendeleo mikoani .
 
safi sana. lazima tuwe tunajiwekea commitment na kuwa results oriented.

stock-vector-tanzania-political-map-political-map-of-tanzania-with-the-capital-dodoma-national-borders-most-151269227.jpg

Ramani ya Tanzania haina ziwa Nyasa.? Au umetumwa Na Malawi.?
 
Wakati huu wa science na technologia bado kuna haja ya kuhamia Dodoma. Ni faida zipi tutapata kwa serikali kuhamia Dodoma?
 
J

Kama serikali ndiyo ilikuwa inasababisha jam, ina maana jam sasa itahamia Dodoma, kisha watapendekeza serikali ihamishiwe Mpanda au Mbozi ambako kutakuwa hakuna jam (wakati huo). jam husababishwa na matatizo ya miji kukosa mpangilio tu.
Dodoma patapangiliwa mapema kutokana na kutokuwa na uswahili kubwa ni rahisi kupanua barabara kirahisi na kujenga miundo mbinu kuliko Dsm ambayo imebanwa na nyumba za uswahilini
 
Faida kubwa ni kupunguza foleni jijini pia kuepusha gharama posho za kuwalipa madereva na watumishi wanaokwenda Dodoma kikazi , baada ya kuhamia watalipwa mishahara tu, faida ya pili ni kusambaza maendeleo kwenye miji ya njia kuu kuelekea Dodoma na mikoa yote itaendelea Kama ilivyokuwa south afrika, Malawi , Nigeria na India ambapo miji mikuu ipo mbali na miji ya kibiashara , hakuna hasara kabsa .

1. Kama serikali haiko Dodoma (sasa hivi) hao watumishi wanakwenda Dodoma kufanya nini?

2. Kama ni suala la bunge, kwa nini shughuli za bunge zisihamishiwe Dar au Kibaha? Hiyo itakuwa cheap kuliko kuanza kujenga 'white house' nyingine Dodoma...pamoja na maofisi yote yaliyopo sasa kuya-duplicate huko Dodoma

3. Suala la jam ni la mipango miji. Kama miundombinu ya barabara ingekuwa bora nina hakika tusingekuwa na jam Dar. Juzi nimetembelea Dar kidogo na sikukumbana na ile jam ya siku zote Morogoro road.

4. Kuhusu hilo la kusambaza maendeleo nitahitaji msaada wa ufafanuzi, maana ninachojua serikali na wadau wa sekta binafsi wana jukumu la kuchochea maendeleo nchi nzima kuanzia Dar, Ukerewe, Mlele, Karema, Nachingwea, Tunduru, Marangu, Kihesa, Dodoma, Nyakanazi, Tarime na kwingineko sawa sawia.
 
Brilliant idea..ingawa kiusalama haijakaa sawa
Kiusalama Dsm ipo vibaya kuliko Dodoma kumbuka ikulu ipo jirani na Bahari ni rahisi Adui kupenya Kwa kutumia nyambizi ,Usalama Dodoma upo wa kutosha na endapo serikali itahamia jumla ina maana Usalama utaimarishwa zaidi .
 
1. Kama serikali haiko Dodoma (sasa hivi) hao watumishi wanakwenda Dodoma kufanya nini?
2. Kama ni suala la bunge, kwa nini shughuli za bunge zisihamishiwe Dar au Kibaha? Hiyo itakuwa cheap kuliko kuanza kujenga 'white house' nyingine Dodoma...pamoja na maofisi yote yaliyopo sasa kuya-duplicate huko Dodoma
3. Suala la jam ni la mipango miji. Kama miundombinu ya barabara ingekuwa bora nina hakika tusingekuwa na jam Dar. Juzi nimetembelea Dar kidogo na sikukumbana na ile jam ya siku zote Morogoro road.
4. Kuhusu hilo la kusambaza maendeleo nitahitaji msaada wa ufafanuzi, maana ninachojua serikali na wadau wa sekta binafsi wana jukumu la kuchochea maendeleo nchi nzima kuanzia Dar, Ukerewe, Mlele, Karema, Nachingwea, Tunduru, Marangu, Kihesa, Dodoma, Nyakanazi, Tarime na kwingineko sawa sawia.
Dodoma ikulu ipo nzuri hawajengi ingine , wizara zote wana ofisi Dodoma ni vyema tujifunze South Africa ile miji ya biashara inaachwa iwe huru Kwa biashara na serikali inakaa kingine.
 
Masikini kwetu Rufiji sasa tutakuwa mbali na wadosi wa nchi, tulishazoea wenyewe kwenda na kurudi Dar yetu!
Usihofu. Beijing ni mji mkuu, lakini umezidiwa na Shanghai japo sio kwa mbali sana. Abuja ni mji mkuu lakini umeachwa mbali na Lagos, J'Burg iko vizuri kuliko Mji mkuu wa South Africa. Washington haiifikii New York City na New York State as a whole
 
Natamani ningefungua uzi huu na kukuta mjadala mzito wa faida na hasara.... Mjadala ambao ungezungumzia athari gani zitalikumba jiji la dar baada ya rwizara na serikali yote kuhamia dodoma,...Je na balozi za nchi zitahamia huko?..Ipi itakuwa athari katika uwanja wa ndege wa Dar?...Pia ni faida gani zitapatikana Dodoma na mikoa jirani, ......Tungejifunza mengi sana....Lakini kama kawa wanaJF kazi kujisifu ugreat thinker tu huku wakiongea pumba na kuhusisha siasa katika kila jambo
 
Tena China Kila miji umejengeka huwakuti kulundika mji mmoja Kama Tanzania , hivyo hivyo ulaya nk
 
Wazo zuri Dodoma ni katikati, atasaidia kusogeza huduma za serikali jirani zaidi na mikoa mingi.
 
Hii itakua move nzuri kwa wana Dodoma na Dar pia. Dar ubakie mji wa kibiashara na Dodoma makao makuu ya serikali.
 
Natamani ningefungua uzi huu na kukuta mjadala mzito wa faida na hasara.... Mjadala ambao ungezungumzia athari gani zitalikumba jiji la dar baada ya rwizara na serikali yote kuhamia dodoma,...Je na balozi za nchi zitahamia huko?..Ipi itakuwa athari katika uwanja wa ndege wa Dar?...Pia ni faida gani zitapatikana Dodoma na mikoa jirani, ......Tungejifunza mengi sana....Lakini kama kawa wanaJF kazi kujisifu ugreat thinker tu huku wakiongea pumba na kuhusisha siasa katika kila jambo
Nigeria , Malawi na south afrika baadhi ya ofisi za balozi hazipo miji mikuu wapo kwenye miji ya zamani na huduma zinapatikana kama kawaida , kwanza balozi nyindi Dsm Viza hakuna mpaka watu waombe Nairobi au south afrika , faida ni kubwa kuliko hasara .
 
Kama endapo magufuli ataitekeleza ahadi hii Kwa vitendo Nina hakika mengi aliyoyaahidi atatatekeleza maana huu ni mfupa uliowashinda wengi sana.
 
Back
Top Bottom