1. Kama serikali haiko Dodoma (sasa hivi) hao watumishi wanakwenda Dodoma kufanya nini?
2. Kama ni suala la bunge, kwa nini shughuli za bunge zisihamishiwe Dar au Kibaha? Hiyo itakuwa cheap kuliko kuanza kujenga 'white house' nyingine Dodoma...pamoja na maofisi yote yaliyopo sasa kuya-duplicate huko Dodoma
3. Suala la jam ni la mipango miji. Kama miundombinu ya barabara ingekuwa bora nina hakika tusingekuwa na jam Dar. Juzi nimetembelea Dar kidogo na sikukumbana na ile jam ya siku zote Morogoro road.
4. Kuhusu hilo la kusambaza maendeleo nitahitaji msaada wa ufafanuzi, maana ninachojua serikali na wadau wa sekta binafsi wana jukumu la kuchochea maendeleo nchi nzima kuanzia Dar, Ukerewe, Mlele, Karema, Nachingwea, Tunduru, Marangu, Kihesa, Dodoma, Nyakanazi, Tarime na kwingineko sawa sawia.