Rais Magufuli: Mpaka sasa Tanzania (Bara&Visiwani) hatuna mgonjwa wa Corona. Nawasihi watanzania kuchukua hadhari

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,976
Rais Magufuli ameishukuru serikali ya Germany kwa msaada walioutoa kujenga karakana hiyo ya kisasa.
Pia Rais Magufuli amempa balozi barua maalumu ya shukrani kwa counvillor Mikael wa Germany.

Kadharika Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kuwataka watanzania wajihadhari na ugonjwa huo hatari.
Rais Magufuli amevitaka vyombo vyote vya habari kutoa elimu kuhusu corona.
Kadhalika amewataka wananchi kutosafiri hovyo na amemuagiza CS kutotoa vibali vya kusafiri kwa safari zisizo muhimu.

Rais Magufuli amesisitiza hata ndege ya ATCL inayofanya safari za India ikirejea kesho haitasafiri tena kwenda huko.

Maendeleo hayana vyama!

----------
Kupitia hii hotuba yangu ya leo naomba tu watanzania wote mkachukue tahadhari kila mmoja kujikinga na ugonjwa wa Corona, upo na ni hatari unaua kwa haraka. Tanzania bara na Visiwani hakuna mgonjwa ila haina maana kwamba tusichukue tahadhari.

Niwaombe ndugu zangu tusipuuze ugonjwa huu. Kwa wale wanaopenda kusafiri safiri sana, kama safari sio ya lazima sana usisafiri. Nimeshatoa taarifa kwa Katibu Mkuu Kiongozi kwamba vibali vya kusafiri viwe kwa safari maalum

Tusishikane mikono, tusibusuane, sasa sifahamu usiku watafanyaje, lakini napo unaweza tu usibusu mambo yakawezekana na ni raha tu.

rAIS.jpg

Na hii tahadhari msiwaachie viongozi tu ndio wazungumze,kila mmoja kwenye familia yetu tutoe elimu ya tahadhari. mashuleni walimu watoe tahadhari kwa watoto wetu, kwenye makambi etc ili tuweze kudhibiti hili gonjwa lisiweze kuingia nchini mwetu, gonjwa hili linaharibu uchumi wetu.

Niwaombe wahariri wa magazeti ikiwezekana kila siku kwenye gazeti watoe tahadhari ya ugonjwa wa Corona. Kwenye Tv na redio zetu hata kabla ya kutangaza taarifa ya habari basi wapitishe mistari ya tahadhari ya ugonjwa huu. Tukidharau ndugu zangu tutakwisha, mpaka sasa wanatibu tu symptoms lakini dawa ya kuponesha Corona haipo. Kupitia meseji hii ambayo naitolea hapa jeshini Lugalo ikawaguse watanzania.

Vyombo vya habari mkilisimamia hili tutashinda hii vita, unapopiga Muziki weka na tangazo la corona ili anaecheza na kubinuka amevaa kichupi anaweza akavaa hata gauni kwa kusikia tu neno corona, wekeni Dakika hata moja ya kuelimisha, Wanahabari hili ni jukumu lenu kubwa

Niwaombe viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali kila mmoja katika imani yake tuendelee kumuomba Mungu aweze kutusaidia, Mungu anaweza kila kitu.Hata wakati wa Sodoma na Gomora tahadhari zilitolewa Watu walidharau wakaangamia, tahadhari tuzizingatie,Nchi zimepunguza safari hata sisi Ndege yetu inayoenda India ilienda jana ikirudi leo haitoenda tena. Nchi yetu inaenda vizuri kiuchumi, janga hili litaturudisha nyuma.
 
Karibu.

Unaweza pia kuona kupitia Channel ten tv na ITV.

Up dates;

Maendeleo hayana vyama!
Nalo JWTZ limetoka kuwa jeshi la kupambana na maadui wanotoka nje ya mipaka yetu badala yake limekuwa kama TBA. Maana siku hizi zabuni za ujenzi za Serikali ni kati ya TBA, NHC na JW au SUMA JKT.

Ikitokea vita kwa sasa hatana Burundi au Malawi sidhani kama tuna uwezo wa kuwakabili. kwa wapiganaji tulio nao pale. Wamejaa wafundi mchundo na mafundi uashi tu.
 
Eti mnaweza msibusiane mambo yakawezekana na ikawa raha tu. Interesting.
 
Karibu.

Unaweza pia kuona kupitia Channel ten tv na ITV.

Up dates;
Rais Magufuli ameishukuru serikali ya Germany kwa msaada walioutoa kujenga karakana hiyo ya kisasa.
Pia Rais Magufuli amempa balozi barua maalumu ya shukrani kwa counvillor Mikael wa Germany.

Kadhalika Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kuwataka watanzania wajihadhari na ugonjwa huo hatari.
Rais Magufuli amevitaka vyombo vyote vya habari kutoa elimu kuhusu corona.
Kadhalika amewataka wananchi kutosafiri hovyo na amemuagiza CS kutotoa vibali vya kusafiri kwa safari zisizo muhimu.

Rais Magufuli amesisitiza hata ndege ya ATCL inayofanya safari za India ikirejea kesho haitasafiri tena kwenda huko.

Maendeleo hayana vyama!
Kingine kikubwa zaidi ni kuwa ametoa tahadhai ya virusi vya Korona kwa msisitizo wa hali juu sana, yaani mpaka anawabembeleza watu kujihami kwa msisitizo mkubwa sana. Pia ametoa wito kwa vyombo vya habari na Viongozi wa dini, kushiriki kikamilifu katika kuwaweka watu kwenye tahadhari stahiki na zaidi Viongozi wa Dini kufanya mamobi pia. Amtahadharisha katika namna ambayo inabdi kwa kweli tuchukua tahadhari ya kutosha. Kwa wale waliobahatika kumsikiliza, nadhani wananielewa
 
Back
Top Bottom