Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Wiaslamu tumechelewa katika hilo.Hatuna jeuri wala ujasiri wa kulikemea hilo leo.Reginald Mengi alifuatwa na akachangia misikiti mingi wakati wa Mwinyi.Juzi Kigoma Diamond Platinum,mwanamuziki (haramu katika Uislamu,Mzinzi (kwa ushahidi wa kuwa na watoto nje ya ndoa)kajenga msikiti n akaukabidhi huku akiambatana na kimada.
Hospitali za Misheni zinatibia watu wote bila kubagua.
Kwa hili,msimlaumu JPM amefanya kile kilichomsukuma kukifanya.
Waislamu tujitafakari.
Nalo neno, aisee
 
Unaweza kuwa sahihi au sio sahihi,lengo lilikuwa sio baya tatizo liko kwa wafanyiwa 😊wako very sensitive na dini yao wenyewe 😀😀😀 utadhani itawapa ufalme wa mbingu kumbe ni mambo ya duniani tu
 
Nadhani Rais alichokifanya, kwenye hili, hakuwa sawa, labda kama alikuwa amewasiliana na wakuu wa imani ya Kiislam na wakuu wa Kanisa.

Ujenzi wa msikiti ni sehemu ya ibada kwa Waislam, japo siujui uislam kikamilifu lakini nimeishi na waislam, na nina ndugu waislam.

Hivi Rais Magufuli anajua kuwa kwa Waislam, mathalani muislam akawa ameoa mke ambaye siyo muislam, ikifika wakati wa mfungo, mwanaume yule hawezi kufuturu chakula kilichoandaliwa na yule mke ambaye siyo muislam?

Sasa huu msikiti uliojengwa na watu wasioamini kwenye uislam, kuna uhakika gani waislam hawatauona una mapungufu kiimani? Maana msikiti siyo shule au hospitali. Ile ni nyumba ya kuabudia ambayo inastahili kuwa safi kwa misingi ya imani ya wahusika.

Watanzania tunapendana, tunashirikiana lakini kwenye imani kuna mipaka yake. Ni hizo tofauti ndiyo zinazotufanya tuwe na dini na madhehebu tofauti.

Kwa mfano, kiongozi wa dini ya kikristo jukumu lake kubwa ni kuwavuta wanadamu wote wamjue kristo na wabatizwe. Hilo ndilo jukumu alilolitoa Kristo baada ya kufufuka kwake, "Enendeni Ulimwenguni kote, mkawafundishe na kuwafanya wanafunzi wangu. Mkawabatize kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu".

Sasa unapoitisha mchango katikati ya ibada kwaajili ya ujenzi wa msikiti wala siyo hospitali au shule, unafanya kazi ya kuwavuta wanadamu wote kwenda kwa Kristo au unataka wabakie nje ya Kristo? Hapa hoja yangu ni katika msingi wa imani.

Ile Ijumaa Kuu wakati wa ibada, kwenye ile sala Kuu, wakatoliki huwa tunasali:

"Tunawaombee nao waislam ili waweze kumjua Kristo na Kumkiri .........; tuwaombee nao wayahudi..........".

Sasa kiimani wewe Askofu, ukiwa ndani ya ibada, ukafanya kazi ya kuomba sadaka ya kwenda kujenga msikiti au hekalu, unakuwa unafanya hiyo kazi aliyoiagiza Kristo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu rais, wewe ni Rais siyo sheikh, wewe ni Mkiristu siyo Muislamu, mambo ya Waislamu waachie Waislamu wenyewe!

Una haki ya kuchangisha fedha kwa ajili ya matendo ya imani yako lakini huna haki ya kusimama ndani ya nyumba ya imani yako kudictate kipi kifanywe kwa niaba ya watu wa imani nyingine.

Waislamu wana taratibu zao za kujenga nyumba za Ibada zao, wanachangia wao wenyewe au wanatafuta mfadhili wa imani yao wao wenyewe, au wanafanya kwa kufuata taratibu za dini yao, kisha wanajenga msikiti wao!

Umewahi kusikia wapi Waislamu nchini wameendesha harambee makanisani kwa ajili ya kupata pesa kwa ajili ya kujenga misikiti yao? Au unafikiri Waislamu hawana marafiki Wakiristo wakiwemo maaskofu na mapadre ambao wangeweza kuwaomba wawafanyie harambee wajenge hizo nyumba?

Au lini umewahi kusikia maaskofu na mapadre wameomba michango kupitia misikitini ili Waislamu wachangie ujenzi wa makanisa?

Kuna mambo ni boundary ya kuheshimiana kiimani, nayo ni kutokuingiliana katika namna kila imani inavyoendesha mambo yake!

Najua pengine kibinadamu uliona aibu kutokana na mihela mirefu unayoimwaga makanisani siku hizi kwa jina la sadaka, ukahisi labda umma wa Waislamu utakuona kama mtu anayetumia mafungu yale ya urais yasiyokaguliwa na yeyote kwa ajili ya sadaka hizo, mimi nasema usihofu, maadamu wewe ni Mkatoliki na Mkiristu basi usiuonee haya Ukiristo wako wewe toa tu, Waislamu wanajiweza, wanaweza kujenga misikiti yao wao wenyewe na infact misikiti nchi hii ni mingi kwelikweli na imejengwa na Waislamu wao wenyewe!

Kuhusu misikiti iliyojengwa na Wafalme na marais, hiyo Waislamu tunajua huwa wanatafuta hao wafadhili wao wenyewe, ila sasa kwa kuwa Kiprotokali jambo linalofanywa na mfalme au rais wa Taifa moja katika jingine lazima mfalme au rais wa taifa husika awe na taarifa ndiyo maana taasisi za dini zinaweza kukujulisha ili usaidie kunyoosha mambo! Hii ni tofauti na kwenda kanisani ukaanzisha harambee ya kujenga misikiti! Ndugu Rais ulitumwa au kuombwa na Muislamu gani kutaka kujenga msikiti kupitia fedha za kanisani?

Wakati mwingine naangalia haya mambo na kuona kuwa yamekaa kisiasa. Hata hivyo mambo ya dini ni sensitive sana si vizuri kuchanganya dini na siasa! Mwalimu alionya sana kuhusu mambo haya!

Ipo namna mtu asiye muislamu anavyoweza kuguswa na kuamua kujenga msikiti, kwa mfano, Mwalimu aliguswa moyoni mwake baada ya kustaafu uraisi akaamua kutafuta fedha za kujenga Msikiti Butiama, Mwalimu alikuwa na connection za Vatican, Makanisa makubwa makubwa lakini hakwenda kutafuta fedha makanisani ili ajenge msikiti, Mwalimu alikwenda kwa Ghadafi ndiye aliyempa pesa za kujenga Msikiti huko Butiama!

Nimkumbushe tu ndugu Magufuli kuwa, dini ya Kiislamu pia imeweka misingi ya aina gani ya misikiti inafaa kuswaliwa ndani yake, Quran inasema ile misikiti iliyojengwa kwa dhamira safi ndiyo misikiti ya Mungu na ndiyo inayofaa kuswaliwa bali ile iliyojengwa kwa dhamira isiyo njema, yenye malengomalengo fulani hivi hiyo haina baraka za Mungu na haifai kuswaliwa ndani yake!

Nashauri Ndugu Rais awe makini sana na haya mambo ya dini, haya ni mazito sana, akiyakosea yataiweka heshima nzima ya taasisi ya urais rehani halafu kuja kurekebisha taswira hiyo inaweza kutumia gharama kubwa.

MAMBO YA WAISLAMU WAACHIWE WAISLAMU WENYEWE. NDUGU RAIS FANYA YALE YA IMANI YAKO AU YALE UTAKAYOOMBWA UFANYE KAMA UKIPENDA!
waislamu tutakuwa wajinga kama tutapokea hela za MAKAFIRI, mtume mohamad swalah alah wataal hapendi kujichanganya na wapagani, watu wasiomjua mungu, watu wala nguruwe, watu wa shari , hapanaa, tungine, fedha zao tuwarudishie.
 
Sijui mantiki ya hili. Kama dhana ni hiyo basi wengi wamekosea kuwasaidia Waislam, kuanzia Mkapa kwa kuchangisha michango ya kujengea msikiti, majengo ya umma kuruhusu kutumiwa na waislam. Unapokuwa na mtu unanafasi ya kuwasaidia wengine kutumia kujuana kwako na watu wenye uwezo sioni kosa. Ndivyo alivyofanya marehemu Mengi. Si kweli mtu kutoa msaada kwa jamii ni pesa yake, ni udhamini wa watu wengi. Kama ni utamaduni uliokuwa haujazoeleka inabidi muuzoee. Rais alikuwa Kanisani na waumini wa dini mbalimbali na walichangia.
 
Kuchangisha hela ya kujenga misikiti makanisani,mliona wapi hii kali ya mwaka.
Ukisikia kuzeeka na kupotelewa na akili ndio huku ,CCM imeshapoteza akili ni hatari kuipa kura ya ndio ili iweze kutawala zaidi,WaTz amkeni si shwari tena.
Unapozeeka sana ,midomo haiweki maneno sawa mikono inatetemeka na ni hatari kwa Taifa,CCM imetosha tunakupa hongera kwa kutuwezesha kutupatia uhuru hadi leo imetosha.
 
Msikiti haujengwi na pesa ya kafiri
 
Ndugu rais, wewe ni Rais siyo sheikh, wewe ni Mkiristu siyo Muislamu, mambo ya Waislamu waachie Waislamu wenyewe!

Una haki ya kuchangisha fedha kwa ajili ya matendo ya imani yako lakini huna haki ya kusimama ndani ya nyumba ya imani yako kudictate kipi kifanywe kwa niaba ya watu wa imani nyingine.

Waislamu wana taratibu zao za kujenga nyumba za Ibada zao, wanachangia wao wenyewe au wanatafuta mfadhili wa imani yao wao wenyewe, au wanafanya kwa kufuata taratibu za dini yao, kisha wanajenga msikiti wao!

Umewahi kusikia wapi Waislamu nchini wameendesha harambee makanisani kwa ajili ya kupata pesa kwa ajili ya kujenga misikiti yao? Au unafikiri Waislamu hawana marafiki Wakiristo wakiwemo maaskofu na mapadre ambao wangeweza kuwaomba wawafanyie harambee wajenge hizo nyumba?

Au lini umewahi kusikia maaskofu na mapadre wameomba michango kupitia misikitini ili Waislamu wachangie ujenzi wa makanisa?

Kuna mambo ni boundary ya kuheshimiana kiimani, nayo ni kutokuingiliana katika namna kila imani inavyoendesha mambo yake!

Najua pengine kibinadamu uliona aibu kutokana na mihela mirefu unayoimwaga makanisani siku hizi kwa jina la sadaka, ukahisi labda umma wa Waislamu utakuona kama mtu anayetumia mafungu yale ya urais yasiyokaguliwa na yeyote kwa ajili ya sadaka hizo, mimi nasema usihofu, maadamu wewe ni Mkatoliki na Mkiristu basi usiuonee haya Ukiristo wako wewe toa tu, Waislamu wanajiweza, wanaweza kujenga misikiti yao wao wenyewe na infact misikiti nchi hii ni mingi kwelikweli na imejengwa na Waislamu wao wenyewe!

Kuhusu misikiti iliyojengwa na Wafalme na marais, hiyo Waislamu tunajua huwa wanatafuta hao wafadhili wao wenyewe, ila sasa kwa kuwa Kiprotokali jambo linalofanywa na mfalme au rais wa Taifa moja katika jingine lazima mfalme au rais wa taifa husika awe na taarifa ndiyo maana taasisi za dini zinaweza kukujulisha ili usaidie kunyoosha mambo! Hii ni tofauti na kwenda kanisani ukaanzisha harambee ya kujenga misikiti! Ndugu Rais ulitumwa au kuombwa na Muislamu gani kutaka kujenga msikiti kupitia fedha za kanisani?

Wakati mwingine naangalia haya mambo na kuona kuwa yamekaa kisiasa. Hata hivyo mambo ya dini ni sensitive sana si vizuri kuchanganya dini na siasa! Mwalimu alionya sana kuhusu mambo haya!

Ipo namna mtu asiye muislamu anavyoweza kuguswa na kuamua kujenga msikiti, kwa mfano, Mwalimu aliguswa moyoni mwake baada ya kustaafu uraisi akaamua kutafuta fedha za kujenga Msikiti Butiama, Mwalimu alikuwa na connection za Vatican, Makanisa makubwa makubwa lakini hakwenda kutafuta fedha makanisani ili ajenge msikiti, Mwalimu alikwenda kwa Ghadafi ndiye aliyempa pesa za kujenga Msikiti huko Butiama!

Nimkumbushe tu ndugu Magufuli kuwa, dini ya Kiislamu pia imeweka misingi ya aina gani ya misikiti inafaa kuswaliwa ndani yake, Quran inasema ile misikiti iliyojengwa kwa dhamira safi ndiyo misikiti ya Mungu na ndiyo inayofaa kuswaliwa bali ile iliyojengwa kwa dhamira isiyo njema, yenye malengomalengo fulani hivi hiyo haina baraka za Mungu na haifai kuswaliwa ndani yake!

Nashauri Ndugu Rais awe makini sana na haya mambo ya dini, haya ni mazito sana, akiyakosea yataiweka heshima nzima ya taasisi ya urais rehani halafu kuja kurekebisha taswira hiyo inaweza kutumia gharama kubwa.

MAMBO YA WAISLAMU WAACHIWE WAISLAMU WENYEWE. NDUGU RAIS FANYA YALE YA IMANI YAKO AU YALE UTAKAYOOMBWA UFANYE KAMA UKIPENDA!
Ni rahisi tu, rudisheni hiyo michango iliyochangwa kanisani ili ifanye kazi zingine za maendeleo ya kanisa pale Chamwino
 
Hapo ni kama amewadharau waisilamu na kuwafanya Matonya. Kama alitaka kuchangia msikiti si ni bora angeenda huko huko msikitini aitishe harambee, kisha awapigie simu matajiri wachangie kwa kumuogopa? Na hela isipotosha akatoe hazina. Anasakwa kura kwa mbinu za kizee.
 
Huko Ulaya, waislamu wenyewe waliomba!

It came from the muslims themselves for what they thought is better for them, not otherway around!
Hapo tofauti yake ni nini?, Kuchangiwa kujenga msikiti na kuruhusiwa kuswalia kanisani?. Tatizo kubwa ni kuwa tunapokea mapkeo ya chuki na kusahau historia nzuri ya ushirikiano baina ya ukristu na uislam.

Pitia historia ya madhehebu yaha vizuri utagundua kuwa waliokuletea dini yako hawakuwa na chuki baina ya faith nyingine. Nenda mji mkongwe Zanzibar uone jengo moja la msikiti na kanisa, nenda Jerusalem pia kuna hekalu la namna hiyo. Rais amefanya hivyo kwakuwa anafanya kazi na waislam masaa 24 na hakuna msikiti eneo lile
 
Maoni yako ni sahihi ila jitahidi kupanua uelewa wako. Few months ago huko ujerumani waislam waliwaomba wakristu wawaruhusu waislam kufanya ibada ya ijumaa kanisani kwakuwa misikiti ilikuwa midogo kuruhusu social distancing because of covid. Waislam waliswalia kanisani
Ujerumani???

Sasa ujerumani ndio nini??? Nenda rudia Qur an 09:107
 
Back
Top Bottom